Madereva zaidi ya 40,000 wafungiwa na Bolt, wapo wa makosa ya uhalifu

Madereva zaidi ya 40,000 wafungiwa na Bolt, wapo wa makosa ya uhalifu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kampuni ya taski mtandao Bolt imeweka bayana madereva zaidi ya elfu arobaoni (40,000)wamefungiwa akaunti zao kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo makosa ya uhalifu.

Hayo yamebainishwa na Dimmy Kanyankole Meneja wa Bolt Tanzania wakati akibainisha jinsi kampuni hiyo ilivyowekeza pesa nyingi kwenye ofa (discount) ambazo wanazipata wateja baada ya safari.

Amesema suala la usalama kwa wateja ni jambo la msingi hivyo wamekuwa wakishirikiana na mamlaka Latra pamoja na Jeshi la Polisi kuhakikisha huduma zinakuwa zinakuwa salama kwa watu wote.

Amesema toka mwaka 2017 iliyoanza huduma hiyo, tayari wamewafungia madereva zaidi ya 40,000 kutokana na makosa mbalimbali pamoja na yale ya kihalifu.

 
Back
Top Bottom