Madhara tanatokanayo na kufanya mazoezi!!

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
Habari zenu Jf-doctors,.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24,.

Miaka miwili nilikuwa mpenzi mzuri wa mazoezi hasa wa kuinua vyuma vizito lakini kutokana na majukumu yalivyokuwa yakinisonga nikakosa kabisa muda wa kuendelea na mazoezi ikabidi niache kufanya mazoezi,.

Mwaka jana nilianza kuhisi maumivu ya ghafla karibia viungo vyote vya mwili vilikuwa vikiuma isivyo kawaida na hata katika suala la upumuaji nilianza kupata shida maana kifua kilinibana sana nikahofia kwamba huenda hali hii ipelekewa na kuacha kwangu ghafla mazoezi,.

Kutokana na hali hii ya mwili kuchoka na kukosa nguvu pamoja na kifua na mbavu kuniuma nilijaribu kumuona daktari ambaye aliniamuru nifanye x-ray ya kifua( chest x-ray) ambapo matokeo yalionyesha sikuwa na tatizo lolote katika kifua,.

Kutokana na hali hii kuendelea nilirejea tena hospitali ambapo daktari aliniandikia dawa aina ya KoAct baada ya kunipima na kufanya tena x-ray ambapo pia tatizo halikuonekana lakini akiniandikia dawa na kusema itanisaidia katika kuimarisha mifupa ya kifua,.

My take:

Ninapofanya zoezi kama la kukimbia huwa napata unafuu kiasi fulani ingawa hali hiyo haidumu kwa muda mrefu,.


Naombeni ushauri ili niweze kuondokana na tatizo linalonikabili,.

Natanguliza shukrani,..

Cc: MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Endelea kufanya Mazoezi ya kukimbia ni bora kwa afya yako. wewe ulikuwa unafanya Mazoezi ya nguvu ukaacha kwa gafla sasa kurudi kwa hali yako ya kawaida ndio kumetokea madhara hayo ya mwili kuuma ingawa sio maradhi lakini unapotaka kuacha kufanya mazoezi unakuwa unapunguza kufanya mazoezi sio kuacha mara moja sio nzuri jaribu kufanya hayo mazoezi ya kukimbia japo kwa siku mara moja utakuwa upo fit.
 

Nashukuru sana mkuu MziziMkavu,. Umekuwa msaada sana!!
 
Last edited by a moderator:
Kijana katika mazoezi kuna vitu muhimu sana kuzingatia vinginevyo utajiweka ktk hatari. Kwanza lazima warm ups, either unakimbia au unabeba vyuma. Misuli na mwili lazima upashwe moto. Usione teams zinafanya warms ups kabla ya mechi sio suala la kujifurahisha.
Pia ni muhimu sana kuwa na dk 5-10 za cool down na stretching. Kama ni kukimbia ukimaliza laps zako unaweza ku jog kidogo tena kwa speed ndogo na then kutembea mpaka mapigo ya moyo yanapopungua na kuwa normal. Then nyosha viungo na misuli...

Katika kubeba vyuma lazima uwe unafuata mpangilio maalum. Muhimu ni kuwa na defined repetitions, anza uzito kidogo na rudia round 3-5 na baada ya siku kadhaa unakuwa unaongeza uzito kidogo kidogo. Kwa njia hiyo utakuwa unajenga misuli imara bila kujiumiza. Suala kubwa linalojenga misuli ni repetitions na sio uzito mkubwa tuu. Pia lazima misuli ipate muda wa kujijenga hivyo huwezi kuwa unabeba chuma kila siku. Fanya angalau mara tatu kwa week na kuwa na siku za kupumzika. Unaweza kufanya misuli ya aina moja kila siku au kama unajua unafanya nini basi unafanya opposite kila mara. Mfano mimi nafanya kifua na mgongo, bicepts na tricepts na miguu nafanya misuli ya mbele na nyuma then lower back na tumbo.

Kwa ubebaji vyuma kuwa mwangalifu sana sio kwenda kujiokotea vyuma vya magari na kuanza kujibebea utajitengenezea kilema sio muda mrefu !!

 
Mafuluto umeiweka vizuri sana,huyu jamaa yetu nina uhakika kabisa alivamia mazoezi bila kufuata ethics za kufanya mazoezi,ukweli ni kuwa ni hatari sana kwa afya yako inaweza kukuletea kilema na hata kifo,kuna watu wamevunjika mikono,shingo,miguu,nyonga na hata kupasuka mishipa ya damu na kupelekea kifo,mimi nafanya sana mazoezi ingawa umri wangu uko kwenye middle 40's,lakini utaratibu ninao utumia ni kama uliouelezea hapo MziziMkavu na Mafuluto na sijawahi pata madhara yoyote,anza taratibu na malizia taratibu ni nzuri kwa afya yako.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu tupo pamoja haya mambo sio ya kurukia rukia just kwa kuona picha. Ndiyo sifa mojawapo ya JF, tunapeana ilimu ambayo inaweza okoa maisha ya mtu. Umri ni just a number kama unakula tizi, na kujali lishe bora. Mie pia niko huko huko karibia na kweusi lakini vijana nawapeleka puta hawaamini kama ni boli, volleyball au mambo ya pushups na bench presses au wakitaka round ya Nzawisa kinye kinye kisonzo au vunja mifupa. Na siku za mapumziko napiga ulabu kama kazi then maji kwa wingi sana na kupumzika powa. Ikifika jumatatu nakuwa fiti kuanza routine..

Wa buku 7 wanataka kutuaribia JF kisa kutetea wanaotafuna tutoto !!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…