1. Huangamiza nafsi.
"Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake." (Mithali 6:32)
Mtu hufa kiroho, kama ilivyo dhambi yoyote ile humuondoa mtu katika uwepo wa Mungu, na pia huondoa uwepo wa Mungu
kwa mtu na hicho ndicho kifo cha kiroho.
2. Huondoa ufahamu wa mwanadamu.
"Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu." (Hosea 4:11)
Mtu anakuwa hana uwezo wa kuwa na ufahamu wa mambo mema ya kumpendeza Mungu, maana anakuwa hawezi kulitafakari Neno la Mungu, kila
wakati anakuwa anatafakari uzinzi tu.
3. Huchafua hekalu la Roho Mtakatifu.
"Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe." (1Wakorintho 6:18)
a) Uzinzi unahusisha viungo vya mwili, hivyo dhambi ya uzinzi inahusisha mwili moja kwa moja na ambalo ni hekalu la Roho Mtakatifu, (1Wakorintho 6:19)
Na Mungu anasema atamuharibu anayeliharibu au kulichafua hekalu la Roho Mtakatifu, (1Wakorintho 3:17)
b) Pia mwili ni kiungo cha Kristo,
"Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!" (1Wakorintho 6:15)
Swali la kujiuliza ni hili, Kama miili yetu ni viungo vya Kristo, Je, Yesu Kristo atakubali kuuwa na kiungo kichafu? Jibu ni hapana bali atakiondoa na kukitupilia mbali hadi kitakaposafishwa, mtu asipoomba toba ni lazima ataangamia kabisa maana anasema
tawi lisilozaa atalikata na kulitupa katika moto, (Yohana 15:6)
4. Humuunganisha mtu na madhabahu, miungu na ibada za mtu aliyezini naye, ukoo, kabila, nk.
"Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.”
(1Wakorintho 6:16)
Inawezekana kwa macho ya kawaida mtu asione, bali kiroho anakuwa ameshahama katika uwepo wa Mungu na kuungamanishwa na miungu ya yule mtu aliyezini naye, maana tayari wanakuwa mwili mmoja.
Anakuwa hana uwezo wa kumwabudu Mungu wa kweli, hata akiwepo
ibadani anakuwa hawezi kuunganishwa na Mungu kiroho, maana anakuwa tayari ana ibada za kishetani.
Kwa ujumla dhambi ya uzinzi kama zilivyo dhambi nyingine zote humuondoa mtu katika uwepo wa Mungu.
Hivyo tunapaswa kuepuka sana dhambi hii pamoja na dhambi zote ili Mungu asituache, maana Mungu akituacha shetani anachukua nafasi na kuanza kutuendesha.
Omba toba, tubia dhambi zote pamoja na uovu wote, naye Mungu atakusamehe maana anasema atazisafisha dhambi zetu zote,
(Isaya 1:18)Mungu akubariki sana! Mungu atusaidie tukae kwenye kusudi lake🤝🙏