Madereva Watanzania washindwa kuendesha magari ya kisasa Qatar

Madereva Watanzania washindwa kuendesha magari ya kisasa Qatar

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema madereva wa Tanzania waliopelekwa nchini Qatar hawajaajiriwa kutokana na kushindwa kuyatumia magari ya kisasa.

Inaonyesha jinsi Gani Bado tuko nyuma sana , kuwekeza muda rasilimali kwa mambo yasiyo na msingi huku tukikosa fursa kubwa huko duniani kama hivi..wangepata nafasi hao wote fikiria ni familia ngapi zingekwenda kunufaika na KUAJIRIWA kwao mana kila mmoja hapo ana watu (familia) nyuma yake.
 
Usengeusenge mwingi mipasho mipasho baina ya nchi na nchi kuvimbiana vimbiana ujinga ujinga mwingi kutwa kupiga mapambio ya kijingajinga tu na huku uwekezaji kwenye elimu ya teknolojia iliyoendelea kimufumo huko duniani tupo nyuma ya muda na kwetu teknolojia hio ni sifuri halafu kuongozwa na waimba taarabu ni kazi kubwa sana unajua
 
Magari y kisasa wapi. Madereva wanapimwa kwa uwezo wao wa kutafsiri sheria za barabarani , kitu ambacho madereva wengi wa bongo hawajui .Madereva wengi wanajua kupeleka gari mbele ,kurudi reverse na kukata kona , Tena madereva wenyewe wamejifunzia mitaani.Sasa mtu hajawahi hata kuendesha kwenye freeways/motorways halafu utegemee aendeshe kwenye Nchi zenye miundombinu ya kisasa ya barabara
 
Kuna kitu kinaitwa Skilled work force, tunayo yakutosha?.
Tunazungumzia uwekezaji, wawekezaji wakija tunajikuta hatuna skilled workforce ya uhakika na wala hatuna mipango yakuwa na hiyo workforce.
Tunazungumzia vijana kwenda nje kutafuta maisha, hawa vijana wanafika huko hawana utalaam kufananisha na wengine kutoka Nigeria, Kenya matokeo yake vijana wetu wanaishi mitaani tu.

Watunga sera na wenye mamlaka tuanze kuwa serious sasa na hii tuichukue kama case study.
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema madereva wa Tanzania waliopelekwa nchini Qatar hawajaajiriwa kutokana na kushindwa kuyatumia magari ya kisasa.

Hawakupewa specs za magari watakayoenda kuendesha ? Walipaswa kufanyiwa Orientation.Ni kawaida kwa Mfumo mpya.

All in all Tanzania ni taifa maskini sana kuanzia kwenye akili had viongozi.

Imagine Msukuma ndio anatunga sera
 
Back
Top Bottom