Madeni Yanakutia Stress? Fanya Hivi...

Madeni Yanakutia Stress? Fanya Hivi...

Baada ya maradhi sugu, hakuna kitu kinachokosesha amani kama kuwa na madeni.

Hili jambo linatia stress ya hali ya juu mno.

Na mbaya zaidi ni kuwa stress hii inakufanya ushindwe ku focus kufanya vitu vyenye tija katika maisha yako kama kuendesha biashara yenye kukuingizia faida.

Muda wote huna raha.

Akili imejaa mawazo.

Simu zikipigwa, moyo unapiga pa!

"Nani tena huyo?"

Unaogopa kupokea simu za watu wanaokudai.

Unaanza kujenga tabia ya kusema uongo na kuwakwepa watu kadri uwezavyo.

Kiufupi unaishi maisha ya stress na ya ku pretend.

Kwa nje inawezekana watu wanakuona na nyumba nzuri, gari nzuri n.k.

Kumbe mali zote ni za kukopa. Majasho ya watu wengine.

Mbaya zaidi ni kuwa kila unavyojaribu kuondokana na hilo janga unajikuta unazama zaidi ndani ya shimo la madeni.

Umekuwa MTUMWA wa watu wengine!

Unajihisi dhalili mno kupita kiasa.

Sasa unafanyaje kuondokana na hili janga na kujenga utulivu wa moyo?

Unafuata hatua zifuatazo:
  1. Fahamu Chanzo cha Tatizo:
    Nusu ya utatuzi wa tatizo ni kuelewa chanzo cha tatizo. Watu wengi wanaolimbikiza madeni wanafanya hivyo kwa kutaka kuishi maisha yaliyokuwa juu ya uwezo wao.

    Unataka na wewe uonekane una nyumba na usafiri mzuri ili upate kuheshimiwa na washikaji zako.

    Huna kiwanja, na wala huna pesa za kununua kiwanja lakini unatamani kumiliki kiwanja.

    Unafanyaje?

    Unatafuta njia ya mkato.

    Unaenda benki kukopa pesa za kununua kiwanja pamoja na kujenga nyumba yako.

    Kama huna pesa leo za kununua kiwanja kitu gani kinakufanya uamini kuwa kesho utakuwa nazo?

  2. Elewa Mzunguko Wako wa Pesa:
    Kaa chini na upige mahesabu kwa kina kufahamu kiundani matumizi yako ya kila mwezi.

    Una mambo gani ambayo sio ya msingi yenye kupunguza kipato chako kila mwezi?

    Ukishaelewa, fuata hatua ya 3.

  3. Kata Gharama, Usiishi Maisha ya Uongo:
    Ukitaka kuendelea kuzama ndani ya shimo la madeni endelea kujidanganya.

    Kama kipato chako ni cha shs. 400,000 kwa mwezi huwezi kuishi maisha ya mtu mwenye kipato cha shs. 700,000 kwa mwezi.

    Utakuwa mwongo!

    Unatakiwa kuishi maisha ya mtu mwenye kipato cha shs. 300,000 kwa mwezi ili uwe na akiba ya shs. 100,000 kila mwezi.

    Kama hupendi hayo maisha fanya mkakati wa kuongeza kipato chako.

    Sio kukopa pesa na kuishi maisha ya uongo.

    Hakuna ulazima wa kumiliki gari kama huweza kumudua gharama zake.

    Uza gari na upande dala dala.

    Hakuna ulazima wa kuishi katika nyumba ya kodi ya shs. 400,000 kwa mwezi kama uwezo wako ni nyumba ya shs. 200,000 kwa mwezi.

    Fanya hivi kwa matumizi yako yote yasiyo ya muhimu hadi uwe unaokoa pesa kila mwezi.

  4. Panga Mkakati wa Kuongeza Kipato Chako:
    Baada ya kufanya hayo, kinachofuata ni kupanga mkakati wa kuongeza kipato ili uweze kulipa madeni haraka.

    Je unaweza kutafuta kazi ya ziada kuingiza kipato cha ziada?

    Je unaweza kutumia taaluma yako kutoa huduma fulani?
    (k.m. kama wewe ni mwalimu, je unaweza kufundisha tuition?)

    Je unaweza kutumia taaluma yako kuanzisha biashara kwa mtaji mdogo?

    Kaa chini na kalamu na karatasi na andika idea tofauti ya kuongeza kipato chako?

    Kama unahitaji msaada wa kupata wazo zuri la biashara kwa mtaji mdogo unaweza kuenda hapa: Wazo Fasta.

    ONYO! Usiendekeze fursa zenye kuahidi pesa za haraka bila ya kufanya kazi!

    Utaendelea kuzama katika shimo la madeni

  5. Panga mkakati wa kulipa madeni:
    Kama unaokoa kiasi fulani kila mwezi kutokana na kazi yako na unaingiza kipato cha zaida, utakuwa na dira nzuri ya kutokomeza madeni yako.

    Kama una maradhi ya kutosimamia pesa zako vizuri mweke mtu unayemuamini (kama mke wako au mume wako) kusimamia ulipaji wa madeni yako.

    Kila mwezi mkabidhi fungu la pesa kwa ajili ya kupunguza madeni.

    Andika listi ya watu/benki/taasisi zote zinazokudai pamoja na gharama zake.

    Wapigie simu watu wote wanaokudai na kuwaambia mkakati wako wa kumaliza deni lako.

    Waambie utakuwa unawalipa kiasi gani kila mwezi na tarehe ngapi hata kama ni kidogo namna gani.

    Hata kama hawatofurahi, waambie kuwa huo ndio uwezo wako.

    Wanaweza wasifurahishwe lakini kama kila mwezi wanaona pesa zinaingia watakuheshimu na wataacha kukusumbua.

    Hakikisha unawalipa kwa tarehe uliyowaambia na kama itatokea dharura wajulishe mapema. Kamwe usikubali yeye awe mtu wa mwanzo kukutafuta.

    Njia nzuri ya kutokomeza stress ya kulipa madeni ni kuanza kumlipa mwenye deni la chini yao ikisha ya juu yake na kuendelea.

    Ukifanya hivyo utapunguza watu wanaokudai kwa kasi kubwa na utakuwa una enjoy kulipa madeni kwani utajisikia furaha na amani ndani ya moyo wako.

    Kama unadaiwa na ma benki na taasisi, inamaanisha wanakata deni lao kwenye mshahara wako kila mwezi.

    Hakikisha una kipato cha ziada kumudu maisha yako ya kila siku hadi madeni yaishe.

  6. Jenga Nidhamu ya Kuhifadhi Pesa:
    Umaskini unatokana na nidhamu mbovu ya kutumia pesa ambazo huna.

    Utajiri unatokana na nidhamu nzuri ya kuweka akiba kwenye kipato kidogo unachopata na kutumia akiba hiyo katika biashara au uwekezaji kuzalisha pesa zaidi.

    Matajiri wengi waliishi maisha ya duni kabla ya kujulikana na jamii kuwa wao ni matajiri.

    Wamefanya hivyo kuhakikisha kila mwezi kuna akiba ya pesa ya ziada kwa ajili ya kuwekeza katika biashara yenye kumzalishia pesa.

    Acha kuishi maisha ya kujionyesha na focus katika kuzalisha uchumi wako.

Namwomba Mwenyezi Mungu akuondolee mtihani huu na akupe utulivu wa moyo.

Una swali? Uliza chini

Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako,

Dr. Said Said - Mkurugenzi online Profits
Mungu akubariki Doctor, huwezi jua kupitia hili somo umeokoa watu wangapi. Ahsante sana.
 
Thank you na Ubarikiwe. Hamna stress ya maana kama hiibya madeni. Mungu atuvushe na atupe kibali cha kuyamaliza tuwe huru
 
Amin. Kweli deni inawamaliza watu.
 
Asante sana kwa makala hii
Niliwahi fatilia pia kwa Joel the same mada
Kupunguza kwa madeni ni commitment ambayo inasaidia kuongeza servings crearivity na investment
Nitaendelea ku practice ushauri huu
 
Your welcome. Mr. Joel yupo vizuri sana.
 
Iwapo ukiwa sio mmoja wa kausha damu ushauri wako mzuri.
 
Madeni hayaepukiki ila sio yakuyaendekeza Mimi Nina madeni Hadi nakosa amani na mengine hayalipikii ila katika Uzi wako nimekuelewa Sana ila kiukweli ukiona mtu aliefanikiwa ndio anamadeni mengi mfano mo dewji yee ndio tajiri no moja ila ndio anaongoza kwa madeni hapa Tanzania mfano hata ukiangalia katika mataifa nchi inayoongoza kwa uchumi mkubwa mfano marekani ndio nchi inaongozs deni kubwa benk ya Dunia sema Cha msingi kitu unachokopa unakifanyia Nini kama kwaajiri ya anasa kitakudidikiza ila kwa ajiri ya biashara itakuinua japo hata biashara tunafanya kwa mikopo ila biashara zinskufa mastress kibao
 
Mi nilidhani World Bank na IMF zinakopesha nchi masikini pekee, kumbe hata US naye anakopa humo? Hili jipya nitajifunza.
 
Bonge la mada Dr. Big up 🫡

Nimesoma almost coment zote but naona wengi wanaoshambulia nikuwa hawajui utofauti mkubwa wa Madeni na Mikopo.

Kwa ufupi,

Mkopo ni pesa mtu anaazima mahali fulani labda benki, kwa mtu binafsi, kikundi au taasisi nk kwa matarajio ya kukidhi mahitaji yake na baada ya muda flani wa makubaliano kurudisha kiasi hicho labda kikamilifu au na riba kadhaa.

Deni ni Mkopo uliopita muda wa malipo mfano umeambiwa urudishe mkopo wako tarehe 27.11.2024 ikifika 28.11.2024 hujarudisha hilo ni deni.

Madeni ndio yanayozungumziwa hapo kwenye topic tajwa na sio mikopo, matajiri wengi mnaowataja kama Bakhresa na Mo na nchi kama marekani wanamikopo sio madeni. Mean wapo katika muda sahihi.

Mikopo haina shida kamwe lakini ikifika hatua ya madeni hilo ni tatizo tayari. Na hapa tunafundishwa namna ya kuepukana na madeni.

Shuhuda.

I was among ya watu waliosumbuliwa na madeni miaka ya 2019 to 2022 kupitia kitabu cha Joel nilijifunza hatua kadhaa nikazifanyia kazi zimefanana na za Dr Saidi kwa sehemu zimeniwezesha kuepukana na madeni, nowadays nachukua mikopo kiasi kwa ajili ya kukuza Biashara na kurejesha na najihusisha na mikopo yenye riba nafuu zaidi.

Asanteni
 
Baada ya maradhi sugu, hakuna kitu kinachokosesha amani kama kuwa na madeni.

Hili jambo linatia stress ya hali ya juu mno.

Na mbaya zaidi ni kuwa stress hii inakufanya ushindwe ku focus kufanya vitu vyenye tija katika maisha yako kama kuendesha biashara yenye kukuingizia faida.

Muda wote huna raha.

Akili imejaa mawazo.

Simu zikipigwa, moyo unapiga pa!

"Nani tena huyo?"

Unaogopa kupokea simu za watu wanaokudai.

Unaanza kujenga tabia ya kusema uongo na kuwakwepa watu kadri uwezavyo.

Kiufupi unaishi maisha ya stress na ya ku pretend.

Kwa nje inawezekana watu wanakuona na nyumba nzuri, gari nzuri n.k.

Kumbe mali zote ni za kukopa. Majasho ya watu wengine.

Mbaya zaidi ni kuwa kila unavyojaribu kuondokana na hilo janga unajikuta unazama zaidi ndani ya shimo la madeni.

Umekuwa MTUMWA wa watu wengine!

Unajihisi dhalili mno kupita kiasa.

Sasa unafanyaje kuondokana na hili janga na kujenga utulivu wa moyo?

Unafuata hatua zifuatazo:
  1. Fahamu Chanzo cha Tatizo:
    Nusu ya utatuzi wa tatizo ni kuelewa chanzo cha tatizo. Watu wengi wanaolimbikiza madeni wanafanya hivyo kwa kutaka kuishi maisha yaliyokuwa juu ya uwezo wao.

    Unataka na wewe uonekane una nyumba na usafiri mzuri ili upate kuheshimiwa na washikaji zako.

    Huna kiwanja, na wala huna pesa za kununua kiwanja lakini unatamani kumiliki kiwanja.

    Unafanyaje?

    Unatafuta njia ya mkato.

    Unaenda benki kukopa pesa za kununua kiwanja pamoja na kujenga nyumba yako.

    Kama huna pesa leo za kununua kiwanja kitu gani kinakufanya uamini kuwa kesho utakuwa nazo?

  2. Elewa Mzunguko Wako wa Pesa:
    Kaa chini na upige mahesabu kwa kina kufahamu kiundani matumizi yako ya kila mwezi.

    Una mambo gani ambayo sio ya msingi yenye kupunguza kipato chako kila mwezi?

    Ukishaelewa, fuata hatua ya 3.

  3. Kata Gharama, Usiishi Maisha ya Uongo:
    Ukitaka kuendelea kuzama ndani ya shimo la madeni endelea kujidanganya.

    Kama kipato chako ni cha shs. 400,000 kwa mwezi huwezi kuishi maisha ya mtu mwenye kipato cha shs. 700,000 kwa mwezi.

    Utakuwa mwongo!

    Unatakiwa kuishi maisha ya mtu mwenye kipato cha shs. 300,000 kwa mwezi ili uwe na akiba ya shs. 100,000 kila mwezi.

    Kama hupendi hayo maisha fanya mkakati wa kuongeza kipato chako.

    Sio kukopa pesa na kuishi maisha ya uongo.

    Hakuna ulazima wa kumiliki gari kama huweza kumudua gharama zake.

    Uza gari na upande dala dala.

    Hakuna ulazima wa kuishi katika nyumba ya kodi ya shs. 400,000 kwa mwezi kama uwezo wako ni nyumba ya shs. 200,000 kwa mwezi.

    Fanya hivi kwa matumizi yako yote yasiyo ya muhimu hadi uwe unaokoa pesa kila mwezi.

  4. Panga Mkakati wa Kuongeza Kipato Chako:
    Baada ya kufanya hayo, kinachofuata ni kupanga mkakati wa kuongeza kipato ili uweze kulipa madeni haraka.

    Je unaweza kutafuta kazi ya ziada kuingiza kipato cha ziada?

    Je unaweza kutumia taaluma yako kutoa huduma fulani?
    (k.m. kama wewe ni mwalimu, je unaweza kufundisha tuition?)

    Je unaweza kutumia taaluma yako kuanzisha biashara kwa mtaji mdogo?

    Kaa chini na kalamu na karatasi na andika idea tofauti ya kuongeza kipato chako?

    Kama unahitaji msaada wa kupata wazo zuri la biashara kwa mtaji mdogo unaweza kuenda hapa: Wazo Fasta.

    ONYO! Usiendekeze fursa zenye kuahidi pesa za haraka bila ya kufanya kazi!

    Utaendelea kuzama katika shimo la madeni

  5. Panga mkakati wa kulipa madeni:
    Kama unaokoa kiasi fulani kila mwezi kutokana na kazi yako na unaingiza kipato cha zaida, utakuwa na dira nzuri ya kutokomeza madeni yako.

    Kama una maradhi ya kutosimamia pesa zako vizuri mweke mtu unayemuamini (kama mke wako au mume wako) kusimamia ulipaji wa madeni yako.

    Kila mwezi mkabidhi fungu la pesa kwa ajili ya kupunguza madeni.

    Andika listi ya watu/benki/taasisi zote zinazokudai pamoja na gharama zake.

    Wapigie simu watu wote wanaokudai na kuwaambia mkakati wako wa kumaliza deni lako.

    Waambie utakuwa unawalipa kiasi gani kila mwezi na tarehe ngapi hata kama ni kidogo namna gani.

    Hata kama hawatofurahi, waambie kuwa huo ndio uwezo wako.

    Wanaweza wasifurahishwe lakini kama kila mwezi wanaona pesa zinaingia watakuheshimu na wataacha kukusumbua.

    Hakikisha unawalipa kwa tarehe uliyowaambia na kama itatokea dharura wajulishe mapema. Kamwe usikubali yeye awe mtu wa mwanzo kukutafuta.

    Njia nzuri ya kutokomeza stress ya kulipa madeni ni kuanza kumlipa mwenye deni la chini yao ikisha ya juu yake na kuendelea.

    Ukifanya hivyo utapunguza watu wanaokudai kwa kasi kubwa na utakuwa una enjoy kulipa madeni kwani utajisikia furaha na amani ndani ya moyo wako.

    Kama unadaiwa na ma benki na taasisi, inamaanisha wanakata deni lao kwenye mshahara wako kila mwezi.

    Hakikisha una kipato cha ziada kumudu maisha yako ya kila siku hadi madeni yaishe.

  6. Jenga Nidhamu ya Kuhifadhi Pesa:
    Umaskini unatokana na nidhamu mbovu ya kutumia pesa ambazo huna.

    Utajiri unatokana na nidhamu nzuri ya kuweka akiba kwenye kipato kidogo unachopata na kutumia akiba hiyo katika biashara au uwekezaji kuzalisha pesa zaidi.

    Matajiri wengi waliishi maisha ya duni kabla ya kujulikana na jamii kuwa wao ni matajiri.

    Wamefanya hivyo kuhakikisha kila mwezi kuna akiba ya pesa ya ziada kwa ajili ya kuwekeza katika biashara yenye kumzalishia pesa.

    Acha kuishi maisha ya kujionyesha na focus katika kuzalisha uchumi wako.

Namwomba Mwenyezi Mungu akuondolee mtihani huu na akupe utulivu wa moyo.

Una swali? Uliza chini

Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako,

Dr. Said Said - Mkurugenzi online Profits
Nina miaka saba kazini lakini sioni pesa kila ninapo pata mshahara... naishia kweny madeni tu. Adii nimejiingiza kwenye mikopo ya kausha damu na kubeti ... naomba msaada
 
Ndo mana kuna neno KUKOPA na DENI sasa wanataka tusidaiwe ili? Tuishauri inchi bas na yenyewe iache kukopa
 
Aah maoni mazuri sana,nimechelewa Nina miaka 56sasa,! Acha nitumbue tuu.
 
Back
Top Bottom