Jamii zetu zinaishi kwa kutegemeana, familia ndiyo safety net ukipata matatizo. Hatuna desturi ya kutemea ustawi wa jamii tukipata matatizo. Mama mdogo akiwa mgonjwa, familia itatoa msaada wa hali na mali.
Simu zimerahisisha mawasiliano. Leo hii uko Bukoba utatuma pesa ya MRI scan kwa ndugu aliye Dar , utatuma ada ya shule Arusha na hata mama akilalamika amechoka kula tembele atapata 10,000 ya kubadilisha kitoewo wewe ukiwa bado Bukoba.
Sasa kwa kila hela tutakayo tuma katika kusaidiana machungu ya maisha Mwigulu anakata kipande. Yale matumaini kidogo tuliyobaki nayo ya maisha nayo pia yanapigwa panga. Afadhali ya jana kuliko leo.