Kama taifa tumefanya kosa kubwa sana kuruhusu na kuulea uchawa. Kwamba mtu anayesifia na kujipendekeza kwa rais anaonekana ndiye mwema na mzalendo sana kuliko yule amabaye anapongeza kimya kimya ama anayekosoa.
Matokeo yake watu wengi wakaanza kuwa machawa na kuanza kushindana vikundi vya kukusanya umbea na kutoa sifa kwa rais. Mfano Samia Queens.
Tishio la Makonda kwa mawaziri wanaodaiwa kuwatumia watu wamtukane "mama yake" mpendwa (kama alivyomuita) ni zao la uchawa uliokomaa. Makonda amedhamiria kuwaharibia wenzake na kujikweza mabegani mwa mama yake ili mradi tu aonekane ni mwema na mtu mzalendo zaidi kuliko wengine.
Kusingekuwa na misingi ya uchawa iliyomwagiliwa, kuchipua, na kukomaa, Makonda asingeweza kuyasema aliyoyasema leo.
Lkn amesoma alama za nyakati na kugundua kuwa uchawa ndicho huwainua watu wengi ndani ya ccm na ndani ya serikali.....acha ajimwage.
Endapo "mama yake" atayafanyia kazi matamshi ya kichawa ya Makonda basi ni dhahiri kwamba watu wengi wasio na hatia wataumia.
Uchawa ni hatari kwa ustawi na.mustakabali wa nchi yetu.