Madeni unayodaiwa ni kikwazo, kifungo au utumwa wa kiroho na unyakuo

Madeni unayodaiwa ni kikwazo, kifungo au utumwa wa kiroho na unyakuo

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
4,014
Reaction score
4,600
"akopaye ni mtumwa wa akopeshaye"
Mithali 22:7
Maana na Ufafanuz
"Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye*"

• Hali ya Deni: Linamaanisha kuwa mtu anayekopa anajifunga kwa masharti, shinikizo, au maamuzi ya yule aliyemkopesha, kwani anapaswa kulipa deni hilo

Roho ya MADENI haitokani na Mungu,na Mungu hapendi tudaiwe ndiyo MAANA hata DENI la dhambi alitulipia kwa gharama ya damu/mauti NJIA ya msalaba.

"utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe"
Kumbukumbu la Torati 28:12

Wakolosai 2:14 – Huu ndio msingi mkuu wa neno "deni". Anasema: "Akiisha kuifuta ile hati ya mashtaka yaliyokuwa juu yetu, yaliyokuwa yakitupinga kwa amri zake; akaiondoa isiwepo tena, akiigongomea msalabani." Hati hii ya mashtaka ndilo deni la dhambi ambalo tulishindwa kulipa, naye alilifuta kwa kifo chake.

1 Petro 2:24 – "Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti.

Mungu ANACHUKIA MADENI ama sio Mpango WA Mungu sisi watoto wake tuishi tukidaiwa MADENI ama tukope kope kwa watu,ila mpango WA Mungu sisi ndiyo tukopeshe na Wala tusikope MADENI.

Madeni ni mpango/Roho ya mpinga Kristo ama Shetani ili kutufanya watumwa wake.

Madeni yanaweza kukuzuia kunyakuliwa siku ya UNYAKUO, MADENI maarufu na sugu kwa watu wengi ni kama
1)MAHARI kudaiwa MAHARI yote au kudaiwa NUSU MAHARI
2)MADENI ya vikoba,mikopo ya simu,mikopo ya mabenki,mikopo ya watu wengine ,mikopo ya scholarship ya masomo ya chuo,MADENI ya serikali n.k,

NINI CHA KUFANYA.
Lipa madeni UNAYODAIWA
kama unaweza KUSAMEHEWA WATU WANAOKUDAI..hii pengine inaweza kukusaidia na WEWE kusamehewa?kama maandiko yanavyosema..

Mathayo 6:14-15,
Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu",

Mathayo 6:14-15 yanasemaKwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.

SWALI MAARUFU UNYAKUO UTATOKEA LINI??
A:kabla ya DHIKI KUU
B: wakati WA DHIKI KUU
C:Baada ya DHIKI Kuu

Ni wazi sasa zile dalili zote 5 zilizotajwa zitatokea kabla ya UNYAKUO zilizotajwa kwenye biblia zimeshatimia,ambazo ni
1.ISRAELI kuwa TAIFA moja, TAIFA la ISRAELI miaka 2000 iliyopita lilikuwa limwpigwa nankutawanyika duniani,kwa wengi haikuwa rahisi Waliamini halitaweza kusimama Tena,mpaka may 1948 Israel ikapata uhuru wake,the impossible became possible.

2.MATETEMEKO YA ARDHI yanatokea maeneo mengi mbalimbali duniani
Mathayo 24:7 Kwa maana taifa litasimama kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali."
Hivi karibuni tumeona matetemeko katika NCHI ambazo hazikuwahi kuwa na matetemeko makubwa kwa KIASI hiki KWA miaka mingi VENEZUELA matetemeko makubwa mawili ya ukubwa WA 7.5 na 7.2 ambayo yalitokea ndani ya dakika moja na yakaua maelfu 1000s ya watu.

3.WATU WAMEKUWA WABINAFSI kuanzia viongozi WA serikali,
2 Timotheo 3:1-2
“Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa katika siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi...”

4.INJILI YA UFALME WA MUNGU/MBINGU INAHIBIRIWA DUNIA KOTE(MAANA halisi ya INJILI ya kweli ni habari njema za YESU mwenyewe anayehuburiwa ni YESU kufa kwake masalabani kwa AJILI ya dhambi zetu, tusamehewe ili TURITHI ama TUPATE UZIMA WA MILELE,hii ndio maana halisi ya INJILI na ndio injili inayotakiwa kipindi HIKI CHA siku za mwisho,SIO INJILI YA MAFANIKIO YA HAPA DUNIANI..UTAJIRI, PESA,MAGARI,NDOA hizo prosperity gospel ni INJILI FAKE?!!

sasa injili inahubiriwa DUNIA NZIMA kwa kasi ya ajabu,Tena na malaika wenyewe KWA hii kasi UAMSHO WA INJILI ULIOPO DUNIANI,upo uwezekano kuna malaika wamwshushwa KUHUBIRI watu wengi DUNIANI KOTE wanamkabidhi maisha yao wanampokea Yesu wanaokolewa KUTOKA UTUMWA WA DHAMBI.
Mathayo 11:11 (na pia katika Luka 7:28),
Amin, nawaambia, Katika hao waliozaliwa na wanawake hapajatokea mtu mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.”

kuna manabii waliozaliwa na wanawake MAANA wanadamu,na Kuna ambao hawajazaliwa na wanawake ambao ni kama malaika,kama wengine wanavyoamini huenda Nabii ELIYA alishushwa kama malaika kutoka mbinguni kwa sababu Eliya anapotokea ghafla katika 1 Wafalme 17:1 bila utangulizi wowote wa kifamilia(wazazi wake hawakutajwa) na wakati alipokuja ELIYA Eliya alitokea kipindi ambacho Taifa la Israeli lilikuwa limezama kabisa kwenye ibada ya miungu ya uongo (Baali na Ashera) chini ya Mfalme Ahabu na Yezebeli. Ujio wake wa ghafla—bila historia ya utoto wala shule ya manabii—ulikuwa kama radi inayopiga ghafla (thunderclap) kuamsha taifa lililolala kiroho.

basi NDIVYO ilivyo sasa hivi kuna INJILI KUBWA YA UVUVIO WA UAMSHO injili ya matengenezo DUNIANI KOTE ,maelfu ya watu wanaokoka wanatubu Matengenezo wanaacha dhambi wanamgeukia Yesu(SIO INJILI YA MAFANIKIO YA KIMWILI/KIDUNIA)
hata maeneo ambayo yalikuwa yamejitenga na ambayo hayakuwa na tafasiri ya biblia kwa lugha zao,INJILI KWA KASI KUBWA kila pembe ya DUNIA hii,kuliko kipindi chochote kabla,haijawahi kutokea kabla.

5.Kuongezeka KWA UTUNGU UCHUNGU mateso DUNIANI,
Mathayo 24:8, Yesu Kristo anatumia mfano mzito sana wa kibayolojia kuelezea asili ya ishara za mwisho wa dunia baada ya kutaja vita, njaa, na matetemeko ya nchi katika mstari uliotangulia.
Mstari huo unasema kwa ufupi na kwa nguvu:
“Hayo yote ndiyo mwanzo wa uchungu.”

UCHUNGU uliozungumziwa hapa ni kama ule WA mwanamke mjamzito wakati WA kujifungua.
UCHUNGU huo una SIFA zifuatazo
Kwanza unaanza taratibu unakuwa unachukua muda MREFU kutoka tukio moja kwenda lingine,halafu kadiri muda unavyoenda UCHUNGU unaongezeka ukali na unakuwa karibu karibu(unaongezeka unakazana)hapa na hapa,halafu anazaliwa mtoto(UNYAKUO)

Ulianza taratibu
2004 Tsunami
2008 KUANGUKA KWA UCHUMI WA DUNIA
2019 mlipuko WA KORONA
matetemeko,global warming,ELININO,magonjwa ya mlipuko, ya mbali mbali ya ku bipu bipu,vita vya Ukraine, mapigano mashariki ya kati n.k
Miaka kama 30-40 iliyopita

Mpaka tulipofikia kuporomoka kabisa KWA utu kila muda UCHUNGU unaongezeka ikiwemo vita,kuteswa KWA wakristo DUNIANI n.k
Luka 21:28
28 Mambo haya yakianza kutokea, simameni imara, mjipe moyo, kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.”

Ni dhahiri UNYAKUO UMEKARIBIA SANA,ni KWELI alisema hatujui saa Wala siku,ila sio miaka ,uwezekano mkubwa UNYAKUO utatokea muda WOWOTE KUANZIA sekunde hii hata Leo,kuna watumishi WA Mungu waliofunuliwa tarehe na saa ya mbinguni kalenda ya mbinguni inaonyesha muda umetumia ,KWA sababu ukifuatisha Ile kalenda ya MATUKIO inaonyesha kabisa muda umetumia ni mika hii tuliyopo UNYAKUO utatokea kwenye kizazi chetu hiki hata mwaka huu,ama mwakani..hatujui..ila UMEKARIBIA SANA.

NDOTO watu wengi sana mpaka watoto wadogo hata WANANGU MIMI wametokewa na YESU mara nyingi sana ANAWAAMBIA jiandaeni tubuni dhambi zenu nakuja kuwachukua ,na watu wengine WENGI sana duniani wametokewa na YESU ndotoni ANAWAAMBIA UNYAKUO UMEKARIBIA.

UNYAKUO UTATOKEA KWA AWAMU ZOTE TATU
1.AWAMU YA KWANZA
A😛RE TRIBULATION(UNYAKUO kabla ya DHIKI kuu) RAPTURE
Luka 17:26-37 BHN
Kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Mtu. Watu waliendelea kula na kunywa, kuoa na kuolewa mpaka wakati ule Noa alipoingia katika safina. Gharika ikatokea na kuwaangamiza wote. Itakuwa kama ilivyotokea wakati wa Loti. Watu waliendelea kula na kunywa, kununua na kuuza, kupanda mbegu na kujenga. Lakini siku ile Loti alipoondoka Sodoma, moto na madini ya kiberiti vikanyesha kama mvua kutoka mbinguni na kuwaangamiza wote. Ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Mtu atakapofunuliwa

Luka 17:34-36


34 Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa wamelala kitanda kimoja; mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa. 35 Wana wake wawili watakuwa wanatwanga pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.” [ 36 Wanaume wawili watakuwa wanafanya kazi pamoja shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.]

2.AWAMU YA 2 KATIKATI YA TRIBULATION/DHIKI KUU.
Ufunuo 7:14 S
Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo.

Baada ya dhiki KUU (SIKU YA HUKUMU)
1 Wathesalonike 4:16-17
16 "Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuka kwanza."
17 "Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele."

UNYAKUO UTATOKEA KATIKA HATUA ZOTE TATU,KWA hiyo hata ukiachwa na UNYAKUO WA kwanza ule WA kabla ya DHIKI kuu,ambao utatokea muda WOWOTE hata sasa,usiogope endelea kushika Imani Yako,JUA kabisa umwachwa lakini usipanic usiogope Cha msingi USIKUBALI KUPOKEA CHAPA YA MNYAMA 666 bado kuna NAFSI ya kunyakuliwa awamu ya pili kama utavumilia mateso ya DHIKI kuu kama wakristo kule CHINA wanavyoteswa bila KUKUBALI kupokea hiyo chapa ya digital ID
Mt 24:13
Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.

Ufu 13:17
tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.

Vumilia kukaa njaa,mana hutaishi KWA mkate..kuliko kupokea CHAPA ili uweze KUPATA chakula
Mt 4:4
Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.

Na MASHAHIDI WAWILI watashushwa KUHUBIRI injili wakati WA DHIKI kuu,KWA hiyo hata kama ukiachwa awamu ya kwanza ya UNYAKUO USIOGOPE

Maelezo ya Ufunuo Sura ya 11

• Kazi yao: Watatabiri na kutoa ushuhuda kwa siku 1,260 (miaka mitatu na nusu) wakiwa wamevikwa mavazi ya magunia.
• Ishara zao: Wana mamlaka ya kufunga anga ili mvua isinyeshe, kugeuza maji kuwa damu, na kushusha mapigo na moto kinywani kuwateketeza adui zao.
• Mwisho wao: Mnyama atatoka kuzimu, atawashinda na kuwaua, na miili yao itakaa wazi mtaani kwa siku tatu na nusu.
• Kufufuliwa: Baada ya siku tatu na nusu, Mungu atawarudishia uhai, watasimama, na kupanda mbinguni katika wingu huku adui zao wakiwatazama.

WANANGU walimuona Yesu anawanyakua katika NDOTO,nikawauliza wakati mnanyakuliwa mlikiwa na nani mwingine Yani Nina watoto WAWILI wote wameota NDOTO moja siku moja ,wakajibu WEWE haukuwepo KWA sababu tulimuuliza Yesu mbona baba hayupo Yesu akawajibu huyo ana MADENI MENGI sana makubwa..so nimegundua kuwa MADENI UNAYODAIWA Na watu yanaweza kuwa KIKWAZO Cha WEWE kunyakuliwa.
 
Back
Top Bottom