Madini na rasilimali nyingi ni mapambo kama huna watu sahihi. Tunatakiwa tufumue upya mfumo wetu wa elimu

Madini na rasilimali nyingi ni mapambo kama huna watu sahihi. Tunatakiwa tufumue upya mfumo wetu wa elimu

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Ndio maana nchi yetu wanaotajirika zaidi ni wahindi, waarabu, wakenya, chinese, n.k. sisi tumebaki kujisifu nchi yetu tajiri lakini hatunufaiki na huo utajiri, imahine majirani Kenya ndio wanajulikana zaidi kuuza maparachichi nje kumbe wanayatoa huku kwetu, madini ya Tanzanite dili ndefu zinapigwa Kenya, wahindi na waarabu wapo levels za mbali mno, makabila yenye asili yetu tunayosifia hawagusi.

Kwa kuanza kabisa system ya elimu itinduliwe upya.

Lugha inayotumika iwe ni kiingereza levels zote kuanzia chekechea hadi chuo na ikiwezekana walimu waletwe wakenya na waganda, sijaona pottential ya walimu wetu, lugha wanaifudishia ubaoni hawaiwezi. kiswahili libaki kuwa somo na lugha ya taifa.

Form 5 na 6 zifutwee, ni elimu za kikoloni, hazina taaluma yoyote ndio maana hakuna ajira ya form 6, tunahitaji vijana waanze kujifunza taaluma husika baada ya form 4, hakuna muda wa kupoteza.

Elimu ijikite kwenye kufundisha wanafunzi ku exploit rasilimali zetu huku nguvu kubwa ikitumika kwenye mafundisho ya vitendo na field za kupata uzoefu, wanafunzi wajifunze kilimo cha mbao, kuchimba madini, ufugaji wa nyuki, n.k. nchi yetu ina rasilimali nyingi sana tujikite humo humo kwenye elimu,

vijana wawe encouraged kutoka nje ya nchi, exposure ni muhimu sana
 
Ni rahisi sana kuongea na kushusha lawama kwenye mfumo wa elimu tukidhani ndiyo unaoleta matatizo yote haya tulionayo. Ukweli ni kwamba mfumo wa elimu ni kisingizio tu.

Mchawi mkubwa wa nchi yetu ni MFUMO WA UTAWALA. Kwenye mfumo wetu wa UTAWALA, siasa ndiyo inaongoza masuala ya kitaaluma, wakati ilipaswa kuwa kinyume chake.

Madhara ya mfumo huu ni kwamba kila kitu kipo kisiasa (kinakuwa bandia, yaani kinafanyika kwa lengo la kuleta umaarufu wa kisiasa tu.

Wachina, wajapani na wakorea wametoboa kwa lugha zao. Why Tanzania iwe nongwa kutoboa hata kwa hiki hiki kiingereza cha kubabia?

Kuondoa rushwa, kuajiri kwa vigezo vya ujuzi (meritocracy), kuondoa wizi wa fedha za umma, kuondoa upendeleo ktk teuzi, n.k vyote hivi havihitaji kiingereza .
 
🤝🙏
 
Back
Top Bottom