Chama cha Wamiliki na Waendesha Bajaji na Bodaboda mkoani Kilimanjaro kinawataka waendesha vyombo hivyo vya usafiri kutokujihusisha kwa namna yoyote na matukio ya vurugu au uvunjifu wa amani, endapo wapo wanaojihusisha, na kimeweka wazi kuwa hakihusiki na matukio ya Oktoba 29 yaliyotokea katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo.
Akitoa kauli hiyo katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi za kikosi cha Jeshi la Usalama Barabarani mjini Moshi, Mwenyekiti wa chama hicho, Bahàti Mustapha Nyakiraria, amesema sekta ya bodaboda na bajaji inategemea amani na utulivu wa nchi ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi na kuwawezesha madereva kujipatia kipato cha kila siku.
Amesema ni jambo lisilo la haki kuwatuhumu madereva halali wa bodaboda na bajaji kwa matendo ya baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema kutumia vyombo hivyo kwa uhalifu.
Nyakiraria amesisitiza kuwa madereva wa mkoa wa Kilimanjaro wana vituo rasmi vya kufanyia kazi, hivyo ni vigumu kwao kuvitelekeza na kwenda kushiriki vitendo vya vurugu au uvunjifu wa amani.
“Wahuni wachache wanaotumia bodaboda au bajaji kutekeleza matukio ya uhalifu hawawakilishi kwa namna yoyote taswira na maadili ya madereva wetu wa Kilimanjaro,” amesema.
Ameongeza kuwa kulinda amani ni jukumu la kila Mtanzania, na chama kitaendelea kutoa elimu na maelekezo kwa wanachama wake juu ya umuhimu wa utulivu, uzalendo na kutoshiriki katika vitendo vyovyote vinavyohatarisha usalama wa nchi.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Hamadi Bakari Bendera, amesema kuwa ustawi wa kazi za bodaboda na bajaji unatokana moja kwa moja na kuwepo kwa amani.
Amesema madereva hutegemea kila siku kutoka kazini ili kupata kipato cha kuendesha maisha ya familia zao, hivyo hawawezi kuwa sehemu ya vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa jamii.
Madereva waliohudhuria mkutano huo wameeleza kuwa Tanzania imekuwa kisiwa cha amani na kimbilio kwa watu kutoka mataifa jirani yanayokumbwa na machafuko huku Wakiitaka jamii kutafakari thamani ya amani iliyopo na kuilinda kwa gharama yoyote, kwani kupotea kwake kuna athari kubwa kwa jamii nzima