Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Madereva wa mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani, Mkoa wa Mwanza, wameiomba Serikali kuingilia kati suala la kufungiwa leseni zao, wakidai kuwa hatua hiyo imekuwa ikichukuliwa bila kufuata utaratibu unaostahili.
Madereva hao wametoa kauli hiyo wakati wakizungumza na Clouds Media jijini Mwanza, katika Kituo cha Mabasi cha Nyegezi, ambapo wameeleza kuwa kufungiwa kwa leseni zao kunawaathiri katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Mkoa wa Mwanza, pamoja na baadhi ya madereva, wamesema endapo hatua ya kufungiwa leseni zao kiholela itaendelea, wako tayari kusitisha huduma ya usafirishaji kuanzia tarehe 29 ya mwezi huu.
Wamesema uamuzi huo unatokana na kile walichodai kuwa ni changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao, huku wakisisitiza kuwa wanahitaji utaratibu unaoeleweka pindi dereva anapokiuka sheria au taratibu za usalama barabarani.
Madereva hao wameiomba Serikali kupitia Wizara pamoja na mamlaka husika kuingilia kati suala hilo mapema, ili kutafuta suluhu na kuhakikisha wanapewa nafasi ya kufanya kazi zao kwa uhuru, huku wakizingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Aidha, wameonya kuwa iwapo hakutakuwa na hatua za kutatua changamoto hiyo kabla ya tarehe waliyotaja, hatua ya kusitisha huduma inaweza kuathiri usafiri wa abiria wanaotumia mabasi hayo kusafiri ndani na nje ya Mkoa wa Mwanza.
Soma pia