Madhara ya ongezeko la tozo la miamala katika jamii

Madhara ya ongezeko la tozo la miamala katika jamii

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Jamii zetu zinaishi kwa kutegemeana, familia ndiyo safety net ukipata matatizo. Hatuna desturi ya kutemea ustawi wa jamii tukipata matatizo. Mama mdogo akiwa mgonjwa, familia itatoa msaada wa hali na mali.

Simu zimerahisisha mawasiliano. Leo hii uko Bukoba utatuma pesa ya MRI scan kwa ndugu aliye Dar , utatuma ada ya shule Arusha na hata mama akilalamika amechoka kula tembele atapata 10,000 ya kubadilisha kitoewo wewe ukiwa bado Bukoba.

Sasa kwa kila hela tutakayo tuma katika kusaidiana machungu ya maisha Mwigulu anakata kipande. Yale matumaini kidogo tuliyobaki nayo ya maisha nayo pia yanapigwa panga.

Afadhali ya jana kuliko leo.
 
Screenshot_20210716-002543.png
 
Kuna kitu ccm inakitafuta maana watu tumechoka kujaza matumbo ya watu.so sad[emoji24]Tunakoenda ni kubaya sana tutachoka si mda mrefu.
 
Financial and digital inclusion ndo mwisho wake taratibu tunanitenga na dunia tumerudi karne ya 19 ila nimeipenda jinsi makamouni walivyoiweka vzr sasa kila mtu anaona serikali ya ccm ndo tatizo
 
Lipeni Kodi wakuu,hakuna beberu wakuja kulipa Kodi kwa ajili ya watanzania,let's love our country,kulialia hakuta badili mambo
 
Kama ni kukaba basi wamekaba kooni, kuna watu huko vijijin watapata tabu sana kweny miamala mfano mtu anataka afanyiwe upasuaji wa fasta hospital, labda anategemea mtoto wake aliyepo bukoba atume pesa sasa hayo makato yatasababisha ugumu wa mtu huyu kutuma pesa.

Yaan jamaa kajinyima sana amtumiea mama ake ila nyinyi mnakata ile hela mama anapokea hela kidogo mnamfelisha kupata matibabu.

NASHAULI CCM MRUDI MEZANI HUKU MTAANI WATU WAMEWACHUKIA HATARI.
 
Mama anaupiga mwingi mnoo,

Tulipe sana kodi kwa maendeleo yetu hakuna wa kutuletea zaidi yetu wenyewe.

Humo humoooooooooooooo.
 
Kama ni kukaba basi wamekaba kooni, kuna watu huko vijijin watapata tabu sana kweny miamala mfano mtu anataka afanyiwe upasuaji wa fasta hospital, ...
Unadhani CCM haijui kuwa inachukiwa!? Wajinga ni wale walioamini kuwa ujio wa mama huyu utaleta ahueni ya maisha. Tatizo ni deep rooted kuliko watu wanavyodhani
 
Aina ya maelezo, majibu, thinking, aina ya ujibuji akihojiwa na Clouds 360, bungeni ni anaongea kiujivuni, jeuri, na dharau, dont care fulani, ni kama anasema tumeamua na ndio hivo lazima iwe.

Sina uhakika kama akiba ya BoT ya yale Madola yapo salama, anaemshauri Madam Hassan hakuzoea aina ya majukumu ya kutumika kwa wananchi hasa Miradi kila mahali wamepagawa kuiba wanaiba ila wanaona aibu kutelekeza miradi.

Matembezi ya kwenye miradi ya umeme na reli ya mwendo kasi kuna mtu dhamira yake ni kufifisha ndoto, sasa ili kutafuta ushawishi akaona awapeleke site na wenzake ili awandae vijana wake waje na spinning na alternative thinking kuibua kasoro za kimatumizi kwenye hio miradi.

Aliyetabiri viongozi wa Tanzania hasa Ikulu, Mawaziri na Bunge kuna moto wa laana ya raia inawangoja hakukosea.

Suruali Bwanga ina wenyewe na uvaaji wake una misingi. Jamaa kaacha pia viatu virefu na vipana.

Wa DH na Chachacha hivi viatu hawawezi na hii miradi Samia haiwezi na hata iweza. Mwigulu anaweza ila hana kinywa kizuri cha unyenyekevu na ushawishi.

Swali: Je, kwa nini uzalendo haukuanza na Wabunge na Mawaziri.?

Kampeni ya Samia kuwa Rais 2025-2030 ni haipo na ni ndoto na hawezi kufanikisha. Never afaidi tu kukwapua sasa hivi akapumzike ifikapo 2025
 
Lipeni Kodi wakuu,hakuna beberu wakuja kulipa Kodi kwa ajili ya watanzania,let's love our country,kulialia hakuta badili mambo

Hata mbunge, waziri au kigogo naye wa kulipa kodi hamna?

Na wizi nao kwa mujibu wa CAG nao pale pale?

Wabunge 19 kharam nao mwendo mdundo?

Mashirika yanayozalisha hasara nayo kama kazi?

Tuendelee tu kujikakamua kulipa hadi damu? Wewe utakuwa kati ya wasiolipa au mnufaika wa wizi uliomo, si bure!

Hiiiiii bagosha!
 
Jamii zetu zinaishi kwa kutegemeana, familia ndiyo safety net ukipata matatizo. Hatuna desturi ya kutemea ustawi wa jamii tukipata matatizo. Mama mdogo akiwa mgonjwa, familia itatoa msaada wa hali na mali...
Kuna watu wanapigika mchana kutwa kwa malipo ya shillingi elfu kumi.. Akilipwa hiyo anakata 6000 anatuma kijijini kwa wazazi au familia watoe 5000 kwa wakala wapate kula na matumizi mengine ya lazima(ya muhimu yanawekwa kando) sasa haiwezekani tena kutuma 6000 wapate 5000
 
Hata mbunge, waziri au kigogo naye wa kulipa kodi hamna?

Na wizi nao kwa mujibu wa CAG nao pale pale?....
CAG alipofumua madudu alitolewa madarakani. Juzi tuliambiwa kuna tume imechunguza wizi wa BoT, hakuna kilichotokea na bado tunakabwa tutoe zaidi ili wachote zaidi.
 
Kuna watu wanapigika mchana kutwa kwa malipo ya shillingi elfu kumi.. Akilipwa hiyo anakata 6000 anatuma kijijini kwa wazazi au familia watoe 5000 kwa wakala wapate kula na matumizi mengine ya lazima(ya muhimu yanawekwa kando) sasa haiwezekani tena kutuma 6000 wapate 5000
Sasa unataka nani apigike kwa ajili yao? Kwani huduma si tunatumia wote? Hakuna cha bure
 
Back
Top Bottom