Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Madhara ya mwanasiasa wa upinzani kujiunga na chama Tawala katika SAIKOLOJIA YA SIASA ni makubwa na yana athari za kisaikolojia kwa Jamii, Wafuasi na mfumo wa kisiasa kwa ujumla. ...
Madhara hayo ni pamoja na:
1. Kuimarika kwa Chama Tawala...
Kisaikolojia, hali hii hujenga taswira ya kimapokeo miongoni mwa wananchi kuwa; Hakuna upinzani wa KWELI...
Wananchi wanaposhuhudia wanasiasa wa upinzani wakijiunga na chama tawala, fikra ya mabadiliko hupotea na chama tawala huonekana kama suluhisho pekee, hata kama hakifanyi VIZURI...
Hili hujenga aina ya "uoga wa kisiasa" (political learned conformity), ambapo watu huacha kufikiria TOFAUTI.
2. Upotevu wa Matumaini .....
Wananchi hujifunza kuwa; Hakuna maana ya kupinga au kupigania mabadiliko kwa njia ya kidemokrasia.
Kwa kuwa kila anayesimamia mabadiliko huishia kununuliwa au kuhamia chama tawala, Wananchi hujenga imani ya ndani kwamba juhudi zao hazitazaa MATUNDA...
Hii huathiri ushiriki wao wa kisiasa, na mara nyingine hujiondoa kabisa kwenye masuala ya SIASA....
3. Usaliti wa Kijamii ( Betray Trauma)
Wafuasi huathirika kisaikolojia kwa kuhisi kama "wameachwa" au "kusalitiwa" na mtu waliyemwamini....
Hali hii husababisha mseto wa hisia kali kama hasira, huzuni, na hata msongo wa mawazo (depression). Kwa baadhi, hupelekea kukata tamaa kabisa katika siasa; kwa wengine, huamsha chuki na migawanyiko ndani ya JAMII....
4. Kuimarisha udikteta wa chama tawala....
Chama kinaponyakua wapinzani maarufu, hujiongezea nguvu na huweza kuendeleza utawala wa muda mrefu bila changamoto ya KWELI.....
5. Huchochea sinizimu ya kisiasa. (Political Cynicism)
Hii ni hali ambayo wananchi huamini kuwa; Hakuna tofauti kati ya upinzani na chama tawala - wote ni wale wale- Hivyo; Mwelekeo huu huwafanya kupoteza Imani na mfumo wao wa DEMOKRASIA......
6. Hudhoofisha upinzani....
Huondoa nguvu ya upinzani na ushawishi wake wa kusimamia serikali katika kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa wananchi.
Mwelekeo huu husababisha ukosefu wa uwajibikaji serikalini....
Tuzidi kujifunza, Tusichoke Kujifunza....
Tanzania ni yetu sote...