Mfano halisi usharika wetu ni mpya mwanzo tulikuwa tunasali kwenye jengo la mabati matupu juu mpaka chini mabati matupu.Sasa tumepata neema tumejenga kanisa la matofali tumepaua tupo kwenye hatua ya madirisha...madirisha yapo kuminna jumuiya zipo kumi kila jumuiya ina familia sizizopungua 5 kila jumuiya tumekubalina ichangie dirisha moja
2)lakini hapa ni mjini ukienda vijijini ndio kuna baadhi ya wenzetu wanasali chini ya miti au kwenye majengi ambayo hayajapauliwa hivyo mvua ikinyesha ibada ina hairishwa.Uchumi wa vijijini ni mdogo lakini wale ni ndugu zetu katika Kristo kama,hivyo kila jumuiya tumekubaliana tuchange kwa ajili ya kusaidia kupaua makanisa ya vijijini
3)kila mwezi huwa tunachagia mfuko wa jumuiya kwa ajili ya maafa ,kuuguliwa,mwenzetu akiuguliwa aunakipata tatizo ikiwemo msiba mnatoa kwenye mfuko mnamshika mkono.
4)sadaka tunazotoa siku ya jumuiya nusu zinaenda kanisani nusu zinabaki kwenye mfuko wa jumuiya
5)Lakini pia huwa tuna utaratibu wa kwenda kuwasaidia na kuhudumia wahitaji wanyonge either wafungwa,wagonjwa vituo vya yatima n.k
KUNA BARAKA KATIKA KUTOA (kusaidia wahitaji wanyonge au sadaka madhabahuni)KULIKO KUPOKEA.
Mwisho wa siku MUNGU ni tajiri dunia na vyote viujazavyo hata na sisi ni mali yake,sio kwamba Mungu anahitaji sana sadaka zetu,pia kusaidia wanyonge AU KUTOA SI LAZIMA NI HIYARI haitakiwi ulazimishwe na hautakiwi utoe kwa lazima.
FAIDA YA KUTOA SADAKA AU MISAADA AU MICHANGO ni kwa mtoaji mwenyewe anayetoa ndio anapata baraka/thawabu kutoka kwa Mungu.