Madereva wa magari Stendi Kuu Lindi wagoma kutokana na wingi wa faini za barabani na kuzuiwa leseni zao

Madereva wa magari Stendi Kuu Lindi wagoma kutokana na wingi wa faini za barabani na kuzuiwa leseni zao

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

1736328646940.png

Madereva wa Magari yanayofanya safari za Nachingwea, Ruangwa, Liwale, Mtwara na Masasi kutokea Stendi kuu ya Mabasi Mkoani Lindi wamegoma hii leo januari 8, 2025 kwa kile walichokieleza kuchoshwa na utitiri wa faini barabarani na kufungiwa leseni zao na Jeshi la polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani

Hali hiyo inatajwa kuathiri shughuli za usafiri na usafirishaji hususani kwa abiria wanaoelekea kwenye maeneo hayo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali huku wengi wao wakiwa ni wafanyabiashara na wangonjwa wanaolekea hospitali kupata huduma

Wakizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva aliyefika kusikiliza kero zao madereva hao wamesema biashara kwao inakuwa ngumu na wanashindwa kufikisha hesabu kwa wamiliki wa vyombo kutokana na kupigwa faini Zaidi ya tatu kwa siku na wakati mwingine faini wanaandikiwa bila hata makossa

1736328692793.png

Akizungumzia kuhusu faini hizo mkuu wa usalama barabarani wilaya ya Lindi amesema hakuna dereva ambaye anaonewa katika kuandika faini isipokuwa wengi wanavunja sheria za barabarani huku akiwataka kuhakikisha wanapakia level seat na kutembea mwendo unaohitajika kisheria

Aidha mkuu wa wilaya ya Lindi Victoria mwanziva amewataka madereva hao kurudi barabarani na kwamba changamoto hizo watakaa na kuzijadili baadae katika kikao na wao huku akiwaasa askari wa usalama barabarani kutanguliza hekima kwanza

Hata hivyo madereva hao bado wamegoma wakisema hawataingia mpaka leseni zao zitaporudishwa na kutatuliwa kero zao .

1736328814624.png
 
Hata mimi nisingerudi aisee, mapolisi na matrafiki ni waonevu sana

Nikiwa na gari mimi navunja miguu na viuno tu
 
Back
Top Bottom