Wa ukweli? hatahitaji pesa? Unajua ni hivi hakuna mnachoshangaa,hao wasichana ni kielelezo kimojawapo cha ukosefu wa ajira,unajua baadhi ya hao mabinti ni wasomi kabisa! Ila kungekuwa na utaratibu wa kueleweka wa kuongeza ajira nadhani hiyo adha usingeipata.Ingawa kwa Waafrica bado wamekariri kuwa mwanaume ndo wajibu wake,unaweza kukutana na mtoto wa kike anafanya kazi bt anaomba huyoo.........
Pili kwa maisha yalivyo hapa dar maisha ni magumu bila pesa,kwa kimtazamo KISOSHOLOJIA kuna matatizo mengi sana ya kijamii-social problems.MI NASHAURI USIMSHANGAE HUYO BINTI,KUNA SABABU NYINGI NYUMA YA PAZIA EBU FUNUA PAZIA KWENYE FIKRA ZAKO UMSAIDIE.Huwa namshangaa kamanda moja wa polisi alikuwa anawakamata mabinti wanaouza miili yao.Viongozi wetu wangekuwa serious wangedili na core issues zinazowakabili wananchi si kudili na matokeo hasi yakutowajibika kwao.Binafsi siungi biashara ile lakini nachukulia kila tatizo kwa upana wake hasa kwa kufikirisha kichwa kuhusu cause-effect ya kitu chochote,ingawa kuna wengine wanafanya si kwa sababu matatizo lakini si wengi kiasi hiki!