Madereva wa Uber, Taxify na Rova Dar es Salaam

Madereva wa Uber, Taxify na Rova Dar es Salaam

D Vice

Member
Joined
Sep 24, 2018
Posts
59
Reaction score
40
Madereva wenye uzoefu na kazi na wanaoijua kazi wanapatikana kwa wakazi wa Dar es salaam ,Dodoma na Mwanza.

SIFA ZAO

★Wanajua ufundi wa magari
★Wamepitia mafunzo ya udereva
★Hawana rekodi mbaya ya kutokamilisha hesabu
★wastaarabu
★Wasafi

Wasiliana na sisi tunguunganishe moja kwa moja na dereva kupitia Email hapo chini.

jobsfacilitators@gmail.com

Kwa gari ya mkataba hesabu yake ni Tsh 200,000/= kwa wiki.nahuduma zote za service zitafanya dereva . Kwa mda wa mwaka mmoja na nusu (pia itategemea na hali ya gari kwa mda huo) baada ya hapo gari inamilikishwa kwa dereva. Kwa mda huo mwenye gari utakuwa umeshapatiwa jumla ya kiasi cha Tsh14,400,000/=.

Kwa gari ya hesabu .hesabu yake ni Tsh160,000/= kwa wiki. Huduma ya service itafanywa na mmiliki wa gari isipokuwa pancha na upepo wa tairi.Hii haina mda maalumu wa ukomo.

Gari zinazohitajika ni Ist,passo,vitz,Ractis,Raum,Ipsum na zingine ndogo ndogo

Wasiliana na sisi kupitia Email hapo chini. Tukuunganishe moja kwa moja na madereva wetu.

jobsfacilitators@gmail.com
 
Sasa hapo si kila mtu atanunuwa Passo ili apate profit nzuri kwa mwaka mmoja na nusu? Maana IST bei zake zimesimama huwa hazishuki na Passo bei yake ni nafuu kidogo, je hamjaliona hilo?
 
Sasa hapo si kila mtu atanunuwa Passo ili apate profit nzuri kwa mwaka mmoja na nusu? Maana IST bei zake zimesimama huwa hazishuki na Passo bei yake ni nafuu kidogo, je hamjaliona hilo?
Biashara ni ubunifu. Hivyo ni vyema kuwa na mawazo yenye faida kama yako. Sio kila mfanya biashara anapata faida sawa na mwingine . Hii ni kwa sababu ya utofauti wa mawazo yao. Hivyo ni vizuri umeligundua hilo. Chakufanya wewe litendee kazi wazo lako.
Sasa hapo si kila mtu atanunuwa Passo ili apate profit nzuri kwa mwaka mmoja na nusu? Maana IST bei zake zimesimama huwa hazishuki na Passo bei yake ni nafuu kidogo, je hamjaliona hilo?
ni kweli , ila hata wa ist anapata faida . Kumbuka ist ni imara na inaweza kufanya kazi kwa muda mrefu na kuingiza kiasi kikubwa ukilinganisha na Passo.

Ila kwa gari ya mkataba wa mwaka mmoja na nusu na kwa wazo lako lina mashiko . Hivyo nakushauri ulifanyie kazi wazo lako kama unamtaji wa kutosha na sio kukaa tu na wazo hilo kichwani bila kulifanyia kazi
 
Kwa taxify,Rova na uber . Gari ulizozitaja hazitoweza kukupa faida . Utagombana tu na dereva kuhusu hesabu.gari yoyote ndogo ikiwa smart na inamuonekano unaong'aa abiria huvutiwa nayo. Iwe vitz, ist hata passo.
Hizo gari ulaji wake wa mafuta ni mdogo sana madanga ya mjini wanapenda brevis na mark x
 
Hii biashara ya mikataba huwa tamu sana. ila sielewagi dereva huyo huyo ukimpa kazi ya hesabu ya 160 kila week anashindwa kufanya kazi kwa weledi. The same happens to pikipiki and bajaji.

Mjanja unalenga IST ya million 8-9 hapo unampa dereva apigie kazi akuletee namba zako za noti kila week. Ikifika 14 unamuachia unalenga ingine tena.
 
Ni kweli kabisa. Mkataba raha . Ila ni raha ukiwa na boss muelewa na boss akiwa na dereva mchapakazi. Na gari iwe nzima. Full stop.
 
Ni kweli kabisa. Mkataba raha . Ila ni raha ukiwa na boss muelewa na boss akiwa na dereva mchapakazi. Full stop.
Tatizo ukiwa muelewa dereva analeta utoto. So inabidi um magufulilaiz ili akili zimkae sawa
 
Hahaha. Uelewa simaanishi uboya . Namaanisha asiwe mzinguaji. Mwingine haelewi kazi anakupa gari inashida kama zote,... gari inatetemeka kama jenereta.

Au unakuta boss anataka hesabu kabla ya mda , anadai anashida nayo. Au kitu kimeisha anatakiwa akinunue yeye anazungusha na hesabu anataka.

Kama ni fire extingusher unakuta trafki wanamfaidi tu dereva boss anabaki kusema pole. Ivyo ndivyo nilivyomaanisha kusema boss muelewa na dereva mchapakazi na gari nzima.
 
Hahaha. Uelewa simaanishi uboya . Namaanisha asiwe mzinguaji. Mwingine haelewi kazi anakupa gari inashida kama zote,... gari inatetemeka kama jenereta. Au unakuta boss anataka hesabu kabla ya mda , anadai anashida nayo. Au kitu kimeisha anatakiwa akinunue yeye anazungusha na hesabu anataka. Kama ni fire extingusher unakuta trafki wanamfaidi tu dereva boss anabaki kusema pole. Ivyo ndivyo nilivyomaanisha kusema boss muelewa na dereva mchapakazi na gari nzima.
eh hapo muhimu boss kuwa muelewa, mi nazungumzia kwa dereva ambae ana kila kitu ila kuleta hesabu haleti
 
Vipi wakuu hamfanyi na bodaboda kama ni kwa njia ya mkataba au kipande. Nina boda yangu namba BLY nimeipaki tu hom naitoa mkataba wa miezi 4 hadi 5
 
Vipi wakuu hamfanyi na bodaboda kama ni kwa njia ya mkataba au kipande. Nina boda yangu namba BLY nimeipaki tu hom naitoa mkataba wa miezi 4 hadi 5
Hapana . Hatuna madereva wa pikipiki (bodaboda) kwenye system zetu kwa sasa. Tuna madereva wakutosha upande wa uber na taxify . Wasiliana na sisi kupitia email yetu jobsfacilitators@gmail.com . Asante.
 
Back
Top Bottom