Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukizitumia kwa Muda mrefu unakuwa Mtumwa. Hutaweza kufanya tendo la Ndoa mpaka uboostiwe na dawa husika.
Pili,siyo rafiki kwa watu wenye matatizo ya moyo na shinikizo kubwa la damu. Kwa sababu moyo utalazimishwa kusukuma damu kwa speed kubwa kuelekea katika kiungo chako,inaweza kusababisha hata kifo.
Tatu,kushindwa kulala kwa uume. Dawa hizi mara nyingine zinaweza kusababisha uume ushindwe kulegea hata baada ya kufanya tendo husika.
Nne,gharama za kununua dawa husika ni kubwa. Kidonge kimoja kinanunuliwa kwa sh 2000 mpaka 4000 kwa baadhi ya maeneo. Upatikanaji wake pia ni ngumu.
Tano,baadhi ya Wapenzi na wanandoa hawapendi matumizi yake. Hivyo inaweza kuleta mtafaruku na mwishowe aibu na Mafarakano.
Kuna dawa zingine ukizitumia na bahati mbaya hukupata kile ulichokusudia,basi inasababisha hata kubaka kwa sababu mashine inaweza ikashindwa kulala.
Madhara yake ni Mengi na nakushauri usizitumie kama afya yako ipo fiti. Wagonjwa wa Kisukari ndiyo hutumia mara chache kutokana na kushindwa kusimamisha na mwenza wake akawa na uhitaji wa tendo hilo.