Madeni makubwa yalazimisha Gazeti la Jamhuri kusitisha uchapishaji na usambazaji

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
KUTOCHAPISHWA GAZETI LA JAMHURI​

Jana Jumanne Desemba 30, 2025 kampuni yetu ya Jamhuri Media Limited ilishindwa kuchapisha na kusambaza gazeti letu la uchunguzi la JAMHURI. Tukio hili la kusikitisha limetokana na kampuni yetu kuwa na deni kubwa la uchapaji na kimsingi tumejikuta hatuna fedha za kuchapisha na kusambaza gazeti hili.

Tumeona tuliweke wazi suala hili na tutumie fursa hii kuwaomba wadau tuliotangaza nao ikiwamo serikali na taasisi zake kutulipa madeni yetu ambayo ni zaidi ya Sh milioni 300, tupate nguvu ya kiuchumi itakayoturejesha kutoa huduma ya habari kwa wananchi kama ilivyo kusudio letu la msingi la kuanzisha Gazeti la JAMHURI.

Tunaendelea kufanya kila mbinu kuhakikisha tunapata nguvu za kiuchumi haraka, tulipe deni kwa mchapishaji, kisha turejee kuendelea na kazi yetu ya msingi ya kuhabarisha jamii.

Tunawaomba radhi wasomaji wetu mnaotupigia kuuliza kulikoni hamlioni gazeti. Suala hili la kusikitisha limekuwa nje ya uwezo wetu, kwani kwa muda sasa tumekuwa tukijiendesha kwa ugumu uliopitiliza. Tunawathamini wasomaji wetu, tunapambana kurejee sokoni.

Pia Soma: Gazeti la Jamhuri halionekani leo mitaani baada ya kuandika habari za Warioba, kulikoni?

1767172399195.png
 
Ukiachana na suala la madeni makubwa kinachowapa wakati mgumu ni ukuaji wa teknolojia,siku hizi kila mtu taarifa anazipata mitandaoni wale wachache (wasiokuwa na uwezo wa simu janja) ambao ingetegemewa wawaunge mkono wanawakataa kwa sababu taarifa zenyewe zinazoandikwa humo zimechujwa pamoja na kuandika mapambio kwa watawala.
 
Hivi kuna watu wenye akili timamu wanaendelea na biashara ya magazeti zama hizi! Shigongo naona alishageukia Siasa.

Kweli kila zama na kitabu chake.
 
KUTOCHAPISHWA GAZETI LA JAMHURI​

Jana Jumanne Desemba 30, 2025 kampuni yetu ya Jamhuri Media Limited ilishindwa kuchapisha na kusambaza gazeti letu la uchunguzi la JAMHURI. Tukio hili la kusikitisha limetokana na kampuni yetu kuwa na deni kubwa la uchapaji na kimsingi tumejikuta hatuna fedha za kuchapisha na kusambaza gazeti hili.

Tumeona tuliweke wazi suala hili na tutumie fursa hii kuwaomba wadau tuliotangaza nao ikiwamo serikali na taasisi zake kutulipa madeni yetu ambayo ni zaidi ya Sh milioni 300, tupate nguvu ya kiuchumi itakayoturejesha kutoa huduma ya habari kwa wananchi kama ilivyo kusudio letu la msingi la kuanzisha Gazeti la JAMHURI.

Tunaendelea kufanya kila mbinu kuhakikisha tunapata nguvu za kiuchumi haraka, tulipe deni kwa mchapishaji, kisha turejee kuendelea na kazi yetu ya msingi ya kuhabarisha jamii.

Tunawaomba radhi wasomaji wetu mnaotupigia kuuliza kulikoni hamlioni gazeti. Suala hili la kusikitisha limekuwa nje ya uwezo wetu, kwani kwa muda sasa tumekuwa tukijiendesha kwa ugumu uliopitiliza. Tunawathamini wasomaji wetu, tunapambana kurejee sokoni.

Pia Soma: Gazeti la Jamhuri halionekani leo mitaani baada ya kuandika habari za Warioba, kulikoni?

Hahahaha hiki kipeperushi kilitamba sana enzi za Magufuli!! Vipi Samia hawashiki mkono??
 
Balile hasaidii hapo ,kupewa pesa??
 
Matokeo ya uchawa hilo gazeti linaenda kufa Manyerere aanzishe gazeti lake aachane na mkuu wa machawa kwenye vyombo vya habari
 
Poleni sana...
Serikali ikikudai wewe hutokaa acha ona rangi zote, ila ukiidai yenyewe, inapuuzia kabisa...

Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom