KERO Madereva wa Taxi Mtandao - Morogoro tukitaka kuchukua abiria Kituo cha SGR tunalipia ushuru mara 2

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Madereva wa Taxi Mtandao tunaofanya kazi mkoani Morogoro. Kero yetu kubwa ni suala la maegesho eneo la SGR. Tunapokwenda kituoni kuwachukua abiria wanaotumia, hatupewi nafasi ya kuegesha ndani ya parking ya SGR wakati tukisubiri abiria.

Kinachotokea ni kwamba madereva wa Taxi za Kawaida, wakishirikiana na baadhi ya Askari Polisi waliopo eneo hilo, hawataki sisi kuegesha ndani ya parking hiyo. Tunashinikizwa tutoke nje ya eneo la kituo na kusubiri abiria pembeni ya barabara au maeneo ya nje.

Tatizo linakuja pale tunapokuwa tumeshapata oda ya kumchukua abiria ndani ya kituo, tukitoka nje kusubiri, tunalazimika kuingia tena kumfuata abiria anapofika. Hali hii wakati mwingine inatufanya tulipie ushuru wa maegesho mara mbili, jambo ambalo linaongeza gharama na kupunguza kipato chetu.

Sisi hatupingi madereva wa taxi za kawaida kufanya kazi zao, wala hatuombi kupewa upendeleo. Tunachoomba ni kuwepo kwa utaratibu unaotambua pia uwepo wa Taxi Mtandao na kutupatia sehemu rasmi ya kusubiri abiria ndani au karibu na kituo cha SGR bila kusumbuliwa.

Tunaiomba Serikali, uongozi wa SGR pamoja na mamlaka zinazohusika na usafiri zilitazame suala hili na kuweka utaratibu wa wazi kwa taxi zote za kawaida na za mtandao. Tunachohitaji ni mazingira sawa ya kufanya kazi bila kubughudhiwa au kulazimishwa kulipa gharama mara mbili.
 
Duh poleni. Taxi mtandao inapigwa vita sehemu zote. Airport ndio kabisa. Nakumbuka back then 2018 nilipiga sana izo mishe. Bolt enzi izo Taxify waliniita hadi kupiga tangazo. Ila changamoto na kero nyingi sana hiyo kazi.

Kama mna umoja wenu hapo mkoa, muwasilishe malalamiko yenu kama kikundi mtasikilizwa.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mtoa mada mamlaka haziwezi kuwaruhusu muingie ndani kwa namna hiyo
 
Madereva wa Taxi Mtandao tunaofanya kazi mkoani Morogoro. Kero yetu kubwa ni suala la maegesho eneo la SGR. Tunapokwenda kituoni kuwachukua abiria wanaotumia, hatupewi nafasi ya kuegesha ndani ya parking ya SGR wakati tukisubiri abiria.

Kinachotokea ni kwamba madereva wa Taxi za Kawaida, wakishirikiana na baadhi ya Askari Polisi waliopo eneo hilo, hawataki sisi kuegesha ndani ya parking hiyo. Tunashinikizwa tutoke nje ya eneo la kituo na kusubiri abiria pembeni ya barabara au maeneo ya nje.

Tatizo linakuja pale tunapokuwa tumeshapata oda ya kumchukua abiria ndani ya kituo, tukitoka nje kusubiri, tunalazimika kuingia tena kumfuata abiria anapofika. Hali hii wakati mwingine inatufanya tulipie ushuru wa maegesho mara mbili, jambo ambalo linaongeza gharama na kupunguza kipato chetu.

Sisi hatupingi madereva wa taxi za kawaida kufanya kazi zao, wala hatuombi kupewa upendeleo. Tunachoomba ni kuwepo kwa utaratibu unaotambua pia uwepo wa Taxi Mtandao na kutupatia sehemu rasmi ya kusubiri abiria ndani au karibu na kituo cha SGR bila kusumbuliwa.

Tunaiomba Serikali, uongozi wa SGR pamoja na mamlaka zinazohusika na usafiri zilitazame suala hili na kuweka utaratibu wa wazi kwa taxi zote za kawaida na za mtandao. Tunachohitaji ni mazingira sawa ya kufanya kazi bila kubughudhiwa au kulazimishwa kulipa gharama mara mbili.
ushuru shingapi
 
Back
Top Bottom