Madereva waandamana kwenda LATRA wanataka Uber, Bolt wapandishe bei ya nauli

Saivi watanzania mnaandamana mnamchukulia maza poa eeh[emoji28][emoji28]
 
Najua hapo LATRA wamekula parking fee za kutosha na faini juu........ukija kucheki baada ya wiki moja cheti kimeshiba.
 
Tumechukua uamuzi mgumu wa kusitisha kwa muda huduma za UberX, UberXL na UberX Saver nchini Tanzania, bidhaa hizi hazitapatikana kuanzia Alhamis ya tarehe 14 Aprili 2022. Kanuni za sasa za usimamizi wa sekta hii zimejenga mazingira ambayo si rafiki na zimekuwa changamoto kubwa katika uendeshaji wa biashara yetu, hadi pale muafaka utakapopatikana, hatutaendelea kutoa huduma za usafiri wa UberX, UberX Saver na UberXL nchini Tanzania.

Tunapenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa dhati - kwa kuchagua mfumo wetu kufanya safari zako jijini Dar es Salaam ambako tumekuwa tukitoa huduma zetu kwa kipindi cha miaka sita iliyopita.

Huu ni wakati mgumu kwetu sote, lakini hii haina maanai kwamba ndio mwisho wa kila kitu. Tuko tayari kushirikiana na mamlaka husika na kuwa na mazungumzo yatakayoleta tija na kujenga mazingira wezeshi na tutarudi na kuendelea na kukupa usafiri wa kutegemewa na wa uhakika ambao umekuwa ukiitumia, baada ya kujiridhisha kwamba mazingira ya kibiashara ni rafiki.

Tunafahamu kwamba hiki ni kipindi kigumu na usumbufu unaotokana na uamuzi huu na tunapenda kukuhimiza uwasiliane nasi kupitia kwenye app ikiwa una maswali yoyote.

Asante Sana, Tanzania!

Timu ya Uber
 
Na mbolea ilivyo panda bei kwa100% tupandishe bei ya mchele kwa 200%?
Kwa mkulima
Mbolea imepanda 100%
Mafuta ya tractor yamepanda kwa 13 %.
Mbegu kwa 25%.
 
Hai waliogoma kupandisha nauli ndo wazalendo Sasa?

Serikali iwapongeze Uber na bolt[emoji4]
 
Kuna App za wazawa kama TANTAXI ambazo ziko vizuri sana na zingeleta mabadiliko ila watu wamekariri uber na Bolt. Uwekezaji pia lazima utazame wawekezaji wa ndani ambao gharama zao za uendeshaji sio kubwa kivile kiasi haitowalazimu kuweka kamisheni kubwa kama ilivyo kwa Bolt na Uber: TanTaxi Passenger - Apps on Google Play. Hii TanTaxi haikati kamisheni kwa sasa na wamedhamiria kutovuka asilimia 10%. Abiria anafaidika na dereva anafaidika na kupata moyo wa kutoka huduma nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…