Madhara ya usajili kufanywa na viongozi wa simba badala ya kocha

Sir robby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,396
Reaction score
4,080
Klabu ya SIMBA ilianza kufanya Usajili wa Wachezaji wake kwa Msimu wa 2022/2023 mara tu baada ya kuachana na KOCHA wao.Wapenzi wa Soka tuliamini Mtu mwenye Upeo na Ujuzi wa kujua ni Wachezaji gani wanahitaji ni KOCHA.

Uongozi wa Klabu ya Simba kupitia Kamati yake ya Usajili ilianza Mchakato huo huku wakiwa hawajampata KOCHA MPYA. Mpaka Kocha anapatikana tayari Klabu ya Simba ilikuwa imefanya Usajili na kumkabidhi Kocha Mpya wachezaji.

Matokeo ya Usajili kufanywa na Viongozi Yameonekana tarehe 13/8/2022 Uwanja wa Mkapa kwa Kufungwa na Watani wao YANGA waliofanya Usajili wao Chini ya KOCHA wao.

Katika Mechi hiyo Mapungufu makubwa ya Wachezaji wa Simba yalionekana hali ambayo itakuwa ni ngumu sana kwa Simba kufanya vizuri ktk Mechi zake za ndani na nje.

Wakati umefika kwa Klabu ya SIMBA kuwatumia Makocha wake kwenye USAJILI wa Wachezaji wake.
 
Hapo siwalaumu kwani kipindi cha usajili kiufupi mno na mchezaji mpaka kusaliwa sio kama kwenda gengeni kununua nyanya na timu ikichelewa kidogo utakuta wachezaji wote wa maana wamechukuliwa.

Ninacholaumu mimi ni kufukuza makocha hovyo angalau angekuwepo kocha toka mapema u yule wa msimu ulioisha angerekebisha mapungufu ya msimu uliopita mapema kwakua alipata muda wa kutosha kukaa na kikosi na kuisoma ligi vizuri.
 
Unless hujui mpira kabisa, ila game moja huwezi kufanya conclusion ya kishamba namna hiyo. Kwa hiyo Man U kapigwa mbili so kwa tafsiri yako anashuka daraja? ama hana kocha siyo.

Huwezi ku-rate kocha ama kiwango cha mchezaji kwa game moja ndugu. Tatizo la Tanzania hapa kila mtu anajua kuchambua mpira.
 
Ulitaka afungwe nani yaani, hivi nyie makolo mnajiona kama mna haki pekeyenu ya kuwa na furaha kwenye nchi hii, na bado mtafungwa sana mpaka pale mtakapo acha kubebwa na TFF yenu, yaani kiufupi hamfungwi makolo tu bali mpaka TFF inaugulia maumivi huko ilipo na raisi wake.
 
Yaani sasa hivi ndio tutajua magonjwa ya akili yako wapi. Kwanini nyie kwenye bongo mmeweka akilini kushinda tu, ifike wakati mkubali kuna kupoteza.

Sasa hivi mnalalama mambo ya usajili na vipi mlipopoteza kwenye FA nako sababu ilikua ni kwa sababu kocha hakusajiliwa wachezaji wake. Mbona mlishinda kwa St. George na hatukusia haya

Hata iwejw kufungwa huwa kupo tu mashabiki wa Simba kubalini kiubora bado rekebisheni kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kocha mpya wachezaji wapya. Ni muda Sasa Simba wajifunze kukaa na kocha hata misimu mitatu, haiwezekani Kila msimu unakocha mpya.
 
Ni mapema sana kusema kikosi ni kibovu kwasababu ya mechi moja.Timu ilicheza vizuri sana yaliyotokea ni makosa tu yakiufundi ambayo niyakawaida.

Ata simba ingeshinda bado mashabiki wa yanga wangesema wana kikosi kibovu.Tuupe muda nafasi utatujulisha vizuri.
 
Kwani ile safari yao ya kujinoa kule Misri Ilikuwa mandonga??
 
Nakazia mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…