mlinzi mlalafofofo
JF-Expert Member
- Apr 20, 2008
- 725
- 1,282
Matumizi ya vileo - hii sio rocket science, inajulikana ulevi unapunguza umakini barabarani.
Matumizi ya simu za mkononi hasa ya mara kwa mara - mtu anaendesha huku anachat WhatsApp na kujibu watu s'time kwa text. Hii sio salama kwako na watumizi wengine wa barabara.
Kuendesha kwa mazoea - kuna watu husababisha ajali kwa sababu ya kujiamini kulikopitiliza, mtu anaamini uzoefu wake unaweza kumsaidia kufanya kila atakalo barabarani. Ndugu tambua kuwa haupaswi kuendesha kwa mazoea hata siku moja. Lolote linaweza kutokea barabarani muda wote. kuwa makini muda wote.
Epuka kufanya Ligi za kukimbizana - enenda kwa busara. kuna watu wanaendesha kwa kukimbizana ili kuonesha umahiri wao barabarani au ubora wa vyombo vyao. Hii sio sawa kabisa.
Halafu cha ajabu unakuta mwengine ana kibaby woka chake cha passo au kivitz chake anang'ang'ana kuingia ligi na gari nzitonzito kama cruiser. Hii ni pua pua pua (in stivu nyerere's voice)
Matumizi sahihi ya ishara - taa na indiketa
Karibuni muongezee....