Waliokataza kuzini na mke au mume wa mtu walitazama namna ilivyorahisi sana kushawish mke wa mtu kuwa mume wake ana mapungufu na yata tatuliwa nje ya ndoa. Then kamchezo kakianza huwa kanakuwa na addiction mbaya sana lakini ambayo ikiendelea huwa inaibua matatizo yasiyo na ulazima kama wivu,hasira,visasi,ugomvi,mauwaji,kudhuru,kuvubja ndoa na kadharika.
Whatever you do na huyo mke au mume wa mtu jua tu mwisho wake hautakuwa wa furaha wala faida kati yenu lazima utakuwa mchungu kwa namna yoyote ile.
Mfano, mume akigundua kuwa unamlia mkewe,akija kukwambia tu kuwa amejua,hautakuwa na amani tena na mtaanza kurumbana na huyu mke sababu haitakuwa tena siri na mtajawa na wasi wasi muda wote kuwa nini kitawatokea next time mkionana.
Haya tufanye mnafanya siri,je mahusiano yenu mtakuwa ni watu wa usiri siku zote bila kutaka kuwa huru na furaha yenu yaani mtoke out,mtembee,muende fukweni bila kutazama migongo yenu kama kuna mtu anayewajua atawaona?
Ukisema uchukue mke wa mtu baada ya mumewe kukujua na kuamua kuachana nae then utaanza kudeal na version ya mwanamke yule yule ambaye yule aliyemuacha alikuwa anaishi nae. Ataanza kulaumu na wewe kwa mwanaume mwingine, ataanza kukutazama kwa jicho la mapungufu na hivyo atataka mbadala wako. Ataanza kunyata kama alivyonyata kipindi unamuiba ila safari hii ni kunyata na mtu mwingine sio wewe.
Vipi kuhusu majukumu,mke wa mtu ni rahisi sana kudeal nae akiwa kwa mumewe,akija kwako unaanza sasa kuwajibika nae,utamlisha,kumvalisha,kumpa matunzo na watoto kama anao utawajibika kumsaidia plus familia yake inakuhusu sasa kama wakwe.
Kama ni mwanaume wa mtu utaanza sasa kuwa kero kwake maana mlikuwa mnafurahia moments tu zile za wizi. Now mna uhuru majukumu yako kama mwanamke wake yamebadilika unaanza kuwa na ratiba tofauti plus saa hii atakuwa buzy kukutafutia maisha itabidi akutafutie mwenzako wa kumpa utulivu,hapo ndipo shida inaanza tena. Na vipi kama alikuwa na mkewe? Huyo mkewe hawezi kuwa chini yako atakuwa juu yako wewe utakuwa ni mtu aliyevamia mahusiano ya walionza. Mali na vitu ulivyokuta havitakuhusu.
So kiukweli kuna hasara nyingi sana kudeal na mke au mume wa mtu. Tafuta tu mali yako mpya jenga mji wako.