Madhara ya "uchawa" sasa yameanza kudhalilisha na kuumiza

Nchi inaelekea kusiko huyu mama apumzishwe.
Kama taifa tumefanya kosa kubwa sana kuruhusu na kuulea uchawa. Kwamba mtu anayesifia na kujipendekeza kwa rais anaonekana ndiye mwema na mzalendo sana kuliko yule amabaye anapongeza kimya kimya ama anayekosoa.

Matokeo yake watu wengi wakaanza kuwa machawa na kuanza kushindana vikundi vya kukusanya umbea na kutoa sifa kwa rais. Mfano Samia Queens.

Tishio la Makonda kwa mawaziri wanaodaiwa kuwatumia watu wamtukane "mama yake" mpendwa (kama alivyomuita) ni zao la uchawa uliokomaa. Makonda amedhamiria kuwaharibia wenzake na kujikweza mabegani mwa mama yake ili mradi tu aonekane ni mwema na mtu mzalendo zaidi kuliko wengine.

Kusingekuwa na misingi ya uchawa iliyomwagiliwa, kuchipua, na kukomaa, Makonda asingeweza kuyasema aliyoyasema leo.

Lkn amesoma alama za nyakati na kugundua kuwa uchawa ndicho huwainua watu wengi ndani ya ccm na ndani ya serikali.....acha ajimwage.

Endapo "mama yake" atayafanyia kazi matamshi ya kichawa ya Makonda basi ni dhahiri kwamba watu wengi wasio na hatia wataumia.

Uchawa ni hatari kwa ustawi na.mustakabali wa nchi yetu.

Mzee umeumia sana kwa alichosema makonda, uzi wa ngapi huu?

Uchawa ulikuwepo toka enzi ndani ya chama na serekali, sema umepata umaarufu nyakati hizi.
Wala usishangae!

Uchawa umetokana na uwoga ulipitiliza (huu ulitengenezwa tokea miaka ya uhuru), today wame utulize woga huo, wanasiasa wamegundua jinsi ya kuutumia ili wafaidike kisiasa. Hawajali madhara yake kwenye jamii, jamii inatengeza watu wa hovyo rika zote
 
Kama taifa tumefanya kosa kubwa sana kuruhusu na kuulea uchawa. Kwamba mtu anayesifia na kujipendekeza kwa rais anaonekana ndiye mwema na mzalendo sana kuliko yule amabaye anapongeza kimya kimya ama anayekosoa.

Matokeo yake watu wengi wakaanza kuwa machawa na kuanza kushindana vikundi vya kukusanya umbea na kutoa sifa kwa rais. Mfano Samia Queens.

Tishio la Makonda kwa mawaziri wanaodaiwa kuwatumia watu wamtukane "mama yake" mpendwa (kama alivyomuita) ni zao la uchawa uliokomaa. Makonda amedhamiria kuwaharibia wenzake na kujikweza mabegani mwa mama yake ili mradi tu aonekane ni mwema na mtu mzalendo zaidi kuliko wengine.

Kusingekuwa na misingi ya uchawa iliyomwagiliwa, kuchipua, na kukomaa, Makonda asingeweza kuyasema aliyoyasema leo.

Lkn amesoma alama za nyakati na kugundua kuwa uchawa ndicho huwainua watu wengi ndani ya ccm na ndani ya serikali.....acha ajimwage.

Endapo "mama yake" atayafanyia kazi matamshi ya kichawa ya Makonda basi ni dhahiri kwamba watu wengi wasio na hatia wataumia.

Uchawa ni hatari kwa ustawi na.mustakabali wa nchi yetu.
Pole sana Mzee, mbona kauli ya Mhe. Imekutisha?
 
Alipiga naye picha Marekani.Naona Samia Chickens are coming home to roost. Huyo mwanamke alikuwa chawa wake.

Mtangulizi wake ametukanwa sana na huyo mwanamke, mitandaoni, wapinzani na alitukanwa na wengi ndani ya baraza lake la mawaziri, hajawahi kutoa tamko kukemea chochote.

Ndio kwanza alikuwa anachochea moto kwa kauli zake za kimafumbofumbo akionyesha kuwaunga mkono. Nchi imemshinda, taifa linazidi kugawanyika, maji tu shida kuyapata.
 
Makonda akimaliza miezi 6 kwenye uRC nitakunya kwenye daladala.
Ahahahahahahhaha nimekumbuka Mwijaku eti Simba ikifungwa atakunya mpaka posta, ebwanaee ngoja Simba aogelee magari jamaa na kazi akafukuzwa ahahahahahha
 
Frankly speaking, aliyoongea Makonda sio sawa kabisa, kwanza Mh. Rais wetu Mama Samia sio mama yake, pili kumchonganisha Mh. Rais na mawaziri wake tena hadharani mbele ya Mkuu wa nchi sio sawa kabisa, kama kuna mawaziri wanamtukana Mh. Rais ni kuchunguza haraka sanaaaaa na vyombo vipo kazini 24/7/365 every second vipo kazini na kuwafukuza kazi haraka sana, sio suala la kuongea hovyo kwenye umma.

Mh. Rais anaweza wakati wowote ule kumfukuza kazi mtu yeyote yule aliyemteua bila kuulizwa na mtu yeyote yule, ni barua moja tu na kumteua mwingine hapo hapo, sio sawa kusema hadharani wako mawaziri wanamtukana Mh. Rais, hata kama wapo ni kuwachunguza haraka sana na kuwatoa katika kazi haraka kabisa, hakuna kuchelewa, sbb huko ni kumhujumu Mh. Rais wetu.
 
Vipi kama yeye ndio kamtuma aseme hivyo?

Sikubaliani na lugha ya matusi anayoitumia huyu mwanamke wa Marekani lakini point zake zote ni za ukweli. Nchi imemshinda, teuzi, hovyo, huduma hovyo, mfumuko wa bei, kodi, tozo, huduma serikalini hovyo.

Ndio kwanza wanajiongezea marupurupu kwa wenza wa familia za vigogo, mara wanapanga wanunue ndege mpya kwa Rais. Uhuni, ufisadi, vurugu tupu.
 
Back
Top Bottom