Madereva 9 Wakenya waliotokea Tanzania wagunduliwa kuwa na Corona. Visa vyafikia 700

Madereva 9 Wakenya waliotokea Tanzania wagunduliwa kuwa na Corona. Visa vyafikia 700

Hivi madereva wa malori wana nini lakini? Kwenye VVU wamo, wanaitwa kundi hatarishi. Haya kwenye Corona tena ndio hivyo. Wanakwama wapi?
 
yuzazifu,

Sasa mzee sehemu ambazo maambukiz yamepungua wanalegeza mashart ya lockdown huku maambukizi ndio kwanza yamepamba moto, dunia itakapokuwa wazi sisi tutafungiwa kwenda nchi yeyote mpaka tupitie hizo phase walizopita wengine na wajiridhishe kuwa hakuna maambukizi, sawa lockdown sio nzuri lakin kama haifanyi lockdown unafanya nini ? whats the alternative. Upuuz ni kudhan hawa wanavyolegeza lockdown ni mambo yamewashinda wanataka kuwa kama sisi sio kweli sisi hatujakaa lockdown na maambukiz yanazid kusambaa, wakuu muwe mnafikiria kidogo, watu wanakufa sana na healthy system zina jam saivi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
kinachowatoa lock down ni anguko la uchumi mkuu au hukumsikia trump akisema uchumi umeharibika vibaya?

marekani bado anaongoza kwa rate ya maambukizi na vifo duniani bt hujiulizi kwa nini anatoa lock down

tatizo letu watu weusi kifikra hatujitegemei ndo maana tunasubiri wasemacho weup
 
Hivi madereva wa malori wana nini lakini? Kwenye VVU wamo, wanaitwa kundi hatarishi. Haya kwenye Corona tena ndio hivyo. Wanakwama wapi?

Kuna jamaa yangu fulani kitambo alikua dereva lori, alikua akiniambia yaani kuanzia bandarini hadi mpakani alikua na mwanamke kila kituo au mji, na hao wanawake walikua na waume ambao waliwasubiri kwa ratiba.
Pia jamaa alikua anapiga hela sana kwa kubeba mizigo ya watu kisiri.
 
Hapo nimeelewa vizuri. Kwa hiyo wanaambukizwa na machangudoa. Hatari sana hii.
 
Tuwe makini sana katika hili, tuwe makini katika kulifikiria, nimeanza kuhisi kuna kitu nyuma ya hili janga. Kuna ukweli umefichwa, kuna kitu dunia imefichwa.

Ila tukiweka itikadi pembeni, akili zitatumika kuna ambacho wengi hawajakiona.
na soon mtaanza kumwelewa magufuli why aliwaita ikulu viongozi wa usalama na why alipima mpka mapapai na why anaongea kama kuna kitu kipo nyuma ya ugonjwa huu.Ndo maana hata ukimuona anaongelea hili swala unaona kabisa kwenye sura hayupo sawa kama kuna kitu anataka kukiongea ila anashndwa tu,ni swala la muda tu kila kitu kitakuwa wazi but kuna jambo kubwa sana lipo nyuma la huu ugonjwa.
toka alipotoa tu hutuba yake nilimwelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo nimeelewa vizuri. Kwa hiyo wanaambukizwa na machangudoa. Hatari sana hii.

Kazi yoyote inayohusu mwanaume kulala kwenye mahoteli huku akilipiwa na kampuni lazima ataongozwa na akili za dushe, nimewahi kufanya kazi za namna hiyo, hatari sana, kampuni inakupa zaidi ya laki moja kila siku kama per diem, unapewa usake wapi utalala na kula, pia inakulipia usafiri wa kwenda kwenye baadhi ya miji.
 
Majirani mnachokitafuta mtakipata soon endeleeni kibua ayo matak$
 
Acheni njaaa za umaskini chukua tahadhari, bado mnasongamaana kwenye mabaa, sasa mumefungiwa mipaka na majirani wote, kazi yenu kueneza kirusi tu.

Hebu ona Watanzania waliokwama mpakani Zambia, hawana hata barakoa wanataka kwenda kupeleka kirusi kwenye nchi ya watu.

Mumekua aibu Afrika hii

2396251_20200511_100332.jpg
TANZANIA YATENGENEZA DAWA YA CORONAVIRUS INAITWA #NIMRCAF

DAWA iliyofanyiwa kazi na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), imetoa mwanga wa matumaini kwa wagonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya corona.

Dawa hiyo iliyopewa jina la NIMRCAF, inatokana na mchanganyiko wa vyakula; na katika majaribio imeonesha ina uwezo mkubwa wa kudhibiti virusi vya corona.

Akielezea mchanganyiko huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Tiba Asili cha NIMR, Dk Justine Omolo alisema ni fomula ya tiba lishe, ambayo ina mchanganyiko wa pilipili kichaa, tangawizi, limao na kitunguu saumu, asali na maji.

Alisema dawa hiyo inasaidia kumpa nafuu mgonjwa wa corona, kwa kutibu dalili zinazotokana na ugonjwa huo.

Kwamba tayari imeshaonyesha matokeo chanya. “Mchanganyiko wa tiba lishe hiyo sio dawa ya corona, lakini inasaidia kumpa nafuu mgonjwa wa corona kwa kuwa inatibu dalili zinazoambatana na ugonjwa huo,” Dk Omolo.

Alisema mpaka sasa tiba lishe hiyo, imeshaleta matokeo chanya kwa kuwa imesaidia wagonjwa wengi wa corona. Alisema kwa sasa mahitaji yamekuwa ni mengi, tofauti na awali.

“Mwanzo tulikuwa tukitengeneza chupa 1,000 na tumekuwa tukisambaza hospitali kwa wagonjwa kwa siku chupa 120 hadi 200, lakini sasa mahitaji yamekuwa makubwa na imeonyesha matokeo mazuri kwa wagonjwa,” alisema

Alisema kutokana na mafanikio hayo, serikali imewaongezea vifaa ambapo kuanzia wiki ijayo wataanza kuzalisha chupa 5,000 kwa siku. Alisema chupa hiyo yenye ujazo wa nusu lita, inauzwa Sh 10,000 na ni dozi ya mtu mmoja ambayo inanyweka kwa siku tano, ambapo mgonjwa atalazimika kunywa mara tatu kutwa.

Dalili za ugonjwa huo wa corona ni joto mwilini na kikohozi kikavu; na baada ya wiki moja kikohozi hicho, kinaweza kusababisha tatizo la kushindwa kupumua. Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya duniani (WHO) kwa wagonjwa 56,000, ulibaini kuwa asilimia 80 ya wale walioambukizwa, hupata dalili zisizo kali kama vile kukohoa, joto mwilini na mara nyingine homa ya mapafu, asilimia 14 hupatwa na dalili kali, kama vile tatizo la kupumua.

Asilimia sita hukumbwa na tatizo la mapafu kushindwa kufanya kazi na viungo vingine mwilini na hata kusababisha kifo. Miongoni mwa dalili nyingi zilizoripotiwa na wagonjwa, asilimia 88 walidai kuwa na joto mwilini, asilimia 68 kikohozi kikavu na asilimia 38 waliripoti uchovu. Tatizo la kupumua liliwapata asilimia 19 ya wagonjwa, asilimia 13 waliripoti kuumwa na kichwa na asilimia nne waliripoti kuharisha.

Omolo alisema kwa mtu ambaye hana dalili, anapaswa kutumia dawa hiyo mara moja kwa siku na hiyo itamsaidia kujikinga na ugonjwa huo wa corona, ambao takwimu za WHO zinaonesha hadi Mei 6, mwaka huu, ulikuwa mewakumba watu 3,588,773.

“Watu wanapaswa kujua kwamba virusi vya corona au Covid 19 ni mojawapo ya homa, hivyo basi vina dalili nyingi zinazofanana na homa ya kawaida’’, alisema

“Lazima uwe makini iwapo unahisi tatizo la kupumua. Ni muhimu kutafuta msaada wa matibabu haraka. Tiba lishe hii haina madhara, watu waitumie ili kujikinga na janga hili la corona, “ alisisitiza Watalamu wanasema zipo njia nne za kudhibiti vimelea vya magonjwa hasa virusi ambavyo havina tiba.

Njia ya kwanza ni chanjo na ya pili ni kuzuia virusi visiweze kujishikiza kwenye seli zilizopo mwilini. Njia ya tatu ni kudhibiti visizaliane au kuongezeka mwilini na njia ya nne ni kuongeza protini mwilini ili kusaidia kupambana na virusi hivyo. Kwa mujibu wa Dk Omolo, NIMRCAF ina vitamini C kwa wingi na vitamini K, na kitaalamu mchanganyiko unaopatikana katika tiba lishe hiyo unaitwa ‘Polyphenols’. Mchanganyiko huo unazuia damu kuganda.

Alisema seli zinazopokea virusi vya corona, zipo kwenye mapafu na virusi vikiingia humo, husababisha damu kuganda na kuleta matatizo kwenye mfumo wa upumuaji. “Mgonjwa akitumia tiba lishe hii, ndani ya nusu saa lazima atasikia nafuu.

Wagonjwa wengi waliokuwa hoi walipoitumia, wamepata matokeo mazuri na wengine wamepona kabisa,”alisema Alisema walianza utafiti wa dawa hiyo muda mrefu, kabla dunia haijakumbwa na janga la corona.

Walifanya utafiti huo kwa kushirikiana na watalamu mbali mbali wa tiba asili. Walikuwa katika kutafiti tiba ya Ukimwi. NIMR imekuja na dawa lishe hiyo, ikiwa ni siku chache baada ya WHO kutoa taarifa yake, ambayo ilieleza kuwa wanatambua na kuthamini mchango wa tiba asili kutoka Afrika. WHO ilieleza kwamba dawa hizo, pia zinapaswa kupewa nafasi sawa katika kufanyiwa majaribio, kama dawa kutoka maeneo mengine duniani.
 
na soon mtaanza kumwelewa magufuli why aliwaita ikulu viongozi wa usalama na why alipima mpka mapapai na why anaongea kama kuna kitu kipo nyuma ya ugonjwa huu.Ndo maana hata ukimuona anaongelea hili swala unaona kabisa kwenye sura hayupo sawa kama kuna kitu anataka kukiongea ila anashndwa tu,ni swala la muda tu kila kitu kitakuwa wazi but kuna jambo kubwa sana lipo nyuma la huu ugonjwa.
toka alipotoa tu hutuba yake nilimwelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
CIA wapo kuchunguza Corona,usalama wa Irani waliamua kuungana na taifa fulani kuchunguza ugonjwa huu lakini TISS ya Tanzania imeamua kuchunguza watu wamepokea katika hisia ambazo hawakuwaza sana.
Tujiulize kama sisi kwetu mbuzi ana coroba,papai lina corona,tumekataa.
Vipi kwa wazungu,ngamia ana corona,popo ana corona,nguo ina corona,meza ina corona na bado tukakubali.
alichosema Magufuli siyo kwamba waliweka asilimia mia moja katika matokeo yake,alitoa na angalizo kwa WHO kuliotazama hili na akatoa angalizo kwa wataalamu wa afya kuangalia hili pia.
sisi tulichukulia jambo hili kwa haraka zaidi ana kusahau kuwa Tanzania siyo nchi ya kwanza kutil;ia mashaka vipimo hivi
Kuna kitu nyuma ya ugonjwa huu,hata ukimwi ilijulikana zaidi ya miaka thelathini,hata corona itajulikana hata kama ni baada ya miaka mia moja.
Tunaamua kukaa kimya tu bila ya kutumia vitengo vya usalama kufanya uchunguzi,hili ni tatizo na udhaifu wa hali ya juu kwa watu makini.
Ni imani ya kuwa kwamba baada ya Corona,vitengo vingi vya usalama wa taifa watabadilika na kuwa na vitengo vingine vya kupambana na kuzuia magonjwa.
 
Acheni njaaa za umaskini chukua tahadhari, bado mnasongamaana kwenye mabaa, sasa mumefungiwa mipaka na majirani wote, kazi yenu kueneza kirusi tu.

Hebu ona Watanzania waliokwama mpakani Zambia, hawana hata barakoa wanataka kwenda kupeleka kirusi kwenye nchi ya watu.

Mumekua aibu Afrika hii

2396251_20200511_100332.jpg
Swali kama korona siyo upumbavuu ? Kwanini dalili pekee kwa wagonjwa wengi wanaopimwa bila ya kuumwa na kukutwa na korona ni kipimo tu hadi wananaambiwa wamepona ni kipimo ndiyo hua dalili pekee ,yaani MTU uhumwi kitu chochote toka upimwe na kuambiwa unayo korona hadi unakaa hospitalini mwezi mzima bila kuumwa na kupimwa tena na tena hadi wanakuambia umepona tayari bila hata kujisikia tatizo lolote kiafya isipokua dalili PEKEE NI KIPIMO KUKUKUTA NA KORONA !!!??? ndiyo maana nasema kupimapima ni ujinga isipokuwa kwa wanao nakuwa na tatizo kiafya ndiyo wapimwe kama ni korona inawasumbua over

Send by APOLO 1
 
Marekani wametoa tamko hali ilivyo kwenu....

2397751_1589310856950.png
 
Back
Top Bottom