Madereva 9 Wakenya waliotokea Tanzania wagunduliwa kuwa na Corona. Visa vyafikia 700

Madereva 9 Wakenya waliotokea Tanzania wagunduliwa kuwa na Corona. Visa vyafikia 700

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Jana tumeona ya Zambia, leo ya Wakenya tisa wameingia kutoka Tanzania wote wameathirika, duh! Bongo imekua vipi, hizo sera za kila kitu ruksa hata kusongamana kwenye vilabu kutawaponza sana.

=======

Nine Kenyan truck drivers who arrived in the country from Tanzania are among 28 people who tested positive for coronavirus in the last 24 hours.

This now brings the total number of COVID-19 cases in Kenya to 700.

Health CAS Rashid Aman said the drivers from Kajiado were tested at the Namanga border alongside their Tanzanian counterparts.

“Tanzanian drivers entering Kenya through that border are tested on their side of the border. 5 of the Tanzanian nationals were found to be positive and we have alerted the Tanzanian authorities to take up the matter,” he said.

Those whose samples tested positive in Nairobi within the last 24 hours are from the Kenyatta National Hospital (3), Embakasi (2), Kibra (1) and Pumwani (1).

Patients who tested positive in Mombasa are from Mvita (3), Changamwe (2), Kisauni (2), Nyali (2) and Likoni (1).
Two other patients are from Eldas and Tarbach in Wajir County.

12 people have since been discharged bringing the total number of recoveries from coronavirus to 251.

One patient who was at a health facility in Nairobi has died. The total number of deaths from the COVID-19 disease in Kenya is 33.

Source: Citizentv.co.ke
 
Kama hamtaki korona mnaingia kufata nini huku?

Huko kwenu si kuna lokidauni Sasa mbona raia zenu zinatapatapa huku?

Mi naona kuna namna mnaitumia kuipiga tz maana nikiangalia na mkulu wetu kukaidi hivyo vikao ni kama kuna kitu kinaendelea na inatafutwa namna ya kuichapa tz kiuchumi na kitalii si bure maana hizo takwimu zenu na huku mtaani ni vitu viwili tofauti kabisa!

Nahisi kuna kitu kinaendelea baina ya serikali yetu na ukanda tuliopo kuna kitu si cha kawaida.
 
Kama hamtaki korona mnaingia kufata nini huku?

Huko kwenu si kuna lokidauni Sasa mbona raia zenu zinatapatapa huku?

Mi naona kuna namna mnaitumia kuipiga tz maana nikiangalia na mkulu wetu kukaidi hivyo vikao ni kama kuna kitu kinaendelea na inatafutwa namna ya kuichapa tz kiuchumi na kitalii si bure maana hizo takwimu zenu na huku mtaani ni vitu viwili tofauti kabisa.

Nahisi kuna kitu kinaendelea baina ya serikali yetu na ukanda tuliopo kuna kitu si cha kawaida
Ujinga ndo adui mkubwa kwa Tanzania. Hadi hili la corona unataka uingize siasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi 700 baada ya wagonjwa wapya 28 kuthibitishwa katika kipindi cha saa 24.

Katibu mtendaji katika wizara ya Afya Rashid Aman amesema kwamba kati ya wagonjwa hao wapya 10 wanatoka Momabasa , 9 kutoka kajiado na 7 kutoka Nairobi huku 2 wakitoka Wajir.

Wagonjwa wote tisa kutoka Kajiado ni madereva wa malori ya masafa marefu ambao walikuwa wanarudi kutoka Tanzania katika mpaka wa Namanga.

Jumla ya sampuli 841 zilifanyiwa vipimo katika kipindi cha saa 24 zilizopita

Afisa huyo wa afya alitangaza wagonjwa wengine 12 waliopona na hivyobasi kufanya idadi ya wale waliopona kufikia 251.

Amesema kwamba wagonjwa wengi ambao wamefariki na ugonjwa huo katika kaunti ya Mombasa ni watu wenye umri mkubwa.

Hatahivyo Aman alitangaza kifo kimoja zaidi mjini Nairobi na hivyobasi kuongeza idadi ya waliofariki kutokana na ugonjwa huo kufikia watu 23.

Aman ameongezea kwamba idadi ya kaunti zilizoathiriwa na ugonjwa huo zimeongezeka.

''Ni wazi kwamba ugonjwa huu utasambaa katika taifa zima . huku tukiingia katika mwezi wa tatu ni lazima tulindane'', alisema.

Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Jumatatu , afisa huyo alisema kwamba lengo la serikali ni kupunguza usambazaji katika jamii.

Aman amewataka Wakenya kuripoti katika hospitali zilizo karibu nao kuhakikisha kwamba wanasaidika kabla ya dalili hizo kuwa mbaya.
 
Tuwe makini sana katika hili, tuwe makini katika kulifikiria, nimeanza kuhisi kuna kitu nyuma ya hili janga. Kuna ukweli umefichwa, kuna kitu dunia imefichwa.

Ila tukiweka itikadi pembeni, akili zitatumika kuna ambacho wengi hawajakiona.
Kipi mkuu korona haina siasa wajinga na wapumbavu ndo wanafikiria za kuwaza kwamba kwenye korona kuna mkono wa mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipi mkuu korona haina siasa wajinga na wapumbavu ndo wabafikira za kuwaza kwamba kwenye korona kuna mkono wa mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo katika Corona kuna mkono wa Mungu?

Ishu kubwa ni kusema kwamba kuna kitu nyuma ya hili,hiko kitu pia tujiulize ni kitu gani,ni kitu mtu, ni kitu Mungu,ni kitu shetani, ni kitu silaha, ni kitu janga, ni kitu kutoka mbinguni, ni kitu kutoka maabara,ni kitu kutoka wapi, ni kitu kama adhabu, ni kitu kama gharika, ni kitu kama mkono wa shetani, kuna kitu nyuma ya hili gonjwa, nyuma hiyo ni ipi, ni siri, ni dhahiri, au nini? Ndio maana ya kujihoji kwanza kuna nini nyuma ya hili kuna kitu gani.

Kama ni ugonjwa umeanzia wapi, kwa wanyama au kwa binadamu, kama ni wanyama kwanini leo na siyo mwaka 1978, nyuma ya hii ni nini, kuna nini kilichofichwa, kimefichwa kwanini, na nani, lini ili iweje.

Tutafute pa kuanzia kwanza kabla ya kutafuta tuliopo.
 
Kwa sasa kikubwa chukueni tahadhari acheni kusongamana kwenye vilabu, hayo ya nyuma ya pazia yatajadiliwa baadaye ila kimsingi kwa sasa ni kutafuta namna ya kupunguza kuambukizana.
 
Kwa sasa kikubwa chukueni tahadhari acheni kusongamana kwenye vilabu, hayo ya nyuma ya pazia yatajadiliwa baadaye ila kimsingi kwa sasa ni kutafuta namna ya kupunguza kuambukizana.
Hao wanasongamana kwenye vilabau kama wapo basi akili zao hazihitaji tena kujadiliwa,bali watakua wanahitaji tiba mbadala.
 
Nine Kenyan truck drivers who arrived in the country from Tanzania are among 28 people who tested positive for coronavirus in the last 24 hours.

This now brings the total number of COVID-19 cases in Kenya to 700.
Ebwana eeeeh . . . . .hatari sana, jamani jamani tuchukue tahadhari zaidi. Hali ni mbaya ilikua Zambia na sasa Kenya duuuh . . . . Mungu tuokoe
 
Back
Top Bottom