chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,834
- 26,217
Habari zenu Jf-doctors,.
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24,.
Miaka miwili nilikuwa mpenzi mzuri wa mazoezi hasa wa kuinua vyuma vizito lakini kutokana na majukumu yalivyokuwa yakinisonga nikakosa kabisa muda wa kuendelea na mazoezi ikabidi niache kufanya mazoezi,.
Mwaka jana nilianza kuhisi maumivu ya ghafla karibia viungo vyote vya mwili vilikuwa vikiuma isivyo kawaida na hata katika suala la upumuaji nilianza kupata shida maana kifua kilinibana sana nikahofia kwamba huenda hali hii ipelekewa na kuacha kwangu ghafla mazoezi,.
Kutokana na hali hii ya mwili kuchoka na kukosa nguvu pamoja na kifua na mbavu kuniuma nilijaribu kumuona daktari ambaye aliniamuru nifanye x-ray ya kifua( chest x-ray) ambapo matokeo yalionyesha sikuwa na tatizo lolote katika kifua,.
Kutokana na hali hii kuendelea nilirejea tena hospitali ambapo daktari aliniandikia dawa aina ya KoAct baada ya kunipima na kufanya tena x-ray ambapo pia tatizo halikuonekana lakini akiniandikia dawa na kusema itanisaidia katika kuimarisha mifupa ya kifua,.
My take:
Ninapofanya zoezi kama la kukimbia huwa napata unafuu kiasi fulani ingawa hali hiyo haidumu kwa muda mrefu,.
Naombeni ushauri ili niweze kuondokana na tatizo linalonikabili,.
Natanguliza shukrani,..
Cc: MziziMkavu

Last edited by a moderator: