Madhara ya katuni kwa watoto

Madhara ya katuni kwa watoto

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Kwa sisi Waafrika, katuni na movies zina madhara makubwa sana kwa watoto. Kwenye movies na katuni asilimia kubwa ya heroes ni wazungu. Hili suala huwa linamjenga mtoto kisaikolojia kwamba wenye uwezo, wenye maadili, wazuri na wenye sifa zingine nzuri ni wazungu.

Hili linamfanya asijithamini kama mtu mweusi. Utafiti ulionyesha kuwa mtu pekee ambaye anaongeza kujithamini baada ya kuangalia movie na katuni ni mtoto wa kizungu, hasa mvulana wa kizungu. I thought you should know.
 
Siyo kweli. Kutojiamini kwa mtoto kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na namna mtoto anavyotendewa ndani ya familia au jamii - mfano kama anaambiwa maneno makali makali kila siku: lione, hivi hili likoje? Yaani litoto hili! Hili litoto heri lisingezaliwa...! Maneno na matendo yanayomfanya mtoto ajione kila mara ni mbaya au amekosea ndiyo yanayomfanya awe na low-self image au low opinion of himself or herself. Mfano, watoto wangu wanaangalia educative cartoons kila siku na somehow wamejenga uwezo wa kujiamini kwenye kuongea lugha na kufahamu mambo ambayo wasingeyafahamu kama wasingeangalia hizo cartoons. Na mimi mwenyewe najitahidi kuwa nao karibu kila siku na nisipoonekana wanani'miss' sana! Katika mazingira haya kujiona kwao second class kutatoka wapi?
 
Siyo kweli. Kutojiamini kwa mtoto kinachangiwa kwa kiasi kikubwa na namna mtoto anavyotendewa ndani ya familia au jamii - mfano kama anaambiwa maneno makali makali kila siku: lione, hivi hili likoje? Yaani litoto hili! Hili litoto heri lisingezaliwa...! Maneno na matendo yanayomfanya mtoto ajione kila mara ni mbaya au amekosea ndiyo yanayomfanya awe na low-self image au low opinion of himself or herself. Mfano, watoto wangu wanaangalia educative cartoons kila siku na somehow wamejenga kujiamini kwenye kuongea lugha nk.
Siku zote wanao watakuwa wakijiona ni second class, nyuma ya kina Cinderella wanaowaona kwenye movie. Siku zote watatamani kuwa kama wao.
 
Kwani mtu mweusi ame-add value gani hapa Duniani ambayo ni significant hadi mtoto mdogo ajithamini kama mtu mweusi?

Hao watoto wasipojithamini kama watu weusi ni sahihi kabisa.
Movie zimekufanya usijithamini kabisa. Mtu mweusi kaadd vitu vingi duniani pengine kuliko jamii zote za watu.
 
Siku zote wanao watakuwa wakijiona ni second class, nyuma ya kina Cinderella wanaowaona kwenye movie. Siku zote watatamani kuwa kama wao.
Tatizo ni kwamba watoto wanaweza kuiga wanachokiona - wakiona watu wanapigana na wao wakikutana na wenzao wanaanza kujaribisha walichokiona kwenye cartoons. Watoto wanatakiwa waangalie cartoons zinazowajenga na siyo zinazowafanya wawe violent kwa wenzao na ama kuona kila mara matukio ya vita na mauaji. That's bad for child behavioural development.
 
Kwa sisi waafrika, katuni na movies zina madhara makubwa sana kwa watoto. Kwenye movies na katuni asilimia kubwa ya heroes ni wazungu. Hili suala huwa linamjenga mtoto kisaikolojia kwamba wenye uwezo, wenye maadili, wazuri na wenye sifa zingine nzuri ni wazungu.

Hili linamfanya asijithamini kama mtu mweusi. Utafiti ulionyesha kuwa mtu pekee ambaye anaongeza kujithamini baada ya kuangalia movie na katuni ni mtoto wa kizungu, hasa mvulana wa kizungu. I thought you should know.
Mbona wengine tunaangalia animation mpka leo
 
Lea watoto wako vizuri acha kuzingizia cartoon kwenye malezi.
 
Back
Top Bottom