Shing Yui
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 15,168
- 38,049
Kuna mmoja namjua vizuri tu nae ananifaham, sasa siku moja nashuka na pikipiki kutokea stendi kuu ya Arusha nikaona jamaa kaniovateki mbio na pikipiki yake inapiga kelele hatari kama baruti..., sasa kwa kuwa na mimi nipo vizuri kwenye pikipiki nikaunga nae ili nione mwisho wake.
Tumeenda wee akageuka akaniona nipo nyuma yake akaanza kufanya sifa, mara apige moshi tatu tatu, mara aachie stelingi ilimradi tu ananioshea. Sasa alipokaribia roundabout ya samunge akalala kwenye pikipiki huku ipo mwendo.... Ile anataka ainuke akunje kona kwenye hiyo raund about kofia la sweta yake likawa limevaa kwenye keria ya pikipiki 😅
Kitendo cha dakika sifuri jamaa alfurukuta pale kwenye pikipiki lakini kofia likawa halijaachia na ndio yupo kwenye kona... Kilichotokea alipandia yale maua pale kwenye mzunguko wa barabara akaanguka humo lakini hakufa wala hakuumia sana