Madhara ya kula nyama ya Nguruwe/Kitimoto kwa afya yako...

Kitimoto ina madhara, bado hatusikii

Speed kills, bado watu hatusikii

Ukimwi unaua, bado condom hazitumiki

Sigara inaua, bado hatuachi

Red meat ni hatari, hatuachi

Pombe ina madhara, hatuachi

Kuku wa kisasa nao pia wanamadhara

Chai/Kahawa zina madhara, ....

Anyway jiulize ni kipi kisicho na madhara?? Jibu ni HAKUNA!!!

ChochOte kinachopitia ktk machine ili kitumike kina madhara pia maana mf machine ya kusaga/kukoboa huwa baada ya muda zile chekecheo au gears zinakwisha na zinabadilishwa...
Swali: vile vyuma huwa vinaenda wapi?

Mf mwingine:
Maji ya azam au kilimanjaro yanapitia ktk machine na baada ya muda machine kwa maana ya vyuma vyake vina kwisha pia....je, vinakwenda wapi?

Kwa kukuhakishieni kuwa haya majanga hayakwepeki ni pale unakapo fikia 55+yrs ndo mara bp, canser, figo, ini, kisukari, etc na ukingalia ndo magonjwa ambayo wazee wote wanakufa nayo. Cha msingi ni kupunga hii risk ila kwa ujumla wakw HAIKWEPEKI!

THE MORE YOU LEARN THE MORE YOU....
 
Whatever you eat make sure that you stay health. Huyu mdudu akipikwa vizuri yuo salama. Chezeya wewe Sitoacha Ng'o kula HOT chair
 

Halafu ukisoma iyo makala ya Washington times unaona kua neurocysticercosis inatokana na fecal-oral transmission, proper hygiene inahusika sana na sio kula nyama tu
 
Kitimoto ni noma, yani wataumba kila jambo ili wapunguze utamu, ila mi hamuuuuu ndio imezidi.
 
Ni kweli nyama zote zina madhara kiafya kama zisipo tengenezwa vizuri. Hivyo ni juu ya mlaji kuhakikisha kuwa anafuata kanuni. Ambacho sikubaliani nacho ni kuona kama nguruwe haifaii kabisa, na kutafuta utaalamu na sababu za kuungaunga kwenye mitandao na source nyingine zisizotegemeka. Nyama zote zinamatatizo yake, na kuona hii nzuri na ile ni mbaya huo ni uamuzi wa mtu. Hivyo basi hicho kichaa cha itikadi cha kusema hii ni haramu na ile ni halali sio kweli. Wewe kama unakula nguruwe, kula kwa afya yako na nafasi yako. Na kama huli basi wanaokula wataheshimu maamuzi yako.

Tuache misukumo ya kiitikadi kwa kuwaamulia wengine cha kufanya. Mara nyingi hizi dini zinaletea watu kichaa na kubaki wakitangatanga kwenye mambo wasiyoyajua wakati waliozianzisha walikuwa na malengo yao ya kihuni na kusingizia eti mungu anataka, Nasi wenye akili finyu tunafuata mkumbo tu.
 

Mdau hapo umenena watu wengi-tena wengi sana-wanatangatanga kwasababu ya hizo imani zao wasizojua kuzitumia. Na, KWELI walichotaka ndo hiki tunachokiona NA WAMEFANIKISHA KWA KWELI. Watu wakiSOMA wakaanza kuiona Dunia katika pembe zaidi ya moja hakika HILI SIO SWALI LA KUJIULIZA WALA KUKUFANYA UTANGETANGE. Jamani tusome tuanze kuwaza nje ya mabox yetu. Na sio kusoma mavitu ya ofisini tuu na siasa hizi uchwara za bongo.
 

Mambo ya Usubi hayo, black fly: Simulium spp!!
 
jamani nashauri ukifika kwa muandaaji wa kitimoto umwambie hivi===akichome na mafuta mpaka uridhike/thoroughly==tatizo limekuea 'undercooking' nawasilisha and you can quote me on this. i cant stop eating fish and that animal.
 

Very true maana kila kitu ukianza kukichunguza, kitakuwa na madhara kama hakuna umakini na kiasi. Hata kuku tunaowashobokea wana matatizo kibao, tukiongelea zoonosis! Na kama tunachukulia mawazo ya kila mtu kuwa ndio kanuni basi tutafuata njia nyingi, check kidogo hapa: Vegan RD: Chicken is not health food

Muhimu kujua misingi ya afya bora na kuchukua tahadhari!
 
Nguruwe pamoja na kuwa anakula vinyesi na vitu vichafu pia ina matatizo mengi ambayo watafiti wamegundua kuwa nguruwe hata akilishwa lishe safi, bado:(i) Ni wanyama wachafu katika mambo

mengine na nyama ya wanyama wachafu ikiliwa inamuathiri mlaji.
(ii) Nyama ya nguruwe ina mafuta mengi zaidi kuliko nyenzo za kujenga misuli.(iii) Ina uwezakano wa kupata magonjwa kuliko aina nyengine yoyote

ya nyama (Abdallah Yusuf Ali,
The Holy Qur'an, Revised and edited by the Presidency of Islamic Researches, IFTA, Call and Guidance, uk. 69).
Athari ya madhara ya nyama hiyo sasa inajulikana vilivyo na kila mmoja.

Asidi ya Uric, inapatikana kwa kila mnyama, na mwili wa mwanadamu pia ina nasibu yake, ambayo inatolewa nje ya mwili na mafigo kwa 90% ya asidi ya uric inatolewa kwa njia hii, lakini chemia ya nguruwe

ni kuwa inatowa nje ya mwili 2% ya asidi yake ya uric pekee. Iliyobaki inabakia ndani ya mwili wake. Hii ni sababu ya kupatikana kwa kiwango kikubwa ugonjwa wa baridi yabisi (rheumatism) wa nguruwe na wale

wenye kula nyama yake (Maulana Wahiduddin Khan, God Arises, uk. 209 – 210).
Dkt. Simpson ana haya ya kusema kuhusu nyama hiyo: "kwa sababu ya kuwa na mafuta mengi, nyama ya nguruwe ina tatizo kubwa kusagwa katika vyakula vyote. Mnyama huyo anaweza kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na lava wa Taenia

solium
hivyo kufanya "tegu (surua ya nguruwe)" na hii tegu inaleta aina ya tegu, T. solium. Inaathiriwa zaidi na Trichinella spiralis ambayo inaleta maradhi ya "Trichinosis" (Imenukuliwa na Yousef Saleem, Pork, A Bad Diet Prohibited by Islam, al-Islam, March/April, 1980, p. 29).
Trichinosis ni ugonjwa ambao unaletwa na

kiinitete cha
Trichinella spiralis wakati vinapohama kutoka kwa utumbo wa mwanadamu mpaka kwenye misuli. Katika wiki ya kwanza baada ya kuvamiwa mtu anaanza kutapika, kuhara na kusikia kichefuchefu. Ugonjwa unapoendelea inaleta matatizo ya kumeza, kuzungumza na kupumua.
Njia moja ya kuzuia ugonjwa

ni kuipima nyama kwa tegu. Lakini Leavell na Clark wameandika: "Kwa vile cysts wa
Trichinella ni wadogo sana kuonekana na macho, uchunguzi huo haufalii kitu. Wajerumani rasmi walikuwa wakifanya uchunguzi kwa hadubini kwa lengo hilo lakini ilikuwa ni ghali sana. Njia bora ya kuepukana na trichinosis ni kupika

bidhaa za nguruwe barabara" (Imenukuliwa na Yousef Saleem,
Pork, A Bad Diet Prohibited by Islam, al-Islam, March/April, 1980, p. 29).
Jambo jengine muhimu ni kuwa nguruwe ana shingo ndogo sana (kwa ndani, ingawa nje inaonekana pana), hivyo kuwa shida kuchinjwa. Hivyo, mwanzo anapigwa na chuma na baada ya

kuzirai ndio anachinjwa. Hii ina matatizo kwa sababu Uislamu umeweka aina yake ya kuchinja ambayo inamfanya mnyama atoe kiwango kikubwa cha damu. Kama tunavyojua ni kuwa damu ni chombo cha

kubeba viini vya ugonjwa na kemikali ambavyo vina madhara na hasa kwa mwanadamu. Kubakia ndani ya mnyama damu huenda kukaleta madhara makubwa kwa mlaji. Na kwa kuwa nguruwe hachinjwi kama wanyama wengine, damu nyingi hubakia ndani ya mwili badala ya kutoka nje.
Mwisho, nyama ya nguruwe ni

chakula duni. Charles Annondale ameandika, "Nyama freshi ya nguruwe, japokuwa kwa wengine inachukuliwa kuwa chakula kitamu, hasa anapouliwa akiwa mchanga, ni lishe duni ukilinganisha na nyama ya ng'ombe au mbuzi na inatumika kwa uchache" (Imenukuliwa na Yousef Saleem,
Pork, A Bad Diet Prohibited by Islam, al-Islam, March/April, 1980, p. 29).



Tukizama kwa makini tutaona ya kwamba Dini zote zimeharamisha nguruwe. Mfano tazama katika Biblia (Agano la Kale), Kitabu cha Walawi:

"Na nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hachuei; kwenu huyo ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama zao wala msiguse mizoga yao"
(11: 7 - 8). Na katika Kitabu cha

Isaya: "Mwenyezi Mungu asema hivi: 'Wapo watu waaojitakasa na kutawadha wapate kuingia katika bustani za ibada za sanamu; wanafanya maandamano na kuhani akiwa kati yao. Watu hao hula nguruwe, panya na vyakula vingine haramu'" (66: 17).

Na katika agano jipya, Yesu anasema: "Msidhani kuwa nimekuja kutangua sheria na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha" (Mathayo 5: 17). Na Qur-aan ipo wazi kabisa kuwa nyama ya nguruwe haifai kuliwa. Allaah Anasema: "Yeye Amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu" (2: 173).
 
MAGONJWA YA NGURUWE



Homa ya nguruwe ni ugonjwa unaoambukizwa kutoka nguruwe mmoja kwenda mwingine kwa kasi kubwa sana ukionyesha dalili mbalimbali. Dalili hizi zaweza kujionyesha dhahili au zisijionyeshe wazi wazi wakati huo ugonjwa ukiwa unasambazwa. Dalili ku inayoambatana na ugonjwa huu ni kuvuja na kusambaa kwa damu kwenye viungo vingi vya mwili wa mnyama.


Nguruwe wenye ugonjwa midomo yao ikiwa inavidonda




Nguruwe wenye ugonjwa wakiwa wamejikusanya pamoja wakiwa na vidoa doa vya damu




Masikio yakiwa mekundu kwa damu iliyoviria ndani ya ngozi


Kuvimba kwa figo zilizojaa damu




Madhara yake kwa nguruwe yanaweza kuwa makubwa au madogo yasiyoweza kuonekana kwa macho. Homa ya nguruwe haina tiba maalumu wala

chanjo inayofaa na hivyo uzuiaji wa ugonjwa huu unategemea sana utambuzi wa ugonjwa mapema na kisha kuzuia utembeaji wa holela wa nguruwe (karantini). Maonyo yamekuwa yakitolewa kupitia mikutano ya hadhara na vyombo vya habari kama magazeti ya kuzuia kutembea kwa mifugo ovyo

pamoja na kuzuia kula nyama ya nguruwe kwa kuhofia kusambaa kwa ugonjwa. Kiambatanisho Na 1 na 2 hapa chini vinaonyesha elimu iliyotolewa kwa mlipuko huo yaliyochapishwa na magazeti mawili tofauti kwa siku moja yakiashiria umuhimu wa ugonjwa huo.


Ugonjwa huu umekuwa ukitokea mara kwa mara katika nchi yetu na kuathiri mifugo na soko la nguruwe kwa ujumla. Ugonjwa huu uliripotiwa kwa mara ya kwanza Tanzania mwaka 1914 ukifuatiwa na mlipuko mwingine mwaka ya 1962. Mlipuko mkubwa wa ugonjwa huu ulilipotiwa na Tasisi ya utafiti ya

wanyama (ADRI), Dar es Salaam miaka ya 1987 an 1988 na kusababisha hasara kubwa sana kijamii na kiuchumi katika mikoa ya Mbeya, Arusha na Kilimanjaro. Tafiti zilizo fanywa na wataalamu wa magonjwa ya virusi (Misinzo na wenzake, 2011) kwa kutumia sampuli kutoka Chunya, Ileje, Kyela,

Loliondo, Ludewa, Temeke and Tukuyu zilizokusanywa kati ya mwaka 2010 na 2011 wakati wa mlipuko zilionyesha kuwepo kwa ugonjwa maeneo hayo. Ugonjwa huu kwa nchi yetu umekuwa ukiripotiwa kama mlipuko ukianzia maeneo ya Mbeya ambako unaaminika kutoka nchi ya jirani ya Malawi. Mwezi

may 2011, mlipuko wa ugonjwa pia ulilipotiwa Dar es Salaam nah ii inatokana na sababu kwamba Dar es Salaam sasa imekuwa na wafugaji wengi wa nguruwe kwa vile ufugaji wa nguruwe unaonekana kuwa na faida kubwa kwa mfugaji.
 

Kweli Msimbo. Unajua kila mtu ana hiari ya auchaguzi. Pia ndio kusema wao wanajua sana sayansi kuliko wala nguruwe? Hapana, tena wala nguruwe na walevi ndio wenye maendeleo na wako mbele kisayansi, tiba, na mambo mengine ya kijamii kuliko wanaosema haramu au kutumia lugha nyingine za kukataza. Uchaguzi ni wa mtu kusuka au kunyoa.
 
Nguruwe haramu tu. Hata mumtetee vipi. Na aliyekataza kumla si mtume Muhammad ila ni Mwenyezi Mungu.
 
Haka kamnyama katam bana ikiwezekana wengi muache ili nibaki mimi na jamaa zangu kama 7 hivi tuendeleze utamaduni wa kununua kilo 10 kabla ya Castle lite barrriiiiiiiiiidiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
NIMEKULA KITI MOTO VIPELE VIDOGO VIDOGO VIMEOTA SHINGONI JE NI UGONJWA GANI:sleepy::sleepy:
 
lan Rosemary Alvarez alijikuta akiwa na maumivu ya kichwa na mkono kukosa nguvu. baada ya kufanyiwa scanning ikaoneka kama ni "brain tumor", pindi alipofanyiwa upasuaji alikutwa na "mnyoo (taenia solium)" akiwa hai unakula brain yake. Chanzo hasa cha mnyoo huo ni kula nyama ya nguruwe ambayo kitaalamu anaprotein nyingi kuliko mnyama yoyote na hivyo kuvutia parasite wengi kwa mnyama huyu . Je ni watanzania wangapi wanapata uangalizi wa kugundua afya zao na wanakula nyama hii kila siku tena inayofugwa katika mazingira si salama?. soma zaidi kwenye link hii hapa chini


chanzo. https://www.jamiiforums.com/jf-doct...-nyama-ya-nguruwe-kitimoto-kwa-afya-yako.html
 
Last edited by a moderator:

Kitimoto shushia Konyagi minyoo yote kwishney
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…