Madereva na barabara.

Madereva na barabara.

pachawako

Senior Member
Joined
Mar 30, 2024
Posts
120
Reaction score
315
Habari wana JF.
Nimehamasika fungua huu uzi baada ya kukoswa koswa leo na ajali, barabarani kweli kuna mengi na nisehemu inayobeba roho za wengi. Ukiwa umekosea step kidogo tu kuna uwezekano wakubadiri au kumaliza historia ya maisha yetu au ata kuharibu vyombo vyetu tunavyo vipata na kuvitunza kwa ghalama kubwa.

Naomba ukiwa na swali kuhusu sheria za barabarani au kuhusu chombo chako chochote uliza tuweze kupatiana maarifa zaidi.
 
Swali kwa madereva wenzangu.
Hivi ni hatua gani mnachukua ikiwa umekutana na gari kubwa( ROLI ) limepaki kwenye njia upande wako
(LEFT WAY) ikiwa wewe na waliopo nyuma yako mpo speed?

Binafsi leo ninekutana na iyo shida, niliamua kuovertake (uvivu wa kupunguza gia ) lakini kabla sijaingia mazima nilipishana na Land Cruiser ilikua kibati na sikua nimeona maana mbele ya ile njia kuna kona ndogo, nilipaki pembeni baada ya tukio na nikawaza ni vipi nifanye sikunyingine nikikutwa na hali kama hii ila sijapata majibu.
 
Kuna kitu hukuzingatia ndio maana ukapatwa na hali hiyo ,cha kwanza unapotaka kulipita gari la mbele yako liwe limesimama au linatembea lazima uache nafasi ya kutosha kati yake na wewe hii itakusaidia endapo itokea gari nyingine mbele yako unaweza kurudi kwenye upande wako. Ukienda nit pale watakufundisha udereva wa kujihami itakusaidia sana barabarani
 
Naona wengi mmeisema NIT itabidi niizingatie
 
Back
Top Bottom