Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Katika kudhibiti ajali za barabara Jeshi la polisi mkoa wa Tanga limewafungia leseni za udereva madereva 15 Kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa jumla ya makosa 404 yameweza kuripotiwa na faini za papo hapo zaidi ya shilingi Milioni 119.6 zimeweza kukusanywa.
Alisema kuwa Operesheni hiyo ambayo imefanywa kuanzia kuanzia Desemba 15 hadi 30 mwaka huu katika maeneo mbalimbali na kuweza kuyatoa barabara magari 10 huku namba za usajili zikiondolewa na wamiliki kutakiwa kuyafanyia ukarabati kabla ya kuruhusiwa kurudi tena barabarani.
Soma Pia: Madereva wa mabasi za abiria na malori wapatao 200 wamefutiwa leseni zao kuanzia Agosti hadi Novemba
"Aidha Jeshi la polisi linasisitiza kuwa hatua Kali za sheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya yeyote atakayekiuka sheria au kuonyesha viashiria vya uvunjifu wa amani"alisema RPC Mchunguzi.
Vile vile aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya usalama Ili kupunguza ajali za barabara na kuboresha hali ya usalama Kwa watumiaji wa barabara.