Ajibu hajawahi ichezea Yanga hata hao kina BoKo na Manula bado hawajaichezea simba. Hapa lawama zianzie TFF kwa kuzibeba timu hizi mbili hata ligi kuwa ni ya simba na Yanga. Lawama hawazikwepi maana kila siku huwa tunapinga maamzi ya marefa watanzania kulalia timu ndogo. Kama matimu hayatapendelewa tutawapata wachezaji wenye uchungu na Nchi yao.
Pool of the National Team / terms /mafao
Kuna factor moja mnaisahau: Kuna kosa kuwa na pool ya timu ya taifa? ambayo iwe na ratiba ya kudumu mwaka mzima angalau wiki moja ya kambi kila baada ya 3 months? allowance ya kudumu kwa mwezi kwa wachezaji wa kwenye hiyo pool kuna kosa gani? mpira ni ajira!.
Ratiba ya soccer activities kwa mwaka, usajili na mashindano, haviendani !
Tanzania/TFF hawana timing nzuri. Kwanza tunajua vuguvugu la usajili lina affect vipi performance kwenye aidha klabu na timu ya taifa? Hivi mpaka sasa, ukiwacha wale waliosajili tayari, kabla ya kusajili ilikuwa ni presha ya kuachwa au kusajiliwa, afu na nani? nchini au nje, yote haya yana impact kwenye performance! angalia Banda: simba au Afrika Kusini, msuva: yanga au morrocco, muzamiru sjui...n.k., nyoni mara yanga mara simba, ni shida! hata maguri anaweza rudishwa? kupata timu SA etc. Tunafikiri hawa wachezaji wanaweza buruzwa vyovyote nao waka perform sawa sawa, si rahisi.
Physical state ya wachezaji
Hivi kusafiri na ndege hapa na pale hakuna fatigue? yaani uchovu. Ile safari ya egypt kuweka camp ili ucheze ndani ya 1 week Dar es Salaam afu maelezo eti hali ya hewa ya egypt ni kama ya dar? si dhani kama ni kweli!, haya, uende SA 2 WEEKS, urudi Dar, upewe likizo sijui siku 2 afu flight kwenda mwanza, afu flight au kwa gari kigali yalijulikana mwanzo au walijulishwa in short notice? haya yote si yanataka matayarisho ya kisayansi na kisaikolojia? nafikiri hata structure za kamati za TFF nazo mbovu. Hivi apart from TFF kuna kamati nyingine ya ufundi, specific for the National Teams; achana na zile ad-hoc committees za ushindi kama ya serengeti boys! sizidharau lakini timu zikishindwa hawaonekani kutoa maelezo, wanawaachia wakina Geofrey Lea na wachambuzi wengine wa TV!, Kusaidia kueleza the probable mechanisms behind failure.
Mikakati maalumu kwa mashindano
Kuna nchi jirani nawajua huwa wanavizia wakijua Chan imekaribia, kuna wachezaji wanawatafutia local teams, na wanafanya espionage za timu zote zinazoshiriki kundi moja. Swali hivi waganda kuchezesha mchezo ambao mshindi yuko likely kukutana na uganda iko sahihi? au kanuni haziendi mbali kiasi hicho? samahani kwa kutafuta kisingizio. Banda alishindwa nini kungojea wiki mbili tuwakungute hawa ndiyo aondoke! walikuwa wanafunga usajili kule? au simba na TFF hawaelewani?
Generally, Mayanga siyo mbaya, anahitaji Coach more senior na more exposed kuwa juu yake. Maximo tulilipiwa na JK USD 10,000 kwa mwezi. Hivi hizo pesa ni nyingi sana mpaka leo? Si tutafute kocha mwingine duniani hapa hasa East Europe au mwafrika?
TFF Kujihusisha na vitu ambavyo labda vina maana lakini siyo kipaumbele au priority
Hivi TFF kujifanya wanahuzunika Zanzibar kukosa uanachama ni ukweli au wanajibaraguza. wanaweza kutueleza nini walikuwa wanatafuta kwa zanzibar kuingia CAF au FIFA kinachohusiana na majukumu yao. Kwangu mimi ile ni ishara kuwa TFF haina faida kwa mustakabali wa soka Z'bar na ni jambo la kunyamaza tu na kujirekebisha, ikiwezekana kubadilisha hiyo image. Sijui vizuri ila nahisi kwa Zbar hiyo nayo ni kero ya muungano. TFF wanahusika na kero hiyo ambapo kazi yao ingekuwa kui address ili wa zanzibari waifurahie na sio vinginevyo!