JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan L. Bukumbi ameeleza kukamatwa kwa watuhumiwa wa wizi wa mbuzi.
Amesema tukio hilo lilitokea 09/02/2022 majira ya Saa Saba Usiku, (01:00hrs) maeneo ya Shule ya Msingi Mlandege Kata ya Mlandege Manispaa na Mkoa wa Iringa, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata watu wanne akiwemo JOSEPH CHUZA mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni dereva bodaboda Mkazi wa Kihesa.
Akiwa na wenzake watatu ambao ni madereva bodaboda wakazi wa Kihesa wakiwa na mifugo (mbuzi) watano (5) wote wasio na vibali vya manunuzi, chanjo na usafirishaji wakiwa wamewabeba kwenye pikipiki mbili zenye usajili wa namba MC 626 CMH Boxer iliyobeba mbuzi watatu na MC 920 CWP Boxer iliyowabeba mbuzi wawili kuelekea nyumbani kwa ONESMO PARASELELA maeneo ya Mlandege ndani ya Manispaa ya Iringa.
Mafanikio hayo yametokana na taarifa zilizopatikana kuwa mifugo hiyo imeibwa huko Mahenge mpakani mwa Morogoro na Iringa Wilaya ya Kilolo, mifugo iliyokamatwa imehifadhiwa maeneo ya Mlandege kwenye zizi la machinjio ya Manispaa ya Iringa na watuhumiwa wote wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.