Madereva wa kampuni ya mabasi ya Sauli wamshambulia abiria aliyeripoti kuhusu mwendokasi

Madereva wa kampuni ya mabasi ya Sauli wamshambulia abiria aliyeripoti kuhusu mwendokasi

fantastic philip

Senior Member
Joined
Oct 17, 2015
Posts
195
Reaction score
688
Dereva wa basi la Kampuni ya Saul T 485 DXE wamemshambulia abiria kisa kureport gari ikiwa na speed 115-120.

Kutokana na story ya muhusika anasimulia kuwa alikua na App ya kusoma speed ya gari na kutuma kwenye group la wasafiri mojawapo.

Baada ya muhusika kurecord tukio hilo kwenye group alipokea DM za vitisho kutoka kwa namba tofauti.

Baadae kidogo alipigiwa simu na dereva wa gari hilo na kumtaka asogee mbele yani atoke siti hiyo akakae mbele kwa dereva, alipofika dereva alimpokonya simu na kumtishia.

Baada ya safari kwenda kwa saa kadhaa bila muhusika kupewa simu yake ilifika hatua abiria huyo alitaka kushuka sehem inayoitwa Uyole wakati anataka kushuka walimzuia na kumtaka asishuke kwamba wanampeleka polisi kwa kosa la kurekodi na kuwachomea maovu yao.

Abiria alijitahidi kuwaomba na kuwasisitiza lakini waligoma na kuondoka nae pasipo kumpeleka polisi (utekaji huu).

Baada ya kufika mwisho wa safari walishusha abiria wote na kubaki wao madereva na baadhi ya watu wachache na kuanza kumhoji na kumpiga kwa kumlazimisha kusema nani amemtuma kurecord maovu ya kampuni yao ya SAUL na ilifikia hatua ya kumlazimisha amtaje moja ya mtu wa kampuni shindani ya New force.

Baada ya kipigo na vitisho vya muda mrefu walikagua simu na kujaribu kuweka namba za baadhi za watu waliohisi wao ndio wamemtuma ila walikuta abiria huyo hana namba za wahusika hao kabisa, ndipo walipomlazimisha kuformat simu yote na vitisho juu.

Baada ya muda walimuachia abiria huyo akiwa na majeraha maeneo ya mgongoni kutokana na kipigo walichomshushia.

Kutokana na taarifa hiyo inaonesha ukanda huo Dar mpaka Tunduma kumekuwa na ajali nyingi sana sababu ya rushwa na madereva kujiona tayari wameshika system.
 
Back
Top Bottom