ibada ya jumuiya ni ibada kamili mbele za Mungu kama zilivyo ibada nyingine.
Tofauti ya hii inakuwa inahusisha zaidi watu /familia wenye imani dhehebu moja,usharika mmoja ila mnaoishi eneo moja familia za jirani au mtaa mmoja.
FAIDA ZAKE.
1)Ibada mbele za Mungu umuhimu wa kusali kwa uzito na faida zile zile za ibada kama ilivyo ibada nyingine au ibada ya juma pili kanisani.
2)kushirikiana katika jamii,mahusiano mema,ujamaa,kusaidiana,kuunganisha jamii majirani wa imani moja,kujenga umoja na mshikamano upendo na ujamaa katika shida na raha.MIPANGO mikakati ya kusaidiana ikihusisha kutunisha mfuko wa jumuiya wa kusaidiana kushikana mkono katika matukio ya furaha na huzuni,ikihusisha kuchangiana kwa hali na mali
3)kushiriki shughuli za maendeleo ya kanisa/dhehebu ikihusisha kuchangia hali na mali
4)kusaidia wahitaji katika jamii ambao nje na ndani ya jumuiya udiakonia mfano wagonjwa,wahitaji masikini,walemavu,yatima,wafungwa,
KUHUSU MICHANGO
ipo ya aina mbili
SADAKA
safaka zipo zinazoenda kanisani kujenga/shughuli za kanisa ambazo zinatolewa kwa jumuiya
MICHANGO ya mfuko wa jumuiya kwa ajili ya kusaidia wanachama shida na raha na kazi za jumuiya.
Michango kwa ajili ya kusaidia wahitaji kwenda kuwatembelea na kuwasaidia walemavu,wafungwa wagonjwa,yatima n.k hapa unachanga fedha au mali au vitu,pia kuna kuwahudumia kama wagonjwa wasiojiweza unaweza ukatoa huduma pia
Pia kuna shughuli hata zamu za usafi wa kanisa hufanywa kwa jumuiya n.k
HITIMISHO
SADAKA NA MICHANGO yoyote au hata msada wowote kanuni ya kutoa UTOAJI iwe kwa jamii (wahitaji wanyonge wasiojiweza) au sadaka kwa madhabahuni kwa Mungu inataka mtoaji atoe kwa moyo wa shukrani,kwa kupenda kama alivyokusudia mwenyewe kutoka moyoni mwake KWA KUPENDA si kwa lazima wala kwa huzuni.
Sadaka ikitolewa kwa manung'uniko na malalamiko/huzuni inakuwa ni laana badala ya baraka.NI BORA kuacha kutoa kama moyo wako hauna amani ya kutoa.
ILA JUMUIYA SIYO KITU KIBAYA
Na jumuiya ni kitu ambacho ni utamaduni wa kijamaa hasa kwa sisi jamii zetu bado zina element ya mfumo wa kijamaa,ndio mana unaona vikundi vingi vya kijamaa mfano vikoba,waliosoma shule moja,wanaotoka mkoa mmoja wafanyakazi wanaofanya taasisi moja,kabila moja ,kuna vikundi vingi hata watenda dhambi wana vikundi vyao vya umoja wa watenda dhambi.VIKUNDI VYA UMOJA ,hizi JUMUIYA sio kitu kibaya ,mfano kuna umoja wa boda boda huwa wanasaidiana sana boda mmoja anapopata tatizo.
JUMUIYA NI KITU POSITIVE SANA sio kitu kibaya.