Madereva tuliowahi kukutana na vichapo toka kwa raia na abiria

Madereva tuliowahi kukutana na vichapo toka kwa raia na abiria

Kingsharon92

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Posts
8,560
Reaction score
12,277
Natumai wote mu buheri wa afya pole kwa wale wanaosumbuliwa na mara Mungu awafanyie wepesi.

Tukutane madereva tuliowahi kucheza kichapo toka kwa raia na abiria.

Mimi nakumbuka ilikuwa mwaka 1993 nimebeba abiria toka Geita kuja Mwanza gari ikazingua clutch ikabidi tukatafute fundi Sengerema mjini na kama unavyojua enzi hizo simu hakuna tukaenda kufika mjini acha tukatafute kula maji ya TBL tunarudi tuko chakari chaka tunakuta abiria wamefura balaa wakaanza kutukana mimi nikawajibu mbovu aiseee usiombe nilichezea vitasa ikabidi nilale mbele bila kupenda.

Ya pili nilichezea kichapo cha wafanyabiashara mnadani niligoma kupakia mizigo yao halafu gari limebaki langu na inatakiwa wasafiri nilikimbia na kuzama ofisini kwa mtendaji bila kupenda.
 
Nakumbuka kumgonga bodaboda Arusha wenzake wakataka kuchoma gari moto nikatoa mashine na kupiga juu wote wakatawanyika nikaenda Polisi kutoa taarifa ilikuwa mwaka 2010
 
Nakumbuka 1987 nikiwa naendesha basi txd 50 Isuzu maarufu (kichwa ng'ombe) Arusha-Tanga ilizingua gia box,ilibidi tulale hadi siku ya pili,nlikua nimebeba wachezaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanakuja kaka, mimi najifunza hapa!
 
Back
Top Bottom