Madhara ya kula nyama ya Nguruwe/Kitimoto kwa afya yako...

Madhara ya kula nyama ya Nguruwe/Kitimoto kwa afya yako...

Ni Wapi aliposema Yesu kuleni Nguruwe katika Biblia ? mimi ndio ninayotaka usilete maneno yako ya mafumbo hapa toa Aya inayosema hivyo RGforever

SI MIMI GOMBANA NA MANENO YA YESU

"KIINGIACHO MWILINI HUTOLEWA CHOONI"
Na Nguruwe huliwa na Kutupwa Chooni kama Kinyesi..

"SAFISHENI KWANZA ROHO ZENU NA KILA KITU KWENU KITAKUWA HALALI"
[UNAACHA KULA NGURUWE NA KUMWITA NAJISI WAKATI WEWE NI MZINZI NA MWASHERATI wa kutupwa]

kama Umeenda SHULE utajua nini maana ya Mafumbo na Tafsiri zake Lakini kama shule yako ni Madrasa bora usisumbuke.

Nakushangaa wewe uliyefundishwa Darasa la nne/Tano Mafumbo leo unaniambia nisikuletee Mafumbo. Inadhihirisha jinsi gani hukuelewa huko shule na Elimu yako ni Matatizo
 
Last edited by a moderator:
Kumb. 14:8 Nguruwe pia ni najisi,
ingawa ana kwato zilizogawanyika, hacheui.
Msile nyama yake wala kugusa mzoga wake.

Mkuu Zomba ni sahihi kwa andiko hilo. Lakini umejiuliza alikuwa anamwambia nani? Kifupi, MUNGU alikuwa ameahidi kwa nyumba ya Ibrahim. Sasa ili kuhakikisha lengo linatimia, aliamua kuwatenga waahidiwa kujizuia kufanya mambo fulani wakati jamii nyingine inaruhusiwa kufanya. Walawi, ndio waliochanguliwa kwa ajili hiyo, hivyo kuwatenga na watu wengine wa nyumba ya YAKOBO, Mungu akawapa sheria hiyo ya nini wale, nini wasile. Ni walawi tu nasisitiza.

LAKINI

Mwanzo 9:1-4 inaeleza tofauti.
9
Ndipo Mungu akambariki Noa na wanawe,
akiwaambia, ‘‘Zaeni mkaongezeke kwa
idadi na mkaijaze tena
a
dunia.
Wanyama wote
wa duniani, ndege wote wa angani, kila kiumbe
kitambaacho juu ya ardhi na samaki wote wa
baharini wamekabidhiwa mikononi mwenu, nao
watawaogopa na kuwahofu.

3
2
Kila kitu chenye
uhai kiendacho kitakuwa chakula chenu. Kama
vile nilivyowapa mimea mbalimbali, sasa
nawapa kila kitu.

“Lakini kamwe msile nyama ambayo bado
ina damu ya uhai wake, kwa maana damu ni
uhai.
4
Hakika damu ya uhai wenu nitadai.
Nitadai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa
kila mwanadamu pia nitadai kwa ajili ya uhai wa
mtu mwenzake.

Hapa Mungu alisema na NUHU, ni baada ya wanadamu wote kuteketezwa, hivyo alikuwa akiongea na dunia nzima. Anayekataa kula kitimoto, si kwa sababu Mungu kamkataza, bali ana alegi nayo, kama wengine walivyo na aleji na kuku, mbuzi, kondoo na wanyama wengine.

Ubishi wenu ndio unawaponza! Wewe kula tu ukikuwa utaacha!
 
Siwezi kula nyama najisi chafu aliyoharamisha Mwenyeezi Mungu mimi ni muungwana SPANERBOY UDZUNGWA

Tukizama kwa makini tutaona ya kwamba Dini zote zimeharamisha nguruwe. Mfano tazama katika Biblia (Agano la Kale), Kitabu cha Walawi: "Na nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hachuei; kwenu huyo ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama zao wala msiguse mizoga yao" (11: 7 - 8). Na katika Kitabu cha Isaya: "Mwenyezi Mungu asema hivi: 'Wapo watu waaojitakasa na kutawadha wapate kuingia katika bustani za ibada za sanamu; wanafanya maandamano na kuhani akiwa kati yao. Watu hao hula nguruwe, panya na vyakula vingine haramu'"(66: 17).
Na katika agano jipya, Yesu anasema: "Msidhani kuwa nimekuja kutangua sheria na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha" (Mathayo 5: 17).

Na Qur-aan ipo wazi kabisa kuwa nyama ya nguruwe haifai kuliwa. Allaah Anasema:
"Yeye Amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu" (2: 173).

Nguruwe pamoja na kuwa anakula vinyesi na vitu vichafu pia ina matatizo mengi ambayo watafiti wamegundua kuwa nguruwe hata akilishwa lishe safi, bado:
(i) Ni wanyama wachafu katika mambo mengine na nyama ya wanyama wachafu ikiliwa inamuathiri mlaji.
(ii) Nyama ya nguruwe ina mafuta mengi zaidi kuliko nyenzo za kujenga misuli.
(iii) Ina uwezakano wa kupata magonjwa kuliko aina nyengine yoyote ya nyama (Abdallah Yusuf Ali,The Holy Qur'an, Revised and edited by the Presidency of Islamic Researches, IFTA, Call and Guidance, uk. 69).

Athari ya madhara ya nyama hiyo sasa inajulikana vilivyo na kila mmoja. Asidi ya Uric, inapatikana kwa kila mnyama, na mwili wa mwanadamu pia ina nasibu yake, ambayo inatolewa nje ya mwili na mafigo kwa 90% ya asidi ya uric inatolewa kwa njia hii, lakini chemia ya nguruwe ni kuwa inatowa nje ya mwili 2% ya asidi yake ya uric pekee. Iliyobaki inabakia ndani ya mwili wake. Hii ni sababu ya kupatikana kwa kiwango kikubwa ugonjwa wa baridi yabisi (rheumatism) wa nguruwe na wale wenye kula nyama yake (Maulana Wahiduddin Khan, God Arises, uk. 209 – 210).

Dkt. Simpson ana haya ya kusema kuhusu nyama hiyo: "kwa sababu ya kuwa na mafuta mengi, nyama ya nguruwe ina tatizo kubwa kusagwa katika vyakula vyote. Mnyama huyo anaweza kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na lava wa Taenia solium hivyo kufanya "tegu (surua ya nguruwe)" na hii tegu inaleta aina ya tegu, T. solium. Inaathiriwa zaidi na Trichinella spiralis ambayo inaleta maradhi ya "Trichinosis" (Imenukuliwa na Yousef Saleem, Pork, A Bad Diet Prohibited by Islam, al-Islam, March/April, 1980, p. 29).

Trichinosis ni ugonjwa ambao unaletwa na kiinitete cha Trichinella spiralis wakati vinapohama kutoka kwa utumbo wa mwanadamu mpaka kwenye misuli. Katika wiki ya kwanza baada ya kuvamiwa mtu anaanza kutapika, kuhara na kusikia kichefuchefu. Ugonjwa unapoendelea inaleta matatizo ya kumeza, kuzungumza na kupumua.

Njia moja ya kuzuia ugonjwa ni kuipima nyama kwa tegu. Lakini Leavell na Clark wameandika: "Kwa vile cysts wa Trichinella ni wadogo sana kuonekana na macho, uchunguzi huo haufalii kitu. Wajerumani rasmi walikuwa wakifanya uchunguzi kwa hadubini kwa lengo hilo lakini ilikuwa ni ghali sana. Njia bora ya kuepukana na trichinosis ni kupika bidhaa za nguruwe barabara" (Imenukuliwa na Yousef Saleem,Pork, A Bad Diet Prohibited by Islam, al-Islam, March/April, 1980, p. 29).

Jambo jengine muhimu ni kuwa nguruwe ana shingo ndogo sana (kwa ndani, ingawa nje inaonekana pana), hivyo kuwa shida kuchinjwa. Hivyo, mwanzo anapigwa na chuma na baada ya kuzirai ndio anachinjwa. Hii ina matatizo kwa sababu Uislamu umeweka aina yake ya kuchinja ambayo inamfanya mnyama atoe kiwango kikubwa cha damu. Kama tunavyojua ni kuwa damu ni chombo cha kubeba viini vya ugonjwa na kemikali ambavyo vina madhara na hasa kwa mwanadamu. Kubakia ndani ya mnyama damu huenda kukaleta madhara makubwa kwa mlaji. Na kwa kuwa nguruwe hachinjwi kamawanyama wengine, damu nyingi hubakia ndani ya mwili badala ya kutoka nje.

Mwisho, nyama ya nguruwe ni chakula duni. Charles Annondale ameandika, "Nyama freshi ya nguruwe, japokuwa kwa wengine inachukuliwa kuwa chakula kitamu, hasa anapouliwa akiwa mchanga, ni lishe duni ukilinganisha na nyama ya ng'ombe au mbuzi na inatumika kwa uchache" (Imenukuliwa na Yousef Saleem, Pork, A Bad Diet Prohibited by Islam, al-Islam, March/April, 1980, p. 29).

Tunayopata katika maagizo na shari’ah ya Kiislamu kuhusu mbwa ni kuwa yeye ni najisi na pia ni haramu kuliwa. Hivyo, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuagizia kuwa ikiwa mbwa ataramba chombo chochote basi chombo hicho kioshwe mara saba moja wapo ikiwa ni kwa mchanga. Na utafiti wa sasa unaonyesha kuwa katika umaji maji wake vipo viini ambavyo ni hatari haviwezi kuuliwa wala kuondoshwa isipokuwa kwa mchanga, kwani mchanga una vitu ambavyo vinaua viini hivyo. Kwa kuwa maslahi ya mwanaadamu anayeyajua ni Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala). Na pia mbwa kama carnivorous (walaji nyama) wengine wanakula vitu vingi hivyo kuliwa na binadamu inamtoa katika ule ustaarabu na unaweza kumletea maradhi mengi kwa ajili ya hilo.

Ukichanganya na ndizi bukoba we acha tu .mate yananitoka
 
Last edited by a moderator:
gonga tena mdudu....
uone kama utatoka vipele...
utazoea tu, tupiamo.
 
Jana kuna mshikaji kanikuta faragha nakula haka kamdudu, akanicheka sana, eti anadai haka kamdudu huwa kanakuwaga mwezini na kutoka damu kama mademu, je nikweli waungwana? mimi nishakuwa mraibu wa hii kitu, kunawakati naweza kufululiza kama lunch wiki nzima, kwa ufupi haishi wiki bila kukatafuna haka ka haramu, kwasasa napatashida kwakuwa nimefunga, natamani mfungo uishe hata kesho.

hakika ww co muislam na acha porojo zko za kutaka kupotosha umma na dhana yako ya kidini........
kwa maneno yako ww ni Bwana Sensa....... kimbia kafanye kaz yko
 
attachment.php

Asprin

Mbona ngamia nae kapasuliwa kwato na amehalalishwa sinagogini?
 
Last edited by a moderator:
Mbona ngamia nae kapasuliwa kwato na amehalalishwa sinagogini?
[h=2]Kumbukumbu la Torati, Chapter 14[/h][SUP]14:7[/SUP] Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang'a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;

[SUP]14:8[/SUP] na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse. Bujibuji
 
Last edited by a moderator:
mi naomba niulize kitu kimoja kabla hatumjabishana saana ina maana nikila nguruwe siku nikifa nitahukumiwa mbele ya haki kuwa ulikuwa unakula nguruwe?? assume kuwa mambo yoote nilikuwa nafanya mema isipokuwa kula nguruwe? ebu jadilini vitu vingine vya maana sio hivi tafadhali maana tunaishi kwa unafiki sana watu mnaambiana unakula najisi wakati anaemwambia mwenzake anafanya najisi zaidi ya kula nguruwe, please stop it
 
huwezi kuhukumiwa kwa kula nguruwe, ila kwa matendo maovu,
 
huwezi kuhukumiwa kwa kula nguruwe, ila kwa matendo maovu,

asante
je na yule anaemwambia kuwa unafanya dhambi kwa kula nguruwe wakati yeye anafanya maovu mengine zaidi ya kula nguruwe huyu mtu tumuiteje??
 
Hana mpya huyo. Kakurupuka tu na hiyo info kutoka ABC bila ku-digest. Tunamsaidia kumpiga shule analeta ubishi. Nikagundua kuwa nasomesha degree kwa mtoto wa miaka minne! Nimem-shit na elimu yake finyu ya minyoo. Isitoshe akienda lab huyo, anaweza kutwa na hiyo minyooo....

Kweli ibilisi atakwenda na wengi motoni kama alivyoahidi.
 
Nguruwe ambapo katika mwili wake hukusanyika jumla ya vijiumbe maradhi visivyoondoka kwa kuoshwa
Mdomo ni maficho ya vijidudu, bakteria na virusi vinavyokwenda kwa binadamu na wanyama.
Baadhi yake vinamhusu nguruwe, mfano wa kidudu kiitwacho Trchinella, nywelenywele ziitwazo Balantidium Dysentery, wadudu wa tumbo (Taenia Solium) na mchango wa nguruwe (Spiralis). Baadhi yake huingizwa kwenye maradhi mengi ya pamoja baina ya binadamu ( Cysticercosis & Influenza) na wanyama.

Minyoo (Ascaris na Fasciolopsis Buski) hupatikana kwa wingi nchini China.

Maradhi ya Balantidiasis hupatikana kwa wachunga nguruwe na wenye kuchanganyika nao, na yanaweza kuenea kwa sura ya mlipuko kama ilivyotokea katika moja ya visiwa vya bahari ya Pacific baada ya kimbunga. Maradhi yanakuwepo panapokuwepo nguruwe katika nchi zilizoendelea kiviwanda kinyume na madai ya uwezekano wa kuushinda uchafu wake kwa kutumia teknolojia mpya zinazoharamisha kula nyama bila ya kibali, hasa nchini Ujerumani, Ufaransa, Philippines na Venezuela.
Kwa kula minofu ya nyama ya nguruwe, (Trichinellosis) hupatwa na ugonjwa wa Balantidium Dysentery. Kwani mke hubungua kuta za matumbo kwa ajili ya kuweka mayai ambayo yanafikia kiasi cha 10,000. Mayai hayo huingia kwenye misuli kupitia damu na kugeuka kuwa ni vijiyai vyenye kuambukiza.
Ama kupata maradhi kupitia mchango wa nguruwe, ni kuwa hiyo hupatikana baada ya kula minofu ya nguruwe mwenye ugonjwa.

Minyoo hukua kwenye mchango wa binadamu na urefu wake unaweza kufikia meta saba, na unakuwa na kichwa chenye miba inayosababisha kukwaruzika kwa kuta za michango na mchupo mkubwa wa damu, na ana mirija minne na shingo. Aina za mke huzaliwa kama kwamba ni wanyama pekee na hufikia maelfu. Na katika kila mmoja kati ya mnyama, huzaliwa zaidi ya mayai elfu moja iwapo utakula Cysticercosis.

Kupatwa na ugonjwa wa minyoo ya tumbo la binadamu, hutokana na kula chakula kilichoingia mayai na kutoa lava, na huingia katika damu kupitia kiungo chochote. Na hatari yake hukisiwa kwa mujibu wa umuhimu wake.
Maradhi haya hayatokei kabisa kutokana na kupatwa na mchango usio na miba katika kichwa na wenye madhara madogo
kabisa Taenia Saginata ya ng’ombe.

KIIMANI
kwa upande wa Quran
"Yeye Amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu" (2: 173).

KWA UPANDE WA BIBILIA
“Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao” wala msiguse mizoga yao (Walawi 11: 7 – 8).

Pia nimsikia kuwa nyama ya nguruwe ndio inaingoza kwa kusababisa magonjwa mengi ya kansa

na pia hivo vijidudu vilivopo kwenye nyama ya nguruwe hata vipikwe vipi havifi vinahamia kwenye mwili wa anayekula hiyo nyama na kumea huko

Mnataka kututoa kwenye issue ya msingi........ Umbumbumbu unawatawala
 
Back
Top Bottom