Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 243
- 287
Kuna kitu kimenishangaza sana, nilikua na safari yangu ya kutoka Nilipo kwenda Kigoma, nilisafiri na basi la Adventure, wakati tukiwa tumepita Kibondo dereva akaanza kupiga soga na sisi Abiria tuliokua karibu na yeye kuhusu Makampuni ya Magari namna wanavyodhoofishana.
Basi akasema kwamba alishawahi kupewa Pesa na Moja ya Kampuni ya mabasi hapa nchini kwamba aangushe gari makusudi ili kampuni hilo likose soko, unaambiwa baada ya kupewa kiasi alichokitaka basi bwana wakati yuko safarini Usiku, akiwa kwenye mwendo anaoujua yeye Ghafla akazima taa za gari mara Paaa. Gari likaanguka upande wa kondakta watu kadhaa wakafariki na yeye akaondoka kwa kutoroka.
Basi hivi kweli madereva wamefikia hatua ya kufifisha nyota za makampuni ili wasipate wateja? hebu Madereva kuweni na Ubinaadamu na msiniangalie maskahi yenu.