Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Ubora wa kitu chochote huwa ni kati kwa kati.Ukionyesha heshima kupitiliza kwa mtu yeyote unaweza kugeuzwa mtumwa kwa kulazimishwa kuhatarisha maisha yako kwa lengo la kumfurahisha mtu ambaye unamuheshimu kupitiliza.
Vilevile kama hauna heshima kabisa kwa Watu wengine utaonekana upo na kiburi, majivuno, jeuri na dharau jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa maisha yako kwa ujumla, vilevile siku ambazo utakuwa na matatizo utakosa mtu wa kumkimbilia kwa ajili ya kuomba msaada iwe wa kifedha, ushauri n.k
.
Je wajua madhara ya tabia ya kuheshimu Watu wengine kupitiliza?
Ukweli mchungu ni kwamba heshima kupitiliza kwa binadamu mwenzako inaweza kusababisha maisha yako kuwa magumu sana.
Pale ambapo unamuheshimu sana mtu yeyote mpaka mhusika anajua kwamba unamuheshimu kupitiliza ndipo maisha yako yanapoanza kuwa magumu sana.
Mtu ambaye unamuheshimu sana ataanza kukuvunjia heshima kwa makusudi kwa sababu anajua hauwezi kupingana naye kwa jambo lolote.
Mtu ambaye unamuheshimu kupitiliza anaweza kukufokea, kukutukana, kukudhalilisha hadharani, kukufanya kichekesho, kukugombeza, kukukaripia, kukukosoa kwa lugha ya udhalilishaji, kukushambulia kwa maneno makali sana,kuingilia uhuru wa faragha yako,kukupangia namna ya kuendesha maisha yako,kukupanda kichwani, anaweza kukutumia kwa maslahi binafsi, anaweza kukuaminisha kwamba malengo yako siyo ya muhimu lakini malengo yake yeye ni ya muhimu sana.
Watu ambao unawaheshimu kupitiliza hugeuka ukuta wa furaha yako na mafanikio yako kwa ujumla kwa sababu maamuzi yako yote utafanya kwa kuangalia wao watasema nini au watakuonaje lakini wao hawawezi kukuangalia wewe wala kujali utajisikiaje juu ya maamuzi yao na vitendo vyao kwako.
Ukiheshimu Watu wengine kupitiliza siyo kwamba utakuwa kipaumbele kwake bali unageuka mtumwa kwake.
Jifunze kupingana na mawazo ya watu ambao unawaheshimu bila kuwavunjia heshima,bila kuonyesha ubabe, udikteta,ujeuri, ujuaji, misimamo mikali - Unaweza kusema "Ninaheshimu sana mawazo yako japokuwa Sikubaliani na mawazo yako kwenye kipengele 1, 2,3 kwa sababu nipo na mtazamo tofauti kuhusu jambo hili"
Hapa unaonyesha heshima kwa watu wengine lakini hauonyeshi kwamba upo tayari kugeuzwa mtumwa kwa sababu tu unamuheshimu sana mhusika.
Jiwekee mipaka.Hata kama utakuwa unaonyesha heshima kwa mzazi, mwenza, rafiki,ndugu wa damu, bibi, au babu, mwajiri, mwalimu wako, mfanyakazi mwenzako, mshauri wako,mfano bora wa kuigwa (role model), kiongozi wako wa dini, supervisor wako n.k lazima wajue nini hauwezi kuvumilia kutoka kwao sio wajione kama malaika kisha wafanye chochote juu yako eti tu kwa sababu wanajua unawaheshimu kupitiliza.
Wapendwa wako wanatakiwa kujua haupendi nini,makosa gani unaweza kusamehe na makosa gani kamwe hauwezi kusamehe bali unaweza kufanya maamuzi magumu sana bila kujali maneno ya wakosoaji wako.
Ukweli ni kwamba mtu ambaye anajua kwamba unamuheshimu kupitiliza hawezi kukuheshimu hata kidogo.Anaweza kufanya makosa makubwa sana kwa makusudi kabisa kisha anageuza kibao kwako kwa kujifanya hajakukosea bali wewe ndiyo mkosaji umuombe msamaha.
Wapo watu ambao wanafanya makosa kwa makusudi kabisa kisha wanajifanya kukasirika,kununa, kutishia muachane,kususa,kuanza kulia na kutoa machozi ya uongo,wapo wanaofanya makosa kwa makusudi kisha wanakwenda kushitaki lakini wanageuza kibao kwako ubaya wao wanaugeuza kwako na mazuri yako wanajifanya wao ndiyo wanatenda wema sana halafu wewe uonekane mnyanyasaji.
Mtu yeyote ambaye anajua ûnampenda sana, unamuheshimu kupitiliza hauna kujenga tabia ya ubabe, kiburi, dharau, majivuno, jeuri na ujuaji, misimamo mikali,atakupanda kichwani,atakuvunjia heshima kwa makusudi kwa sababu anajua hauna madhara kwake.
Ukiwa mpole kupitiliza, mvumilivu kupitiliza, mnyenyekevu kupitiliza, king'ang'anizi, mstaarabu sana,unataka amani, haupendi migogoro wala ugomvi Watu wengine watakuona DHAIFU,wapo watakuona bwege,wengine watakuona mshamba mshamba kisha watakuharibia maisha yako.
Jifunze kufanya maamuzi magumu sana hasa pale ambapo uonapo heshima yako imevunjwa.
Mtu anaweza kukupenda sana kisha atakuvunjia heshima kwa makusudi,mtu anaweza kukupenda lakini anakusaliti,anakuchafua kila kona,anakusema vibaya anaweza kutishia muachane lakini lengo lake anataka upate hofu uendelee kumbembeleza,umnyenyekee,umuombe msamaha,upige magoti n.k
Katika haya maisha upendo wa dhati ni kupoteza muda.Kitu cha kupigania ni kupewa HESHIMA pekee.