Madereva waandamana kwenda LATRA wanataka Uber, Bolt wapandishe bei ya nauli

Madereva waandamana kwenda LATRA wanataka Uber, Bolt wapandishe bei ya nauli

Saivi watanzania mnaandamana mnamchukulia maza poa eeh[emoji28][emoji28]
 
Najua hapo LATRA wamekula parking fee za kutosha na faini juu........ukija kucheki baada ya wiki moja cheti kimeshiba.
 
Tumechukua uamuzi mgumu wa kusitisha kwa muda huduma za UberX, UberXL na UberX Saver nchini Tanzania, bidhaa hizi hazitapatikana kuanzia Alhamis ya tarehe 14 Aprili 2022. Kanuni za sasa za usimamizi wa sekta hii zimejenga mazingira ambayo si rafiki na zimekuwa changamoto kubwa katika uendeshaji wa biashara yetu, hadi pale muafaka utakapopatikana, hatutaendelea kutoa huduma za usafiri wa UberX, UberX Saver na UberXL nchini Tanzania.

Tunapenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa dhati - kwa kuchagua mfumo wetu kufanya safari zako jijini Dar es Salaam ambako tumekuwa tukitoa huduma zetu kwa kipindi cha miaka sita iliyopita.

Huu ni wakati mgumu kwetu sote, lakini hii haina maanai kwamba ndio mwisho wa kila kitu. Tuko tayari kushirikiana na mamlaka husika na kuwa na mazungumzo yatakayoleta tija na kujenga mazingira wezeshi na tutarudi na kuendelea na kukupa usafiri wa kutegemewa na wa uhakika ambao umekuwa ukiitumia, baada ya kujiridhisha kwamba mazingira ya kibiashara ni rafiki.

Tunafahamu kwamba hiki ni kipindi kigumu na usumbufu unaotokana na uamuzi huu na tunapenda kukuhimiza uwasiliane nasi kupitia kwenye app ikiwa una maswali yoyote.

Asante Sana, Tanzania!

Timu ya Uber
 
Mafuta yameongezeka kutoka wastani wa shs 2540 mpaka kufikia 2861 ambapo ongezeko ni tshs 321 ongezeko hilo ni sawa na 13% ila sasa cha kushangaza huko mitaani wasafirishaji wanaongeza nauli kwa ongezeko la mpaka 100% mfano kuna baadhi ya maeneo ambako nauli ilikuwa ni Tshs 500 wameongeza imekuwa 1,000 ambayo ni ongezeko la 100% hii si sawa

Hata hao wanaoandamana waruhusiwe tu kuongeza bei ya nauli kwa 13% kukata mzizi wa fitina otherwise watajiongezea wenyewe wapate pa kupigia hela
Na mbolea ilivyo panda bei kwa100% tupandishe bei ya mchele kwa 200%?
Kwa mkulima
Mbolea imepanda 100%
Mafuta ya tractor yamepanda kwa 13 %.
Mbegu kwa 25%.
 
Hai waliogoma kupandisha nauli ndo wazalendo Sasa?

Serikali iwapongeze Uber na bolt[emoji4]
 
View attachment 2184978


Madereva wa taxi za mitandao (Uber na Bolt) wameamua kuandamana mpaka makao makuu ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhnj(LATRA), kudai kupandishwa kwa bei elekezi ambazo licha ya kupandishwa wahusika bado hawazifanyii kazi hali hiyo inatokana na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta

Source: Dar Mpya


==========================================

Madereva wa taksi za mitandao wameandamana mpaka makao makuu ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Jijini Dar es Salaam kudai kupandishwa kwa bei elekezi ambazo licha ya kupandishwa bado kuna wahusika awazifanyii kazi hali hiyo inatokana na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta.

Madereva hao ambao ni wanachama wa Chama cha Madereva wa Mtandaoni (Tanzania Online Drivers Association - TODA) wamedai kuwa wamiliki wa huduma ya Uber na Bolt ndiyo ambao hawataki kupandisha bei ya nauli kitu ambacho kinawaumiza wao.

"Tumekuja LATRA kwa kuwa wao ndiyo waliowapa leseni Uber na Bolt, kuna App nyingine zimeshaongeza bei ya nauli, lakini wao hawataki, hivyo wateja hawawezi kwenda kwenye App yenye bei kubwa.

"Tunataka LATRA wafanye maamuzi, tulikuwa nao leo asubuhi (Aprili 12, 2022) pale Leaders Club, tukashindwana kwa kuwa wao wanaishia kusema wamewaandikia Uber na Bolt barua, kila siku hivyohivyo, ndiyo maana tumewafuata ofisini kwao watuleleze vizuri.

"Muda huu kuna wenzetu wachache tumewachagua wameingia ndani wanazungumza na viongozi, tunasubiri majiu yao," alisema dereva mmoja wa walioandamana.

Kuna App za wazawa kama TANTAXI ambazo ziko vizuri sana na zingeleta mabadiliko ila watu wamekariri uber na Bolt. Uwekezaji pia lazima utazame wawekezaji wa ndani ambao gharama zao za uendeshaji sio kubwa kivile kiasi haitowalazimu kuweka kamisheni kubwa kama ilivyo kwa Bolt na Uber: TanTaxi Passenger - Apps on Google Play. Hii TanTaxi haikati kamisheni kwa sasa na wamedhamiria kutovuka asilimia 10%. Abiria anafaidika na dereva anafaidika na kupata moyo wa kutoka huduma nzuri.
 
Back
Top Bottom