lordchimkwese
JF-Expert Member
- Nov 16, 2015
- 1,914
- 3,356
Mzee double lane kuna mambo ya ku keep distance??Wewe siyo dereva makini. Dereva makini anaendesha gari 5 akiwa barabarani. Ya kwake, ya mbele, nyuma, na kulia na kushoto.
Ni jukumu lako kumlinda wa mbele yako, tena hili halina mjadala. Yaani hata kama wa mbele anacheza zigzag, ni sharti umlinde usimgonge, kama unabisha gonga halafu traffic aje. Tena utoe sababu eti jamaa alikuwa anayumba? Traffic atakuambia hukuweka umbali unaotakiwa wa mita 3. Yaani, unatakiwa uone matairi ya gari ya mbele yanazunguka. Ukisogelea sana na usipoyaona matairi ya mwenzako ujue muda wowote unamgonga. Sijui udereva mnasomea wapi?
Huwa ninasikitika sana, lakini hakuna namna.
Kingine, hapa mtoa mada analalamikia mwendo wa 30KM. Kimsingi, huu mwendo haukatazwi na sheria. Sanasana, kama speed limit inasoma 50km/hr, ukitembea 30km siyo kosa. Kosa, ambalo utapewa karipio iwapo ukibainika, ni kutembea speed 20 wakati limit ni 50. Ila Kama hamna limit ukiwa 50 hakuna kosa.
Lakini pia Kuna speed limit za 20 na 30. Mfano, barabara ya kutoka Marangu Mtoni kwenda Rombo ina kona nyingi na miteremko. Speed limit sehemu kubwa ni 20 na 30. Sasa kuna madereva wengine wanataka ukiwa njia hii basi ukanyage 50 na 60 Jambo ambalo ni hatari. Nimeshuhudia huu usumbufu na mwingine anaovertake sehemu hatari.
Udereva siyo kujua kuendesha chombo Bali ni nidhamu, kujua na kutii sheria. Na hapa ndipo kuna wasumbua wengi. Hata Jana Singida ile ni ajali inatokana na wrong over taking.
Tujifunze utii
We upo kulia mwenzio kushoto unaakaa mbali ili iweje?