Madhara ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango huku wanawake wakisahau njia bora ya kupanga uzazi ni kutumia kondom na kalenda tu

Pamoja na kusaidia wengi kumbuka kuna madhara ambayo huwezi kuyaona kwa muda mfupi ni mpaka baada ya miaka kadhaa na ni makubwa kuliko unavyotarajia,mbona kondomu ni nzuri tu kutumia?
Hakina ambacho hakina madhara dunia ya leo chamsingi nikuangalia kile chenye madhara kidogo.Swala la kalenda nalo sio la kuamini sana kwasababu miili ya wanawake ina mambo mengi na wako wanawake wengi sana hawajui au hawazingatii hizo tarehe.na pia condom hapa napo kuna changamoto,wanaume wengi tunatumia condom kwa mwanamke mpya ila mkishazoeana au mkeo hii kitu haina tena kazi.Nenda uko vijijini hudhuria dispensar siku ya clinic ndo utaona kulivyo na umuhim wa hizo dawa.
 
Mkuu matumizi ya hivyo vitu hasa condomu na calendar ni comitment tu ya mtu binafsi ndizo ambazo tunatumia na mwenza wangu siku ambazo hazieleweki condomu ila muda mwingi ni Calendar njia moja nzuri sana na rahisi kutumia......sema waliowengi hawajui kuitumia kazi yao kubwa ni kuangalia tu tarehe badala ya kucheki pia na mabadiliko ya mwili ikiwemo ute utolewao siku husiku.......ni rahisi sana hii kitu
Mi nachosema tu hapa kila mtu afanye anavyoona inafaa maana kumbadilisha mtu si suala dogo
 
Kwa faida ya wengi please tuelezee jinsi ya kutumia/hesabu kalenda na nini cha kuangalia kwenye hayo mabadiliko ya mwili (ute etc.) Naamini utasaidia wengi.
 

Kwa kweli hizi dawa siyo nzuri...binafsi nimezitumia na madhara nimeyaona. Niko kwenye mchakato wa kuziacha na kurudia njia za asili.
 
Ushauri wangu:
Kama uko kwenye ndoa na bado unazaa, usitumie hizi dawa. Tumia njia za asili, hata ikitokea umepata mimba, itakuwa ni sawa tu maana ulikuwa una mpango wa kuzaa anyway.
Kama ushamaliza kuzaa, bora kufunga kizazi. Hii itakufanya kuwa huru/kujiachia na mwenza wako bila wasiwasi wa kupata mimba,
Kama bado hujaolewa, tumia kondom/kalenda. Hakuna sababu ya kutumia madawa….
 
Hakuna dawa isiyo na maudhi(side effects) ktk mwili wa binadamu ,mf. Piriton ni maalumu kutibu mzio lkn ukinywa utasikia uchovu na usingizi cha muhimu ni kupata hitaji lililokusudiwa na hayo maudhi yasiwe permanent.
Ndio maana kabla ya kupewa njia unaeleweshwa jinsi inavyofanya kazi na side effects zake na zaidi ya hapo unasaidiwa kufanya uchaguzi kwa njia iliyo sahihi kutokana na jinsi ulivyo au kama una matatizo mengine ya kiafya.
Labda kwa kumalizia uzazi wa Mpango ktk nchi yetu Si LAZIMA na kila mtu ana haki ya kuelimishwa na kuamua kwa HIARI yake pia uzazi wa Mpango sio kwa Mwanamke pekee hata Mwanaume anaweza shiriki kwa kufunga kizazi.
 
Kama huyo mtoto yupo nenda kamtolee sadaka na kuomba toba na kukataa roho ya kukataliwa!

Manaa huuo akishakataliwa toka akiwa tumboni mwako, so unawwza usije kuamink kitakachomtokea huko mbele ya safari ya maisha.
 
Bora mie nawangu nipo Rombo yupo Dar hatuhitaji njia yoyote maana kwa miezi minne mpaka sita tunakutana mala moja au mbili tena kwa hesabu kubwa. Njia nyingi zimeorodheshwa lakini sijaona Calender.
 
Njia nzur n withdrawal tu kwa wanaume tunaoweza lkn

Kalenda inachange sana na condom ngumu kutumia kabisaa
 
Bora mie nawangu nipo Rombo yupo Dar hatuhitaji njia yoyote maana kwa miezi minne mpaka sita tunakutana mala moja au mbili tena kwa hesabu kubwa. Njia nyingi zimeorodheshwa lakini sijaona Calender.
Si ndio huyu nimelala kwake Jana au
 
Matumizi ya muda mrefu wa dawa hizi yanaweza kupelekea matatizo
1.Figo
2.kansa
3.kisukari
4.UKIMWI.
TUijikite kwenye njia za asili .
Pharmceutical companies create customers not cure.
 
Mi kiufupi nawaombea wote watumiao njia hizo za madawa wasizae milele
 
Ndio maana ma kansa ya vizazi na utumbo yanaongezeka siku hizi na huwez kuambiwa ukweli kwamba hiyo midawa inachangia,mi huwa namwaga zangu nje sitaki drama za njia hizi za uzazi wa mpango na tunaenda vizuri sana na wife ktk kupangilia uzazi wetu,na hii ni tangia enzi hzo hatutaki mimba kabla ya ndoa mpaka sasa ambapo tunataka watoto kwa mpangilio mzuri.
 
Masuala ya kupanga uzaz yana changamoto nyingi. Mimi napenda atumie vidonge kwani sipend condom kabisa. Inaninyima raha ya tendo
 
Hivi ile ya mwanaume akifunga kizazi anakua na uwezo wa kumwaga wazungu?
 
Wewe ni mwanaume mzuri na unamhurumia mkeo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…