Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 157
- 155
Baadhi ya madereva wa magari ya serikali katika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, wamelalamikia madai ya kuamrishwa kuacha sehemu ya mafuta wanayopewa kwa matumizi ya magari yao, ili kiongozi wao aitumie kwa matumizi binafsi.
Kwa mujibu wa madereva hao, kila wanapopewa kibali cha kuchukua mafuta — kwa mfano lita 30 — hupewa maelekezo yasiyo rasmi kuacha takribani lita tano, kabla ya kuondoka kituoni anbacho kinamilikiwa na mfanyabiashara wa mjini Maswa Bw Walji.
"Mara nyingi tunaandikiwa lita 30 lakini tunaambiwa tuchukue lita 25 tu, zile tano zinazobaki kiongozi anazichukua na kuweka kwenye gari lake binafsi," alisema mmoja wa madereva aliyeomba hifadhi ya jina kwa sababu za kiusalama.
Madereva hao wamedai kuwa mfumo huu wa hujuma umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu tangu DAS huyo,Athuman Kalaghe ateuliwe kushika wadhifa huo miaka miwili iliyopita hali inayosababisha baadhi ya magari kushindwa kutekeleza majukumu kikamilifu kutokana na upungufu wa mafuta.
Mmoja wa madereva alisema kuwa walipojaribu kulalamika kwa uongozi wa juu, waliitwa na kuonywa dhidi ya "kuvujisha siri" na kwamba hatua kali zingechukuliwa iwapo wangeendelea kulalamika.
Vitendo vya aina hiyo ni ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma na kwamba endapo taarifa hizo zitathibitika, hatua kali za kinidhamu zichukuliwe na mamlaka yake ya uteuzi.
"Mafuta yanatolewa kwa matumizi rasmi ya magari ya taasisi, si kwa matumizi binafsi ya mtu yeyote. Hili ni kosa kubwa.
Taarifa hizi zimeibua maswali mapya kuhusu uadilifu wa matumizi ya rasilimali za umma katika baadhi ya taasisi nchini, huku wadau wa uwajibikaji wakitaka uchunguzi huru ufanyike haraka.