jukumu la waliolimika hasa kwa kweli ni kusaidia wengie au kusaidiana nao kutatua mataizo
philosophically, kuna njia mbili ya kwanza ni kumkomba mwanadamu na ya pili ni kurithisha tu yale ya vizazi vilivyopita. Kwa hiyo wasomi wanapaswa kujitahidi kuwasadia watu wajikomboe. labda swali linakuja KUJIKOMBOA ni nii? au kunahusu nini?
Kujikomboa ni uwezo wa mtu kudhibiti dhamira namatendo yake, uhuru wa kufikiri ktk kufanya uamuzi juu yake, jamii na mazingira yake. UKOMBOZI huo ni kunahusu uhuru wa fikra, kutenda na wajibu wake ikiwemo kuelewa athari za vitendo vya mtu katika jamii.
Lakini kuna uwezekano kwamba mtu anaweza maliza shule lakini hajajikomboa.
Kulingana na Mtazamo wa William James, alizaliwa 1842, ambae ni Mwana Falsafa na Mwana Saikolojia: Alisema kwamba-
"Kuna namna mbili za maarifa. Nazo zinatofauti dhahir. Tunaweza kuziita kua ni
Maarifa ya kitambulisho, na Maarifa ya kuhusu". There are two kinds of knowledge broadly and practically distinguishable. We may call them respectively Knowledge of Acquaintance and Knowledge-About. [William James, Psychologist & Philosopher b. 1842].
Nikisherehesha alivyosema James, ni kwamba
MAARIFA YA KITAMBULISHO ni maarifa ya kutambua elimu bila kufahamu kuhusu elimu hiyo. Kwa mfano: Mtu mwenye elimu ya kitambulisho anaweza kuhitimu na akapata shahada, lakini hana ufahamu wa kuhusu maarifa hayo. Kwa mfano mtu ana shahada ya uchumi, na alifaulu vema, lakini hawezi kutumia maarifa aliyoyasomea katika maswala ya uchumi. Kwa hiyo huyu mtu ana maarifa ya kitambulisho.
MAARIFA YA KUHUSU, mtu mwenye maarifa kuhusu elimu, anafahamu kuhusu yale alie yasomea. Kwa mfano: Mtu mwenye elimu kuhusu uchumi, hata kama hana shahada, anafahamu maswala ya kuhusu uchumi.
Kwa maana hio, mwenye maarifa ya utambulisho, haitumii maarifa yale katika kufanya maamuzi hasa yanayohusiana na kile alichosomea. Ni kama vile alivosema PLOTINUS Philosopher aliezaliwa 205 C.E katika First Ennead II.
Plotinus alisema kua "Maarifa ikiwa hayato amua kitendo, basi ni maarifa yaliyo kufa" Knowledge if it does not determine action, is dead to us. [Plotinus, Philosopher b. 205 C.E]
SWALI linalonijia ni kwamba, ikiwa watu wenye elimu wana jukumu la kufundisha wengine (kama ilivoandikikwa na mdau), Maarifa yanayopatikana ambayo ndio lengo la elimu, ni jukumu la nani kuamua elimu ya aina gani mwanafunzi aondoke nayo kutoka shule?