Madereva wa mtandaoni wafanya maandamano kuitangaza huduma mpya ya posta iitwayo swifpack

Madereva wa mtandaoni wafanya maandamano kuitangaza huduma mpya ya posta iitwayo swifpack

KIJICHO PEVU

Member
Joined
May 4, 2024
Posts
69
Reaction score
49
Umoja wa Madereva wa Mtandaoni (UMM) umefanya maandamano ya amani leo Juni 26, 2025, katika jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kutangaza na kuhamasisha matumizi ya SwifPack huduma mpya ya usafiri wa mtandaoni iliyoanzishwa na Shirika la Posta Tanzania.

Huduma hii ya kisasa ilizinduliwa rasmi Januari 2025 ikiwa na malengo mahsusi ya kuwawezesha madereva kupata jukwaa rafiki, salama na lenye makato nafuu, huku ikiboresha huduma za usafiri wa abiria kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Akizungumza kwa niaba ya Postamasta Mkuu, Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Ferdinand Kabyemela, alisema kuwa uzinduzi wa SwifPack ni sehemu ya mageuzi ya Shirika katika kuboresha huduma kwa wananchi kwa kutumia mifumo ya kidijitali, sambamba na kuinua kipato cha madereva nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UMM, Bw. Issa Swahibu, alisema kuwa ujio wa SwifPack umepokelewa kwa furaha kubwa na madereva wa mtandaoni, kwani unaleta suluhisho la changamoto mbalimbali walizokuwa wakikumbana nazo kwa muda mrefu, zikiwemo tozo kubwa na ukosefu wa uwazi katika mifumo ya awali.

"SwifPak si tu mfumo wa usafiri, bali ni jukwaa la kijamii na kiuchumi linalolenga kumkomboa dereva wa Kitanzania," alisisitiza Bw. Swahibu.

Tangu kuzinduliwa kwake, SwifPak imeweza kusajili zaidi ya madereva 6,000 na inalenga kuwafikia madereva 20,000 ifikapo mwisho wa mwaka 2025, ikiwa ni ishara ya kukua kwa kasi kwa huduma hii.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania

IMG-20250627-WA0074.jpg
IMG-20250627-WA0061(1).jpg
IMG-20250627-WA0036(1).jpg
IMG-20250627-WA0015(1).jpg
 

Attachments

  • IMG-20250627-WA0075.jpg
    IMG-20250627-WA0075.jpg
    604.3 KB · Views: 36
  • IMG-20250627-WA0046(1).jpg
    IMG-20250627-WA0046(1).jpg
    476.5 KB · Views: 31
  • IMG-20250627-WA0029(1).jpg
    IMG-20250627-WA0029(1).jpg
    307.7 KB · Views: 39
  • IMG-20250627-WA0008.jpg
    IMG-20250627-WA0008.jpg
    625.9 KB · Views: 37
  • IMG-20250627-WA0040(1).jpg
    IMG-20250627-WA0040(1).jpg
    430 KB · Views: 32
  • IMG-20250627-WA0057(1).jpg
    IMG-20250627-WA0057(1).jpg
    882.6 KB · Views: 35
Shida ipo kwenye kupata abiria maana huyu bolt ameshika na inavyo onekana ameshindikana na ndio maana anafanya anavyotaka yeye.
 
Waweke bei nafuu kuliko Bolt na wawe nà customer care nzuri.

Lkn kwa ninavyoijua nchi hiii, huduma yoyote ya serikali huwa ni mbaya. Watajaza ndugu na jamaa wa viongozi ktk huo mtandao na huduma itakuwa mbaya mno.
 
Umoja wa Madereva wa Mtandaoni (UMM) umefanya maandamano ya amani leo Juni 26, 2025, katika jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kutangaza na kuhamasisha matumizi ya SwifPack huduma mpya ya usafiri wa mtandaoni iliyoanzishwa na Shirika la Posta Tanzania.

Huduma hii ya kisasa ilizinduliwa rasmi Januari 2025 ikiwa na malengo mahsusi ya kuwawezesha madereva kupata jukwaa rafiki, salama na lenye makato nafuu, huku ikiboresha huduma za usafiri wa abiria kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Akizungumza kwa niaba ya Postamasta Mkuu, Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Ferdinand Kabyemela, alisema kuwa uzinduzi wa SwifPack ni sehemu ya mageuzi ya Shirika katika kuboresha huduma kwa wananchi kwa kutumia mifumo ya kidijitali, sambamba na kuinua kipato cha madereva nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UMM, Bw. Issa Swahibu, alisema kuwa ujio wa SwifPack umepokelewa kwa furaha kubwa na madereva wa mtandaoni, kwani unaleta suluhisho la changamoto mbalimbali walizokuwa wakikumbana nazo kwa muda mrefu, zikiwemo tozo kubwa na ukosefu wa uwazi katika mifumo ya awali.

"SwifPak si tu mfumo wa usafiri, bali ni jukwaa la kijamii na kiuchumi linalolenga kumkomboa dereva wa Kitanzania," alisisitiza Bw. Swahibu.

Tangu kuzinduliwa kwake, SwifPak imeweza kusajili zaidi ya madereva 6,000 na inalenga kuwafikia madereva 20,000 ifikapo mwisho wa mwaka 2025, ikiwa ni ishara ya kukua kwa kasi kwa huduma hii.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania

IMG-20250627-WA0007.jpg
IMG-20250627-WA0002.jpg
IMG-20250627-WA0005.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250627-WA0004.jpg
    IMG-20250627-WA0004.jpg
    128.6 KB · Views: 37
  • IMG-20250627-WA0008.jpg
    IMG-20250627-WA0008.jpg
    158.9 KB · Views: 35
  • IMG-20250627-WA0008(1).jpg
    IMG-20250627-WA0008(1).jpg
    158.9 KB · Views: 38
  • IMG-20250627-WA0003.jpg
    IMG-20250627-WA0003.jpg
    99.6 KB · Views: 38
  • IMG-20250627-WA0001.jpg
    IMG-20250627-WA0001.jpg
    106.4 KB · Views: 33
  • IMG-20250627-WA0006.jpg
    IMG-20250627-WA0006.jpg
    149.2 KB · Views: 29
Kwanza nawapongeza kwa kuweza kuandaa huduma hii ya kizalendo. Ya Kwetu hii. Na tuiunge Mkono.

Changamoto ni kuwa wanataka kupitia hii huduma, kwa route Ile Ile bei ya Mchana otofautiane na bei ya Usiku. Wanasema Usiku risk ni kubwa hivyo bei iwe kubwa. Kwa namna Fulani hawataki kumpa unafuu mteja bali kumuongezea Mzigo.

Nawashauri waachane na mpango huu ili huduma Yao iweze kuwa shindani.
 
Back
Top Bottom