Madereva mwendokasi hebu jaribuni kuwa waungwana

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Tukiwa tunasubiri gari ya Kivukoni stendi ya Kimara terminal leo Ijumaa Mida hii saa 7:50. limekuja gari la Kivukoni Express likasimama sehemu ya mabasi ya gerezani badala ya sehemu yake ya kivukoni.

Abiria tukakimbilia kutaka kupanda cha ajabu baada ya idadi ndogo ya watu kupanda na abiria wengine wakikimbilia kutaka kuingia dereva akafunga milango na kuondoka na abiria hao wachache akituacha watu tukishangaa.

Hii sio fair kwa kweli, hasa kwa siku yenye changamoto ya usafiri kama leo na pia hapa ni mwanzo wa gari dereva unakimbilia wapi?

Baadhi ya madereva udart mnatunyanyasa jirekebisheni.
 
Hawa jamaa wanahitaji elimu ya kumjali mteja(customer care)kuna siku nilikuwa natoka Dodoma, nikawa namuuliza dereva nikiwa na ticketi ya kwenda Manzese ili nijue kama ndo basi natakiwa kupanda.Wakati namuuliza huku nimeshikilia tiketi akaichukua mkononi na kuichana!
 
Kisha ikawaje mkuu? Ukinijibu nitakuwa nimejua jinsia yako
 
Ningekuwa na ID yako, kwanza angekula vibao 2 vitakatifu ndio natoa ID.
 
Hahaha huo ndio utararibu wenzako ticket inachanwa ndio unapanda hizo Basi ....huu mradi unajifia vibaya Sana...
Hivi kama nauli unalipiwa na kampuni ila unatakiwa Kupeleka ticket utafanyeje na imechanwa.
 
Hahaha huo ndio utararibu wenzako ticket inachanwa ndio unapanda hizo Basi ....huu mradi unajifia vibaya Sana...
Hao madereva wanajisikia utafikiri wanaendesha ndege utakuta hata kama unajaribu kuniulizia swali kuhusu hilo gari la luti ipi kimara au morocco halikujibu utakuta limenuna utafikiri limelishwa mavi asubuhi na mke wake
 
Ni fair, hawa jamaa hawajalipwa mishahara na wana familia, si mmeipa CCM ushindi wa 98% , nendeni lumumba mkawadai si kuja hapa kulia lia.
 
Kitambulisho kilisaidia nini badala ya kumzaba kibao huoni alitaka kukuua mkuu[emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…