Madereva bora tufe tumesimama kuliko kuishi kwa kupiga magoti

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Mtanzania ni mpole, lakini akiamua jambo lake, utamuua tu.

Jana nilikuwa naangalia vitisho vya Polisi nikabaki nacheka. Polisi wanahisi bado wanaheshimika kama zamani.

Tangu waue 29.10.2025 heshima yao imeshuka. Wwanaonekakama kama wanyama mbwa mwitu.. Tunaishi nao kwa timing. Ama zetu ama zao.

Hata mjusi ukimkimbiza sana anageuka kuwa nyoka.

Askari Polisi wamejenga nyumba nyingi kwa jasho letu. Madereva wegeuka kitega uchumi cha Polisi mdo maana kila mmoja anapigania kuwa Trafiki.

Madereva wamechoka.

Mgomo unaendelea siku ya pili hadi kieleweke. Bandueni Plate number mkitaka bandueni hadi rangi za magari. Hatuendeshi bila kujua hatima yetu.

BORA TUFE TUMESIMAMA KULIKO KUISHI TUMEPIGA MAGOTI

Mgomo unaendelea Dar es Salaam Magufuli Bus terminal leo 30 Septemba 2026

===

Mgomo wa madereva pasua kichwa, hakuna basi lililoondoka Stendi ya Magufuli​

Jumatano, Septemba 30, 2026

Muktasari:​

  • Wamiliki wa mabasi presha juu abiria waliokata tiketi wakiendelea kushinikiza kwa kupaza sauti kurejeshewa fedha zao ili waangalie namna nyingine ya kufika wanakohitaji kufika
Dar es Salaam. Hali bado ni tete ndani ya Standi ya Mabasi Magufuli, jijini Dar es Salaam huku madereva wakiendelea na mgomo na hadi saa 1:45 asubuhi hakuna basi lililoondoka kuanza kutoa huduma, wakisema bado hawajaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusu madai yao.

Madereva hao walianza mgomo jana, Jumanne, Septemba 29, 2026, wakishinikiza kutatuliwa kwa madai yao, likiwamo suala la kukatwa pointi, kufungiwa madereva na kuondolewa kwa leseni zao kwenye mfumo.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi alifika katika standi hiyo jana na kuliagiza Jeshi la Polisi kusitisha mara moja mfumo wa kukata pointi kwa madereva ili kupisha tathmini ya kina ya mfumo huo.

Katika maelezo yake, Katambi aliwataka madereva kurejea kazini na kuendelea na shughuli zao kwa amani, huku akilitaka Jeshi la Polisi kutowabughudhi madereva kwa kipindi cha siku 14 cha mpito, wakati Serikali ikiangalia hoja zilizoibuliwa na kuzitafutia majibu.

mgomo-1.jpg

Hata hivyo, hali ya sasa ni tofauti na matarajio, jambo ambalo limewaweka katika wakati mgumu abiria walioahidiwa kuanza safari asubuhi ya leo. Baadhi yao wanahangaika kurejeshewa nauli zao huku wakitafuta njia mbadala za kuendelea na safari zao.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Mustafa Mwalongo, amesema wamiliki wa mabasi nao wameanza kupata shinikizo kutoka kwa abiria wanaotaka kurejeshewa nauli zao.

“Ni kweli, hakuna basi lililoondoka hadi sasa. Madereva bado wanaendelea na mgomo. Tunajaribu kadri ya uwezo wetu kuzungumza nao ili waanze kutoa huduma, kwa sababu hata wamiliki tunapata hasara,” amesema.

Mwananchi limezungumza na mmoja wa dereva, ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema uamuzi uliotolewa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani, katika kushughulikia changamoto hawajauelewa hivyo bado wanahitaji Waziri Mkuu,Dk Mwigulu Nchemba akawasikilize.

"Jana alitoa uamuzi kwa baadhi ya mambo lakini hatujakubaliana kwa sababu hii kazi wengine tunaitegemea kwa kila kitu kulisha familia, Kodi ya pango na kusomesha watoto inakuaje tunafanyiwa namna hii," amesema

mgomo-2.jpg

Jana, kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Katambi kililazimika kusimama mara kwa mara kutokana na baadhi ya madereva kushinikiza Waziri Mkuu afike kuwasikiliza na kueleza namna atakavyoshughulikia changamoto zinazowakabili.

Hali hiyo ilimfanya Waziri Katambi kutoa ufafanuzi kuhusu kutokuwepo kwa Waziri Mkuu, akisema ameshindwa kuhudhuria kutokana na majukumu ya Kitaifa na kwamba yupo nchini Kenya kwa shughuli hizo.

mgomo-3.jpg

Hadi kikao hicho kilipomalizika saa moja na nusu usiku licha ya madereva kuagizwa kuendelea na shughuli zao, nyuso za madereva wengi hazikuonyesha furaha. Baadhi yao walibaki katika makundi mbalimbali wakijadiliana kuhusu hatua zilizotangazwa na Waziri Katambi.

Hadi sasa 7:45 asubuhi hakuna basi lolote lililotoka.

Hii taarifa nimeinakiri kwenye Gazeti la kila siku la Mwananchi
 
Watisoma namba .... majiji yote the likes of Dsm, Arusha,Dom, Mwanza, Mbeya na Tanga wanatakiwa kugoma kote .... hii mikoa ndio kitovu cha uchumi wa Tz......

Hapa sasa serikali wataona umuhimu wa madereva.....
Swali... . HIVI wamiliki wa ma_bus wako nyuma ya huu mpango, ama ni madereva tu na umoja wao wameungana ?
 
Dereva ana backup ya tajiri wake. Hiyo ni vita inayopiganwa kwa akili sana. Rudi nyuma swala la kulazimisha mabasi yaanzie stand ya magufuli halafu unganisha dots
 
Mimi opinion yangu tofauti kidogo ! Nadhani nia ya serikali ni njema sana ili kupunguza ajali barabarani ...madereva wetu wengi wanaendesha magari kwa mazoea ni wagumu kufuata sheria ! Hii sheria hata ulaya ipo na madererva kule wako makini sana
Tatizo letu mambo muhimu tunaingiza siasa ..ukiangalia hili tatizo wazee wa kubeba matukio wamelibeba na kuanza kulitumia kwenye siasa zao
 
Mtanzania ni mpole, lakini akiamua jambo lake, utamuua tu.

Jana nilikuwa naangalia vitisho vya Polisi nikabaki nacheka. Polisi wanahisi bado wanaheshimika kama zamani.

Tangu waue 29.10.2025 heshima yao imeshuka. Wwanaonekakama kama wanyama mbwa mwitu.. Tunaishi nao kwa timing. Ama zetu ama zao.

Hata mjusi ukimkimbiza sana anageuka kuwa nyoka.

Askari Polisi wamejenga nyumba nyingi kwa jasho letu. Madereva wegeuka kitega uchumi cha Polisi mdo maana kila mmoja anapigania kuwa Trafiki.

Madereva wamechoka.

Mgomo unaendelea siku ya pili hadi kieleweke. Bandueni Plate number mkitaka bandueni hadi rangi za magari. Hatuendeshi bila kujua hatima yetu.

BORA TUFE TUMESIMAMA KULIKO KUISHI TUMEPIGA MAGOTI
View attachment 3680834
Mgomo unaendelea Dar es Salaam Magufuli Bus terminal leo 30 Septemba 2026

===

Mgomo wa madereva pasua kichwa, hakuna basi lililoondoka Stendi ya Magufuli​

Jumatano, Septemba 30, 2026

Muktasari:​

  • Wamiliki wa mabasi presha juu abiria waliokata tiketi wakiendelea kushinikiza kwa kupaza sauti kurejeshewa fedha zao ili waangalie namna nyingine ya kufika wanakohitaji kufika
Dar es Salaam. Hali bado ni tete ndani ya Standi ya Mabasi Magufuli, jijini Dar es Salaam huku madereva wakiendelea na mgomo na hadi saa 1:45 asubuhi hakuna basi lililoondoka kuanza kutoa huduma, wakisema bado hawajaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusu madai yao.

Madereva hao walianza mgomo jana, Jumanne, Septemba 29, 2026, wakishinikiza kutatuliwa kwa madai yao, likiwamo suala la kukatwa pointi, kufungiwa madereva na kuondolewa kwa leseni zao kwenye mfumo.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi alifika katika standi hiyo jana na kuliagiza Jeshi la Polisi kusitisha mara moja mfumo wa kukata pointi kwa madereva ili kupisha tathmini ya kina ya mfumo huo.

Katika maelezo yake, Katambi aliwataka madereva kurejea kazini na kuendelea na shughuli zao kwa amani, huku akilitaka Jeshi la Polisi kutowabughudhi madereva kwa kipindi cha siku 14 cha mpito, wakati Serikali ikiangalia hoja zilizoibuliwa na kuzitafutia majibu.

mgomo-1.jpg

Hata hivyo, hali ya sasa ni tofauti na matarajio, jambo ambalo limewaweka katika wakati mgumu abiria walioahidiwa kuanza safari asubuhi ya leo. Baadhi yao wanahangaika kurejeshewa nauli zao huku wakitafuta njia mbadala za kuendelea na safari zao.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Mustafa Mwalongo, amesema wamiliki wa mabasi nao wameanza kupata shinikizo kutoka kwa abiria wanaotaka kurejeshewa nauli zao.

“Ni kweli, hakuna basi lililoondoka hadi sasa. Madereva bado wanaendelea na mgomo. Tunajaribu kadri ya uwezo wetu kuzungumza nao ili waanze kutoa huduma, kwa sababu hata wamiliki tunapata hasara,” amesema.

Mwananchi limezungumza na mmoja wa dereva, ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema uamuzi uliotolewa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani, katika kushughulikia changamoto hawajauelewa hivyo bado wanahitaji Waziri Mkuu,Dk Mwigulu Nchemba akawasikilize.

"Jana alitoa uamuzi kwa baadhi ya mambo lakini hatujakubaliana kwa sababu hii kazi wengine tunaitegemea kwa kila kitu kulisha familia, Kodi ya pango na kusomesha watoto inakuaje tunafanyiwa namna hii," amesema

mgomo-2.jpg

Jana, kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Katambi kililazimika kusimama mara kwa mara kutokana na baadhi ya madereva kushinikiza Waziri Mkuu afike kuwasikiliza na kueleza namna atakavyoshughulikia changamoto zinazowakabili.

Hali hiyo ilimfanya Waziri Katambi kutoa ufafanuzi kuhusu kutokuwepo kwa Waziri Mkuu, akisema ameshindwa kuhudhuria kutokana na majukumu ya Kitaifa na kwamba yupo nchini Kenya kwa shughuli hizo.

mgomo-3.jpg

Hadi kikao hicho kilipomalizika saa moja na nusu usiku licha ya madereva kuagizwa kuendelea na shughuli zao, nyuso za madereva wengi hazikuonyesha furaha. Baadhi yao walibaki katika makundi mbalimbali wakijadiliana kuhusu hatua zilizotangazwa na Waziri Katambi.

Hadi sasa 7:45 asubuhi hakuna basi lolote lililotoka.

Hii taarifa nimeinakiri kwenye Gazeti la kila siku la Mwananchi
CCM CHANZO CHA MATATIZO
 
Mimi opinion yangu tofauti kidogo ! Nadhani nia ya serikali ni njema sana ili kupunguza ajali barabarani ...madereva wetu wengi wanaendesha magari kwa mazoea ni wagumu kufuata sheria ! Hii sheria hata ulaya ipo na madererva kule wako makini sana
Tatizo letu mambo muhimu tunaingiza siasa ..ukiangalia hili tatizo wazee wa kubeba matukio wamelibeba na kuanza kulitumia kwenye siasa zao
Nia ni nzuri lakini kwa aina ya polisi tulio nao unaona madereva watakuwa salama kweli mana watakuwa wanakatwa point wakigoma kutoa chochote kitu!

Labda tujikite katika teknolojia kama huko Ulaya. Si umeona malalamiko ya madereva wengine wanasema LATRA wana mabasi ya maelekezo yanakimbia hadi spidi 100 lakini inasoma 80
 
Hivi karibuni naona kama viongozi wanajiamulia sana mambo.

Hili suala la point
Kuita wasanii Central kuwasamehe makosa
Vyombo vya ulinzi ni mali ya CCM
Mbunge anataka taarifa binafsi za mlipa kodi
Jezi ni Mbaya
kuzuia Mikutano ya hadhara
......................
........................
..........................

hebu ongezeni mimi nimechoka kutype
 
Kwa nini swala la point linaonekana ni kwa ajili ya madereva wa binafsi?
Wote ni mashahidi jinsi madereva wa gari za seikali wanavyovunja Sheria za barabarani, na huwa hawachukuliwi hatua zozote kwa overtake za hovyo, kutozingatia 50, na mengineyo, hapo ndio linapoingia swala la uonevu na rushwa.
Swala la kunyang'anywa leseni na kuambiwa uifuatilie kwa RPC ni kitu cha kawaida na utaipata kwa mikwala na kutishiwa kuwekwa selo.
 
Watisoma namba .... majiji yote the likes of Dsm, Arusha,Dom, Mwanza, Mbeya na Tanga wanatakiwa kugoma kote .... hii mikoa ndio kitovu cha uchumi wa Tz......

Hapa sasa serikali wataona umuhimu wa madereva.....
Swali... . HIVI wamiliki wa ma_bus wako nyuma ya huu mpango, ama ni madereva tu na umoja wao wameungana ?
Lazima wamiliki wawe nyuma yake na ni watu wenye nguvu na viongozi haohao.. swala lao linashughulikiwa tu .
 
Kwan kwenye hao madereva hakna hata chawa kama LUCAS KUPELEKA UMBEA mapema kwa wanataka kugoma? Hakuna?
 
Back
Top Bottom