Madeni bado shida kubwa kwangu

kirisha

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2017
Posts
573
Reaction score
663
Niliomba ushauri huku mkanipa vizuri kabisa nikaenda kufanyia kazi.

Nilifanikiwa kupunguza deni kwa mtu mmoja ila bado deni langu kubwa sana.

Alafu mzigo dukani umeshuka sana mwezi wa kwanza napaswa kulipa kodi na pia Kuna watu napaswa kuwalipa madeni yao.

Hapa nipo njia panda kabisa sijui nifanye aje ili nitoke kwenye hii changamoto.

Naombe mawazo yenu.
 
Kitu ambacho naogopa kabisa ni kukopa !!!. Ila wakati mwingine inabidi kukopa maana there is no way out. Kazi inakuja wakati unapofika wa kurudisha deni!! Namshukuru Mungu nimeondokana na hili tatizo baada ya kupata kazi yenye maslahi bora zaidi kuliko ile ya awali. Pole ndugu.
 
Yani akili imeganda kabisa
Jaribu kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
Mfano kama ulikuwa unatumia 10000 kwa siku tumia 5000. Jinyime na kama una familia piga moyo konde warudishe kwenye maisha ya kawaida. Anza kusave ukipata hela ya kueleweka ata kidogo punguza deni. Binafsi ndiko nlikotoka huko nmefata huo ushauri huu mwaka umekuwa mgumu kwangu lakin mpaka inafika December naona nina amani sana na naweza fanya maendeleo makubwa zaidi.
Pia tafuta kitu kingine cha kukuingizia faida, kiwe kidogo au cha aibu fanya ili mradi huvunji sheria za nchi
 
Pole sana mkuu. Ushauri wangu ni 1.kuachana na madeni
2.Kuuza asilimia fulani ya umiliki kwa mtu(mwekezaji)(niko tayari)
3.Kuuza biashara yote(niko tayari)
 
Pole sana mkuu. Ushauri wangu ni 1.kuachana na madeni
2.Kuuza asilimia fulani ya umiliki kwa mtu(mwekezaji)(niko tayari)
3.Kuuza biashara yote(niko tayari)
Vizuri Mkuu achukue ushauri wako, ila pia kama unakakazi kokote mkuu hata ka day work nahitaji pia, au kama unajua mahali naweza kupata kazi unaweza niunganisha pia, soma posted post yangu nimeweka maelezo yangu yote.
 
Vizuri Mkuu achukue ushauri wako, ila pia kama unakakazi kokote mkuu hata ka day work nahitaji pia, au kama unajua mahali naweza kupata kazi unaweza niunganisha pia, soma posted post yangu nimeweka maelezo yangu yote.
We jamaa posted Post ni kitu gan!!?
 
Pole sana mkuu dah hivyo ndivyo watu hupata magonjwa ya moyo

Hebu jaribu haya,
1😱ngea na mtu/taasisi inayokudai waeleze ukweli ulivyo, kisha waombe wakusogezee mbele au wakupunguzie kias unachtakiwa kurejesha sambamba na kukuongezea muda usio na ongezeko la riba endapo watakubali
Bana matumizi uwezavyo Ili uweze kurejesha kias Fulani baada ya muda utajikuta umepunguza deni kabisa

2:ikiwa una baadhi ya vitu ambavyo huvitumii/umeviweka store baada ya kununua vipya uza kapunguze deni

Mfano
TV
Kabati,
Redio
Vitanda
Nk
Uza unakaa na mavitu kibao na unadaiwa uza

3; kama huna hiyo namba mbili
Uza asset ambazo unatumia mfano friji kabati
Redio na utanunua vingine baadae


Ni hayo tu


ONYO

Epukeni kukopa kwenye sacos za mtaani nenden kwenye taasisi zinazoeleweka
Sacos za mtaani ni maumivu na hawana Sheria inayowasimamia au kuwalimit wanaweza kukuongezea riba muda wowote wanaotaka hasa unapopitisha muda wa rejesho


Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…